ATCL: Another Richmond!

ATCL: Another Richmond!

Koba,
Kwa nini serikali ijenge viwanja?...Why not hizo kampuni zijenge viwanja zenyewe maanake tunauza kila kitu kulingana na mifano yako.
 
Sioni faida ya shirika hili,kama mengine tulikuwa nayo ambayo yalikuwa yanatuingizia faida tumeuza na migodi yenye thamani tumekodisha na tunapata upumbavu,nini maana ya kuwepo kwa ATC? ni dhuluma tu. Sekta hii tuwaachiae watu binfsi wafanye kazi, kwani tumeona ujio wa community airline sisi wakazi wa mwanza tumepata unafuu mkubwa sana. enzi za ATC na precission, safari ya saa moja na robo ilikuwa Laki mbili na miatano, leo ndani ya community ni 89,000/= kwa safari hiyo hiyo. ATC wezi wakubwa ovyooooooooooooooooooooooooo
 
"The leasing of the 150 seater plane will cost the company 370,000 US dollars every month, which according to the ATCL Chief Financial Officer; Mr Eliasaph Mathew will boost the net contribution to the company operations. He said that in the first 12 months of services ATCL projects to record a total revenue of 1.7 bn/-, while during the second year the company will realise some 3.5 bn/-."

Du mi nna tatizo na hizi revenue na lease figures. Kukodisha kwa mwaka 1 inacost USD.4.4 Million, wakati revenue ni only Tzs. 1.7 Billion hata the 2 year revenue ni Tzs.3.5 Billion.This does not make any sense to justify leasing this plane. Maana hata hawataweza kubreak even.

Halafu ATCL kwa uwezo wao wa sasa ni bora wangeconcentrate kwenye local routes. Hii ndege kuipeleka Dubai, South Africa, India na Kuwait, mi nadhani ni kosa kubwa mno maana hizo routes zina ndege za uhakika na mashirika makubwa kama Emirates,Qatar, KQ, SAA,Ethiopia Airline etc.
 
Mbangaizaji kweli hapo umefanya simple and quick analysis ambayo unajua umefungua macho yangu kiaina kwenye hii maneno hapo kwenye revenue..... Mkuu umeona ambacho wengi hatujakiona manake tukumbuke kuwa dege hili pamoja na kulilipia hizo njuruku (US $ 370,000) according to ATCL, still tumeshachangia mengi (sina uhakika ni kwa kiasi gani lakini yote ni kwenye ufufuzi wa mighty, formerly about dead Jamaican Air A320).

Kwenye hii thread hapo nyuma:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=9508&page=3

nili comment kwamba tuangalie among other things kwenye shirika letu tukuka "MIKATABA YA HIZI NDEGE ZA KUKODI", na hapo Mkuu umeshaonyesha wasiwasi nilikuwa nao kwenye huu mkataba ndugu yangu. Kwenye huu mkataba nadhani kuna vipengele ambavyo vimehusishwa vikiwemo malipo ya wafanyakazi (crew – manake ni wet lease hii, so I hear), maintenance, pre-deployment checks and other maintenances (thread inaonyesha kuwa kuna malipo ATC imeshafanya), na malipo mengineyo zikiwemo "bond" nk….. Sasa hawa waheshimiwa wa ATCL mnaosoma hii thread (najua mpo ndugu zetu) hebu tuambieni mliweka hayo manake hapo juu Mbangaizaji aliyoweka hapo juu kwenye "cost-benefit analysis??".... Manake hata kwenye original article ya kwenye gazeti as per MKJJ inaonyesha hata currency inayotumika haijaonyeshwa (apart from malipo ya mwezi ya US $ 370,000)... Au ile Annual revenue" ya 1.7b ni US $, manake huwezi jua bwana BONGO hii…

By the way, ATCL bado mna zile "Complimentary tickets" za kina baba, bibi, shangazi, mjomba, vimada etc manake pamoja na competition ya makampuni mengine kwenye ruti pia kuna competition ya ndani baina ya wafanyakazi kusafiri bure, kaazi kweli kweli hapa nchini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Bottom line is hii kitu lazima iangaliwe manake isijekuwa ni mkenge mwingine......Panapofuka moshi…….

Naomba kuwakilisha....
 
