Atumia mtandao wa Facebook kuwalawiti wanafunzi wenzake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Atumia mtandao wa Facebook kuwalawiti wanafunzi wenzake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Feb 10, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  Atumia mtandao wa Facebook kuwalawiti wanafunzi wenzake


  Anthony Stancl Tuesday, February 10, 2009 8:21 AM
  Mwanafunzi mmoja aliyejifanya msichana anayetafuta mpenzi katika mtandao wa Facebook na kuomba picha za utupu za wanafunzi wenzake na baadae kuwatishia kuzisambaza shule nzima picha hizo wasipokubali awalawiti amekamatwa baada ya kuwalawiti wavulana 7
  Taarifa zilizotolewa zilisema kwamba Anthony Stancl mwwenye umri wa miaka 18 alijifanya msichana katika mtandao wa Facebook na kujaribu kutumia kila njia kuwavutia wanafunzi wenzake ili wamtumie picha zao za utupu na baadae kuwatishia wanafunzi hao kuzianika picha zao shule nzima iwapo hawatakubali matakwa yake.

  Stancl mkazi wa New Berlin Wisconsinite, nchini Marekani amekamatwa na anashtakiwa kwa makosa ya kujifanya msichana,kubaka, kuwatishia wanafunzi wenzake wa kiume na kumiliki picha za ngono za watoto.

  Stancl alianza mchezo wake huo mwaka 2007 baada ya kujisajili kwa jina la kike katika mtandao wa Facebook akijiita Emily na kuweka picha nzuri za kike akijifanya yeye ni msichana aliyekuwa akitafuta mpenzi.

  Kwa mujibu wa polisi, baada ya kupata picha hizo za wanafunzi wenzake wavulana Stancl aliwatishia kuzisambaza picha hizo shule nzima na kuwataka wafanye naye mapenzi.

  Stancl alifanikiwa kupata picha za utupu za wanafunzi wenzake 31 na alifanikiwa kuwalawiti wavulana saba kati yao.

  Inasemekana Stancl alifanya uovu wake huo kwenye mabafu ya shule, sehemu za kuegesha magari na wengine alidiriki kwenda majumbani mwao na kuwafanyia uovu wake huo.

  Mtandao wa Facebook umewataka wanachama wake wawe makini na marafiki wanaojiunga nao kwenye mtandao huo na imeahidi kutafuta njia za kuzuia matatizo kama hayo yasitokee tena baadae.
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...na wao walitaka tu kulawitiwa,...:( mtu anaona bora alawitiwe kuliko kusambazwa picha yake ya utupu? mwehu nini huyo?
   
 3. killo

  killo JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 393
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45

  Eti kisa picha tuu, pic zenyewe ziko kwenye facebook inwhich they dont allow any explicit material anyway , otherwise facebook themselfves would have them down as of immediately
  Y worry for the school to know???? hence almost 99% of the kids at school have internet access on phones, home, school labs.....! I dont get it :confused:
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ehhh, Banana Zorro anaimba "Mambo ya kizungu.."
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Feb 10, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ni hapo sasa...! Aah! Siajabu ukakuta hao walio lawitiwa wana chembe chembe za ushoga...!

  Kama ni picha tu na azianike... zikikauka si zita anuliwa...!? Tatizo liko wapi!?

  Kwanza kwa nchi za Ulaya na Marekani kuonekana ukiwa mtupu wal si jambo la ajabu. Otherwise hizo picha nazo zilikuwa zimekaa kishoga shoga!
   
 6. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  sijui tunaelekea wapi jamani.
   
 7. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hamna mbona ni ajabu usione kwenye mapicha lakini na wao wanatazama pia ,demu akikatisha au akivaa viguo vya kuonyesha maungo wanamtazama na kurusha rusha maneno, ndio maana kunaongoza kwa ubakaji.
   
 8. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2009
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,025
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Kaaaazi kwelikweli kwani huo ndio wehu na uendawazimu wa watu weupe. Yaani heri kulawitiwa kwani itakuwa siri baina yenu kuliko picha zako za uchi ziwe mtaani, hii ni ajabu na kweli
   
Loading...