Unajua wakuu ATCL ni shirika letu ila nathani kwenye hili la kuleta A320 under lease si uamuzi mzuri hata kidogo

Mi nilitizamia kwa shirika la ndege lililopata hasara ya zaidi ya over Tzs. 24 Billion in the last 5 year. Walitakiwa wabadilishe stategy ya biashara. Airbus A320, inaweza kutua kwenye viwanja vingapi hapa kwetu. My guess ni Dar Kia, Mwanza na Mtwara tu. ATCL kama carrier ya Tanzania ilitakiwa kwanza kuwezesha usafiri mzuri wa Anga within Tanzania.Sababu kubwa kwa hili ni:-
1. Routes za Tanzania zinalipa sana maana Dar- Tabora, Dar -Kigoma, Dar -Mwanza ni chini ya Tzs. 160,000 return ticket. Na hii ni baada ya kuja Community Air, before ngoma ilikuwa over Tzs. 300,000. Wakati Dar - Dubai ni kati ya USD. 500- 700, na hii ni trip ya masaa 6 sio 2 ya local flight. Halafu competition sio kubwa kwa local routes especially za kama Tabora,Kigoma,Arusha,Bukoba,Dodoma,Mafia etc.
2.ATCL inahitaji ndege ndogo kama za watu 50 - 75 ili ziweze kutua kwenye hivi viwanja vidogo kama ATR-60,72,au Dash 8 Q ambazo wanasema wanampango wa kuzileta.

The fact remains kuwa ATCL haina muscle ya kukompete kwenye International routes kwa sasa maana hata Community Airline na Precision Air zinaipeleka mswaki.

Huu ni ushauri tu tusianze kujaribu kukimbia wakati hata kutambaa hatuwezi
 
Mbangaizaji..... umenena Mkuu!!! Unajua tatizo ni kwamba zile routes wakati ule zilikuwa na faida sababu competition haikuwa kubwa... Sasa hivi with India na China (Hong Kong and mainland) kuwa ni kitovu cha wafanyabishara wa Middle East na African regions ni kwamba hata wale waliokuwa hawana ndege/ruti nyingi wame multiply... Angalia Emirates, Qatar,ET, KQ na wengine weeengi wana flight daily to Dar..... Chukua routes nyingine za huku ulaya na americas kule napo watu wanafuata cheapest (EgyptAir etc) au Exec (KLM/BA etc).... Sasa hapo mimi binafsi nadhani ATCL itawachukua sio chini ya 2 years ya good service kuwezxa kupata "clientele" ya kuringa, meaning kuna loss making/kujitembeza for a minimum of 2years - Could ATCL try that, hakuna kitu hapo......

So back to the point ni kwamba kama ilivyokuwa TANESCO,IPTL,Richmonduli,Buzwagi na mengine meeengi hili nalo laweza kuwa booomu nambari elfu!!!!

Mungu Ibariki Tanzania na watu wake!!
 
0080941.jpg


Kwa safari za Kigoma, Tabora, Zenj, Mtwara na Mbeya
 
Waheshimiwa,nimesoma kwenye gazeti la The Citizen leo,na Mattaka anasema hio 1.7b ni NET PROFIT....will quote the exact wording.."On the company's business outlook in the forseeable future,Mr Mattaka said ATCL expected to make a net profit of shs 1.7 billion during the first twelve months of operations,this profit is expected to grow to shs 3.5 billion after the airline takes possession of the airbus..."
 
Koba,
Kwa nini serikali ijenge viwanja?...Why not hizo kampuni zijenge viwanja zenyewe maanake tunauza kila kitu kulingana na mifano yako.

...viwanja ni infrastructure za nchi kama bandari,barabara au madaraja ambazo zinahudumiwa na pesa za walipa kodi na viwanja vya ndege sio kwa sababu ya profit ndio maana viwanja vingi duniani ni mali ya serikali,jeshi,city au municipal na viko pale kwa ajiri ya kusupport shughuli za kiuchumi/kijeshi lakini sio profit,uhusiano wa mashirika ya ndege na viwanja ni landing fee na kodi nyingine kama storage etc lakini haviingiliani kabisa
 
Ngoja tuuweke na huo mkataba wao wa ATC na Wallis Trading hadharani...

...hebu uweke maana nimeshanusa ufisadi hapo na kahistoria ka huyo mkuu wa hilo shirika kamegubikwa na ufisadi fisadi tuu,najua lazima kuna rushwa tuu na utapeli hapo,kama EL tumeweza kumfukunyua kwa rushwa hivi vidagaa kina mattaka tutaweza kuvi handle tuu na kufukuzia mbali hawa mafisadi
 
Sioni faida ya shirika hili,kama mengine tulikuwa nayo ambayo yalikuwa yanatuingizia faida tumeuza na migodi yenye thamani tumekodisha na tunapata upumbavu,nini maana ya kuwepo kwa ATC? ni dhuluma tu. Sekta hii tuwaachiae watu binfsi wafanye kazi, kwani tumeona ujio wa community airline sisi wakazi wa mwanza tumepata unafuu mkubwa sana. enzi za ATC na precission, safari ya saa moja na robo ilikuwa Laki mbili na miatano, leo ndani ya community ni 89,000/= kwa safari hiyo hiyo. ATC wezi wakubwa ovyooooooooooooooooooooooooo

...Mkandara soma hapa!
 
Daily News

AIR Tanzania Company Limited (ATCL) is expected to resume its operations in Africa, Middle East and India next month, using a wide body aircraft leased from Air Jamaica. The Managing Director of ATCL, Mr David Mataka has said the nation’s flag carrier will start flying its newly leased aircraft A320-11 Airbus to South Africa, Dubai and Kuwait routes.

The newly leased plane however is expected to arrive in the country in early March, he said. “We are in the final touches to secure the government’s guarantee which should be ready by next week, in order to conclude the leasing of the aircraft which is to start its maiden operations next month,” he said.

The leasing of the 150 seater plane will cost the company 370,000 US dollars every month, which according to the ATCL Chief Financial Officer; Mr Eliasaph Mathew will boost the net contribution to the company operations. He said that in the first 12 months of services ATCL projects to record a total revenue of 1.7 bn/-, while during the second year the company will realise some 3.5 bn/-.

Earlier, the Airline could not compete as its planes lacked the capacity to carry passengers and cargo simultaneously and was forced to drop one of the two in some destinations, to allow the planes instead to carry more fuel, Mr Mathew said. “We will be able to carry passengers not only to Dubai, but to other destinations like Mumbai, India without worries of overload which previously had led to losses,” he said.

Mr Mataka further said in the first month of operations, the aircraft would be on a wet lease which means both the pilots and crew will be hired from abroad. As soon as the ATCL personnel complete training, they will take over from the foreigners to continue with the running of the aircraft.

Mr Mataka also refuted reports that the leased plane was “not airworthy ”, saying it was only eleven years since it was built, “which is a very young age for an aircraft, even for those being operated by international airlines”. He said most of those aircraft had been in operation for more than 16 years.

He further said most of aircrafts currently operating in the country were more than 30 years old and “still working perfectly”. He added that the plane has also been checked by US Airbus company in collaboration with the local experts, who have established that its aviations' landing gears and engine were in tip top condition.

Meanwhile, ATCL has already acquired two Canadian manufactured Dash 8Q 300 planes owned by a British company that will start operations by the end of February. According to Mr Mataka, the low level noise aircraft with capacity of 60 passengers each will be used on domestic routes. This brings the number of ATCL planes to 5, he said. He sad that the planes would ply Kigoma, Shinyanga and Tabora routes. Other routes include Mwanza, Kilimanjaro and Mtwara.

My Take:

Wakifikishwa mahakamani ndipo watakapoimba!

Nimesoma hii taarifa ya ATCL najaribu kuipitia haraka iwezekanavyo ili niweze kutoa mchango wangu (if necessary).
Kwa bahati mbaya sana sina information zilizopelekea kuandika hizo projection kwa vile nipo safari nje ya nchi kwa wiki mbili sasa. Lakini nitajitahidi kuchangia kwa yale ambayo ni obvious.
 
Haya mzee tunasubiri input yako. Binafsi natafuta namba ya Mataka ili tuweze kuzungumza kindugu (wote tunatoka Mfaranyaki, pale penye bomba hii nyumba hii)
 
Habari wana Jambo,

Nimesoma hii topic na nina hoja na maswali kwa wanajambo wa viongozi wa ATCL:

1. ATCL itapata widebody aircraft kutoka Air Jamaica.
Air Jamaica currently wana operate 2 widebody aircraft katila route ya Jamaica - London. But wanaidrop hiyo route kwa ajili ya profitable reasons. Hizi ndege mbili mpaka muda huu Zishauzwa kwa Turkish Airline ambazo watazipata April 2008 sasa hii taarifa inatia wasi wasi yale ya mahujaji yasije yakatokea tena.

2. A320- 100 , hiyo ndiyo version wa kwanza ya Airbus A320 series, ingawa mashirika yanayo operate hiyo ndege limebaki Air france wanazo more than 20. na last year British Airways wali retire ya kwao ya mwisho. Hivyo haimanishi hiyo ndege ni ya zamani au sio fuel efficient, la hasha wanazi retire because kuna more effient A320 series A320-200. A319, A318 na A321.

3. Q400 na Dash 8- 300. hizi ndege ni efficient especially Q-400 iko faster than any other turbo propellor.na Incident ya SAS Scandinavia Airline ni Kwa SAS tu haijatokea kwa mashirika mengine na hiyo inareflect Maintananc hanger yao especially ya Q400 ni mbovu. Kwa sababu mashirika Makubwa yana operate na hawana matatizo yeyote na nitayaorodhesha.

Air Nippon Network (14)
Augsburg Airways (5)
Austrian Arrows (10)
Continental Airlines(Colgan Air) (4 with 11 on order)
Croatia Airlines (4 on order)
Flybaboo (2)
Flybe (35, 25 on order)
Frontier Airlines (Lynx Aviation) (10)
Horizon Air (33)
Japan Air Commuter (11)
Jeju Air (4)
Luxair (3)
Porter Airlines (4, 6 on order)
Royal Jordanian (1)
Scandinavian Airlines System (24, all grounded) [20]
QantasLink (7,12 on order)
Tassili Airlines (2, 6 on order)

kati ya hayo ni SAS ndiyo walio ground hizo ndege.

4. Mzee mwanakijiji hizi taarifa kila siku ndege inakuja next month zitaisha lini? hawa viongozi hawaoni wanajishushia hadhi
 
Mimi nasema ni kichaa kapewa rungu sokoni, sababu Mattaka anajulikana mitaani kuwa ni tapeli, Fisadi na mzinzi mkubwa, inasemekana kuwa alifanya vizuri PPF lakini ikumbukwe kuwa PPF ilikuwa kama bima tu , mashirika yaliweka akiba za baadaye za wafanya kazi wake, haikuwa biashara yenye competion kama biasha ya usafirishaji wa anga. huyu bwana hana business experiance, tuombee ATCL Mungu maana hapa wamemweka kichaa sokono na watu wataumizwa kama unavyoona tayari keshaanza, nasikia huko ATC watu wameanza kujuta na kulia.
 
Natumaini hawa jamaa wa ATC wasije kudhani kuwa nimewasahau.. ni mambo mengine muhimu ya Taifa yamenitinga tu. Ila after all this tunao. Wenyewe sasa wanatarajia ndege kuingia nchini "sometime in
April". Sijui kama wameshapata ile guarantee ya serikali ngoja nicheki na watu wa Wizara.

Ningekuwa mimi mmoja wa hawa jamaa ningeomba kujiuzulu mapema kabla hili halijafumuka.
 
UFISADI ATCL – JK IOKOE KAMPUNI
Sisi wananchi tuliyo ndani na nje ya ATCL tumeona hatuwezi kukaa kimya tukiangalia jinsi kampuni inavyoangamia kwa ufisadi wa kisayansi.
Ufisadi wa kisayansi kwa sababu wanaofanya ufisadi huu ni uongozi wa kampuni kwa kutumia nafasi zao za madaraka na kujifanya huo ndio uongozi.
Tuanze kwa kueleza ni maeneo gani yenye ufisadi halafu tutaje viongozi hao na sifa zao.

Tutataja maeneo yenye ufisadi na matumizi mabaya ya mapato ya kampuni na mikopo toka mabenki mbalimbali.Pia safari zilizo nyingi na za muda mrefu bila kujali gharama na faida za safari hizo.Manunuzi ya magari kwa fedha za mikopo na bila kufuata taratibu. Mwisho ni hila za kuwafukuza ama kuwaondoa katika nafasi nyeti wafanyakazi wa zamani na kuweka wapya ambao huajiriwa kiholela na bila ya sifa zinazolingana na kazi zenyewe au hata na wale waliyoondolewa.
Jopo la viongozi na sifa zao zinazoangamiza kampuni ni:-

1. Mkurugenzi mkuu wa kampuni ni David Mataka. Yeye aliteuliwa na Rais JK baada ya rais aliyemtangulia kumtimua kwa ufisadi. JK alimuonea huruma DM baada ya kukaa ubaoni kwa muda na pia kushindwa kinyang'anyiro cha ubunge kwa tiketi ya chama tawala. Wananchi wa jimbo lake na wa chama chake hawakumpa kura kwa kuwa alikwisha onekana mbele ya rais BM kuwa ni fisadi wa hali ya juu japo yeye rais BM alikuwa anawakumbatia mafisadi kama Balali.
Mkuu huyu wa kampuni ameanzisha uongozi wa dharura(Management by crisis) ambapo kila asubuhi wakurugenzi na mameneja wateule katika ufisadi hukaa vikao vya kuangamiza kampuni. Amepata Benz ya kisasa katika mgao wa magari yaliyotolewa na wauzaji baada ya kununua magari ya kampuni huko Dubai kwa bei ya juu. Magari hayo ni ya mwaka 1998 japo bei yake ni karibu na mara mbili ya yale yanayouzwa na makampuni mengine ya Dubai. Yeye huwa anasuka jambo halafu anamwachia George, Eliasaph au William walichochee katika kikao cha hao viongozi.

2. Mark Manji yeye ni mtu wa Musoma japo jina lake la kihindi. Huyu ni mshauri wa mkurugenzi mkuu. Alikuwa mkurugenzi wa idara ya operations wakati wa makaburu japo idara hii huwa inaongozwa na marubani. Alipewa cheo hiki na makaburu ili kuwaweka marubani katika himaya ya makundi. Makaburu walipoondoka aliomba kuacha kazi kwa hiari na akastaafu akaomba kuendelea na kazi tena kama mshauri wa mkurugenzi mkuu. Kwa kuwa alikuwa na mapenzi na makaburu na kwa kuwa ameshapata mafao yake, hana huruma na kampuni kwa sasa badala yake yeye ni kichocheo na hujifanya analijua shirika. Anatumia utoto wa mjini kufanya kazi kwani hana shahada hata moja japo amepewa nafasi nyeti.

3. Eliasaph Mathew aliajiriwa na makaburu kama meneja wa fedha kwa maana hiyo ni mtu wa makaburu. Baada ya mkurugenzi wa fedha aliyekuwa kaburu kuondoka amekaimu nafasi hiyo hadi leo. Huyu ndie kinara wa kupindisha taratibu za matumizi ya fedha na ununuzi. Ni mfuasi namba moja wa DM kwani kwa sasa pesa za kampuni hutolewa kiholela kulipia gharama kwa ufisadi. Mfano kabla ya kufunga mwaka 2007 shillingi millioni mia mbili hamsini zilichotwa kulipa gharama za kutoa magari nane yaliyokuwa katika yadi ya kuweka mgari iliyo ya watu binafsi. Haishi hapo huchota dola elfu tatu taslimu toka kwa mtunza fedha kila mwezi na kumpa huyu mwenye yadi ya kuhifadhi magari. Huidhinisha malipo kwa ankara tu bila kujali taratibu nyingine. Ndiye aliyejumuika katika jopo lililokwenda Dubai kuchagua magari ya kampuni na kuyanunua kwa bei mbaya bila kufuata taratibu za ununuzi. Magari haya ni ya 1998 japo ATCL ni mali ya serikali,hilo halikutiliwa maanani. Yeye amepata zawadi ya VX Landcruiser ya kisasa kama mgao katika hayo manunuzi na sasa ameweka pembeni Vitara yake. Hutumiwa katika mikakati ya kuwaondoa watu wa zamani na wenye sifa kwa kuwazulia kesi na shutuma za matumizi mabaya ya pesa kitu ambacho si kweli.
Waliyoonja joto hilo ni pamoja na Hassani ambaye aliamua kuacha kazi, Hamisi na Mndeme ambao wamesimamishwa kwa suala la bwana Mohamed Makaratasi ambaye ni rafiki wa George Mazula.

4.George Mazula yeye eti ndiye rubani kiongozi na mshauri wa DM. Huyu aliwahi kuachishwa kazi wakati mwenyekiti wa bodi alikuwa ni Abasi Sykes. George aliwahi kuunguza injini mbili za Fokker kwa mpigo pale Tanga. Amewahi kuangusha ndege aina ya Fokker hapa Dar es salaam. Amewahi kuua mtu pale uwanja mpya wa JK Nyerere kwa kukatwa na pangaboi baada ya yeye kuzembea kuzima injini. George ni kiungo wa mikakati yote ya ufisadi na kuondolewa watu katika nafasi zao. Alikuwa mfadhili wa DM wakati akiwa ubaoni. Ni rubani mwenye makeke na mikosi mingi. Katika dili ya Dubai yeye amepata Volvo na kujidai amekopa.

5. Amin Mziray huyu ni katibu wa kampuni. Yeye ni chapombe. Alipewa gari ya kampuni na makaburu na kulipindua kwa ulevi. Anayo shahada ya sheria lakini haitumii kwa maslahi ya kampuni. Kampuni imeshindwa kesi nyingi kwa kutokuwa makini huyu mwanasheria. Yumo katika hili jopo la ufisadi wa kampuni. Katika mgao wa magari ya Dubai yeye amepata VX Landcruiser la nguvu. Hayupo tayari kutetea hoja mbovu zinazotolewa ndani ya vikao vya hili jopo la ufisadi.

6. William Haji, anakaimu nafasi ya mkaguzi mahesabu wa ndani. Aliajiriwa wakati wa makaburu kama mkaguzi wa mahesabu wa ndani chini ya bwana Yakubu. Baada ya muda bwana YAkubu aliwekwa pembeni na huyu bwana kukaimu nafasi yake. Kwa sasa yeye ndiye anayekagua malipo (Pre-audit) hivyo yumo ndani ya mtandao wa ulaji. Ndiye anayetumiwa kutengeneza taarifa za kuzua kesi na uonevu kwa wafanyakazi wa chini. Huchukua nafasi ya afisa usalama wa kampuni ili kupindisha ukweli na hatimaye kuwadhalilisha ama kuwatimua wafanyakazi wasiyo na hatia. Ni hatari sana kwani yupo karibu na DM na Eliasaph katika kila mpango.

7. Sadiki Muze, Yeye ni mkurugenzi wa idara ya operations kwa sasa. Amepewa nafasi hiyo yeye kwani ndiye aliyekuwa mfadhili mkuu wa DM wakati akiwa ubaoni. Pia ni mshirika wa DM katika vinywaji na mwanachama wa kijiwe kimoja na George. Ni Sadiki na George pekee waliyopewa vyeo na kuenguliwa wengine baada ya DM kuchukuwa uongozi ATCL na ni chapombe. Sadiki na George wamelipwa fadhila.

8. Heho Mbiru ni Mkenya, aliajiriwa kwa nguvu enzi za makaburu kama mkurugenzi wa masoko. Aliajiriwa kwa nguvu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi ya ATCL wakati huo Ali Mufuruki kwa kisingizio kuwa hakuna Mtanzania mwenye uwezo wa kushika nafasi hiyo. Ni mzalendo wa Kenya kweli kweli kwani kazi zinazoweza kufanyika hapa (kama Graphics) huzipeleka kwenye kampuni yake. Anayo mapenzi na makaburu hivyo kuleta mabadiliko tunayotaka yeye ni kikwazo na ndiyo maana ni rahisi kutumiwa katika hujuma. Kumbuka tunaushindani na Kenya Airways huyu atatumaliza.

9. Ajay Gopinath raia wa India. Aliajiriwa kwa nguvu wakati wa makaburu na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi Ali Mufuruki. Ajay aliwahi kufukuzwa nchini lakini kwa sababu zake Ali alifanya juu chini na kumrudisha kama mkurugenzi wa mauzo. Anatumiwa katika upatikanaji wa fedha na kutumika vibaya. Hana sauti ndani ya utawala huu kwani ni mgeni.

10. Alphonse Mkinga ni meneja utumishi. Alistaafu na kuchukua mafao yake baada ya makaburu kutimka. Anafanya kazi kwa mkataba na kuzuia ajira kwa waliomaliza vyuo.
Ameidumaza idara ya utumishi kwa kutoweka muundo wa utumishi na taratibu mbalimbali za ajira. Matokeo yake mkurugenzi mkuu huleta watu wake japo wapo waliofanya usaili. Mfano ni ajira ya mhudumu katika ofisi ya mkurugenzi mkuu,ajira ya afisa majengo na mali ambaye ni jamaa yake. Huyu bwana Peter Gosh anachukua nafasi ya bwana Hassan Kikoko alieandamwa na huu mtandao wa ufisadi na hatimaye kuamua kustaafu mapema. Yupo dereva aliajiriwa kwa hila japo wapo waliofanya usaili na hadi sasa hawajapata ajira. Bwana Mkinga hana sauti kwani yupo kulinda maslahi yake baada ya kupata ajira ya pili.

11. Fidelis Tarimo ni mkurugenzi wa uhandisi. Historia yake ni ufisadi mtupu. Aliwahi kusimamishwa kazi na aliyekuwa mwenyekiti wa bodi wakati huo Mzee Abasi Sykes. Tarimo alikwenda kusimamia matengenezo makubwa ya Boeing ya ATC wakati huo (major check) nchini Ireland. Hakuwa anafuatilia gharama halisi za matengenezo na kujali maslahi yake hivyo kusababisha gharama kupanda kwa shilingi bilioni moja na nusu toka ghrama halisi na kulitia shirika hasara na kusimamishwa kazi. Alipata nafasi wakati wa makaburu kwani hakuwa mtetezi wa wazalendo. Kwa sasa wafanyakazi wa idara yake hawamtaki na wameandika barua ya kumkataa na wizara inajua hilo. Ni bingwa wa kuuza ndege za kampuni kwa bei ya kutupwa badala ya ile ya makubaliano ya awali. Ana ukabila na hadi sasa ana jamaa yake anasimamia ujaji wa ndege ya kukodi kwa muda mrefu yuko nje ya nchi. Ni fisadi wa kutupwa kwa ajili ya kutaka pesa za kuendeleza biashara zake.

12. Rajabu Itambo ni meneja Galileo Tanzania kampuni tanzu ya ATCL. Rajabu alipewa kazi ya ushauri katika kitengo cha Galileo na aliyekuwa meneja wakati huo Maalim Ali. Kaburu mmoja aliyekuwa mkurugenzi wa biashara Mike Bond aliamua kumuondoa Maalim Ali katika nafasi hiyo na kumuweka Rajabu kwa maslahi yake kwani walitaka kuuza Galileo kabla ya kuondoka jambo ambalo hawakufanikiwa. Mpaka sasa Rajabu ana uhasidi na wafanyakazi wa zamani kwani anataka awe mkuu wa kitengo cha ITC(Information and Technology Communication) Ni mmoja wa vibaraka wa DM.

Hadi tunakwenda mitamboni ATCL haina bajeti na hili linatokana na Eliasaph kutayarisha bajeti hiyo kwa usiri mkubwa akiweka vipengele hewa ambavyo bodi ina wasiwasi navyo hivyo kuikataa kila wakati. Bajeti huwa inatengenezwa na kitengo maalum katika idara ya fedha lakini safari hii imekuwa na usiri mkubwa. Ilibidi iwekwe hadharani kwa wafanyakazi kupitia workers council ndiyo iifikie bodi jambo ambalo halikufanyika.

Kama tulivyoeleza awali matumizi mabaya ya pesa yanapeleka kampuni kusikoeleweka. Pesa huchotwa kama za mtu binafsi bila kujali taratibu za kihasibu. Viongozi hawa kwa vikundi huenda safari kila wakati kuliko viongozi wote waliopita. Posho wanayolipana ni kubwa mno kwa kila siku hivyo hata safari za watendaji wa chini huenda wao. Mwenyekiti wa bodi Mustapha Nyang'anyi aliliambia Sunday Citizen tarehe 12 januari 2008 kuwa uzembe wa menejimenti ya ATCL kutoingia mkataba na kampuni iliyokuwa ikodishe ndege kwa ajili ya mahujaji ndiyo chanzo cha sakata zima la hasara katika usafirishaji wa mahujaji. Ukweli ni kuwa menejimenti haikutaka kushirikisha wafanyakazi wa kawaida kuratibu safari hii kama ilvyokuwa miaka iliyopita. Hii ni kwasababu walitaka iwe siri yao kwa kutafuta ndege ya bei poa kuliko hiyo iliyopatikana kitu ambacho hakikuzaa matunda na hatimaye kusema ATCL haiwezi kusafirisha mahujaji. Mbona kabla ya makaburu iliwezekana. Hapa pana ufisadi sio uzembe tuu. Wapo wazoefu wa kazi ndani ya kampuni lakini wamekodi mtu wa nje Mtambalike rafiki yake DM kwenda kusimamia kurejea mahujaji. Tunasema hii ni hujuma na kuwadharau watendaji wa ndani.
Magari ya kampuni yamenunuliwa kwa bei kubwa bila kufuata taratibu na viongozi wanne kupata magari kutokana na gharama hiyo kubwa na bila kufuata utaratibu wa ununuzi. Hivi sasa kampuni inamadeni mengi kutokana na ufisadi.
Wafanyakazi wasiotakiwa hasa wale wa zamani hutafutiwa sababu za kuwaondoa ili ajira wapewe watu wa DM. Mifano hai tumetaja hapo juu na mingine mingi tunayo kama ule wa Said Ibrahimu kufanyiwa visa na Mark Manji hadi kuamua kustaafu ili yeye Manji aongeze muda alipoamua kustaafu kwa kisingizio kuwa hakuna wa kuchukua nafasi yake.

Kwa sababu tumezungumza kwa kifupi tunaomba yafanyike yafuatayo:-

1. Kuleta wakaguzi kama vile Enerst and Young kukagua mahesabu ya ATCL tangu DM awe mkurugenzi mkuu. Hapa panatosha kuona ufisadi katika:-

(i) Mikopo na over draft na kutafuta jinsi pesa hizo zilivyotumika kwa ukamilifu.

(ii) Kupata maelezo kutoka kwa DM kwa nini toka achukue uongozi ATCL hakubadilisha muundo na uongozi wa makaburu tukijua fika viongozi hao wana maslahi na makaburu.

(iii) Uchunguzi juu ya ununuzi wa magari bila kufuata kanuni na taratibu za ununuzi nje ya nchi na kulinganisha bei na makampuni mengine ya Dubai

(iv) Wachunguzwe hawa viongozi wanne walipataje magari hayo toka kwa kampuni iliyouza magari kwa ATCL kwa bei ya juu. Kama ni mikopo waoneshe pesa walipata wapi na utaratibu mzima wa kuyalipia na kuingiza na kuyakomboa.

(v) Zipatikane sababu za viongozi kuomba kustaafu na kujiajiri tena.

(vi) Uchunguzi ufanywe kupata uhalali wa wafanyakazi wa zamani kunyanyaswa na wengine kusimamishwa kazi kwa hila ili kuajiri wengine kwa maslahi ya uongozi.

(vii) Uchunguzi ufanywe kuhusu malipo yote kwenye kampuni iliyohifadhi magari toka yatolewe bandarini.

(viii)Uchunguzi ufanywe kuhusu elimu na uwezo wa Peter Gosh kwani aliyeondolewa kwa hila alikuwa Civil Engineer.

(ix) Uchunguzi ufanywe kuhusu safari zote walizosafiri hawa viongozi kama zilileta manufaa. Wamesafiri sana na pesa nyingi zimetumika. Kuna wakati menejimenti yote ilikwenda
China kwa pamoja japo waliondoka kwa vikundi.

(x) Mwisho serikali ichukue hatua mapema kabla kampuni haijaangamia. Sisi tuliopo nje na ndani tunaona na tunajua, na kama kutahitajika msaada tupo tayari kutoa ushirikiano.
 
Back
Top Bottom