Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

sijui labda uniambie alihamishwa kwa sababu gani?
anaehamisha maaskofu ni papa mwenyewe
kwani umeshawahi kumsikia Askofu kilaini akilalamika kuhamishwa kwake?
wito wa kitume unatumwa popote kueneza neno

Tusitetee upuuzi, uchunguzi ufanyike kama hiyo pesa haina maelezo ya kutosheleza atawajibishwa tu.

Na kama ni fungu la kumi au zaka kumbukumbu za kanisa zitaonyesha.

Hivi Unajua kwa nini alihamishiwa Tabora toka Dar.?
 
sisi pesa ya rugemalila inatuhusu nini jamani kama wamepeana kirafiki utajuaje kwani kilaini yupo kwenye nafasi gani ya utendaji kwamba akihongwa anaweza kusaidia jambo fulani,hapo ndipo utaamini kuwa pesa za rugemalila ni zake alitoa kama wewe unavyoweza kumpa mdogo wako lakini kama mtu anaushahidi wa kutosha kuwa rafu imechezeka mahakama ndiyo mahara pakuondoa utata.

Hii haihitaji tochi ili kumulika na hatimaye kung'amua ukweli. Maaskofu wa kikatoliki ndio watawala wa nchi hii kupitia mlango wa nyuma. Hivyo Ruge alikuwa anajua kabisa kuwa iwapo nitakamata hawa maaskofu issue hii itapoa nakuwa baridi kabisaa. Amin amin Bank ya Mkombozi inapaswa kupigwa faini kwa mujibu wa sheria za utakatishaji fedha lakini imechukuliwa hatua gani? Mbona accounts za VIP kule Dutchland zimekuwa frozen?
Kilaini ni mtu muhimu ktk Kanisa ndio maana yupo kwenye mgawoo tueleze kitu kingine lakini hii iko wazi
 
Kwa masikitiko makubwa ninayo huzuni kuandika hapa kuwa Mmojawapo wa waliomegewa pesa za mbia wa IPTL ni askofu msaidiza wa jimbo la bukoba mhashamu Askofu Kilaini. Yeye alimegewa pesa hizo kutoka akaunti ya Rugemalira iliyoko kwenye Benk ya Ukombozi.

Kwa mujibu wa statement ya mbia huyo wengine ni akina Anna tibaijuka kama ilivyokwisha kuandikwa awali.
Bila shaka mtaniuliza chanzo au source, source ni kuwa huu ni ukweli mtupu, siandiki kwa chuki za kidini kwa kuwa mimi pia ni mkatoliki, bali nimeandika hapa kwa kuwa Baba askofu ni mtu wa Mungu ajiokeze akanushe kama anaweza, au atueleze nia na madhumuni ya kupewa pesa hizo ili tumwelewe, kwa vyovyote vile simwelewi.

hata wewe hujaweka wazi! kwani alichukuwa kama kama zawadi au za kazi gani!
 
Mch.Msigwa kaigusia hii kitu jana, huenda mambo yakaharibika zaidi
 
In fact,ilikuwa ni ada ya ushauri wa kiroho yaani kule ulaya tunaita spiritual consultancy fee.

Yeah that's a new term spiritual consulatance fee .I wil start my office..lakini inaelekea this man rugemarila is an expert n corrupting aur leaders. since IPTL was brought in tz he has corrupted so many officers and leaders since mzee ruksa erra.
 
Naomba nisaidiwe kitu mimi siyo mkabila lakini kwanini huyu Rugemalila asilimia 99% ya aliowapa pesa ni wahaya wenzake? Kulikoni hapo?

Kwa masikitiko makubwa ninayo huzuni kuandika hapa kuwa Mmojawapo wa waliomegewa pesa za mbia wa IPTL ni askofu msaidiza wa jimbo la bukoba mhashamu Askofu Kilaini. Yeye alimegewa pesa hizo kutoka akaunti ya Rugemalira iliyoko kwenye Benk ya Ukombozi.

Kwa mujibu wa statement ya mbia huyo wengine ni akina Anna tibaijuka kama ilivyokwisha kuandikwa awali.
Bila shaka mtaniuliza chanzo au source, source ni kuwa huu ni ukweli mtupu, siandiki kwa chuki za kidini kwa kuwa mimi pia ni mkatoliki, bali nimeandika hapa kwa kuwa Baba askofu ni mtu wa Mungu ajiokeze akanushe kama anaweza, au atueleze nia na madhumuni ya kupewa pesa hizo ili tumwelewe, kwa vyovyote vile simwelewi.
 
  • nimeikuta hii kwenye profile ya baba askofu kilain, kuna mtu kamuuliza swali kama amepokea mgao. ila hajarijib, sijui hajaingia FB au muda muhafaka wa kulijibu haujafika. natumai magazeti ya kesho yatatoa majibu. wengi wanapitia humu....

    "Tumsifu Yesu Kristo Baba Askofu.
    Natumaini mzima wa afya na unaendelea vizuri na huduma Mungu aliokutuma.Baba Askofu,Sisi waumini wa kanisa lako huku mtaani tunaulizwa maswali ambayo hatuna majibu juu ya kiongozi wa kanisa letu.Kama ujuavyo sasa hivi kuna vugu vugu la Tegeta Escrow.Pesa iliokwapuliwa na wajanja wachache na kuacha watanzania tukiteseka na kukosa huduma za lazima kwa jamii.Mitandaoni jina lako linatajwa kama mmoja uliokuwemo kwenye mgao kutoka kwenye akaunti hiyo.
    Kama waumini mpaka sasa hatuwezi amini tuhuma za mtaani zinazolenga kumchafua kiongozi wa kanisa letu.Ukiwa kama mtu unaekemea maovu tuhuma kama hizi zinaweza kuwa za kupikwa ili kukupunguza kasi ya kupambana na wadhalimu wa nchi hii.
    Waumini tuna imani na utendendaji wako na usafi wako.Hivyo basi uku tukisubiri ripoti itoke rasmi na tunafahamu umebanwa na majukumu ya kikanisa tunakuomba useme neno kuweka anga safi japo kwa uchache uwajibu wanaozusha uvumi huu.

    Tunakuombea kwa Mungu upate nguvu na hekima kuendeleza huduma uliotumwa"
 
Kwa masikitiko makubwa ninayo huzuni kuandika hapa kuwa Mmojawapo wa waliomegewa pesa za mbia wa IPTL ni askofu msaidiza wa jimbo la bukoba mhashamu Askofu Kilaini. Yeye alimegewa pesa hizo kutoka akaunti ya Rugemalira iliyoko kwenye Benk ya Ukombozi.

Kwa mujibu wa statement ya mbia huyo wengine ni akina Anna tibaijuka kama ilivyokwisha kuandikwa awali.
Bila shaka mtaniuliza chanzo au source, source ni kuwa huu ni ukweli mtupu, siandiki kwa chuki za kidini kwa kuwa mimi pia ni mkatoliki, bali nimeandika hapa kwa kuwa Baba askofu ni mtu wa Mungu ajiokeze akanushe kama anaweza, au atueleze nia na madhumuni ya kupewa pesa hizo ili tumwelewe, kwa vyovyote vile simwelewi.

MAASKOFU wengi ni WASANII TU.

Hakuna lolote hapa.

hayo makanisa wanayatumia Kufichia mambo yao HARAMU wanayofanya.

Hizi dini zingine ni MAJANGA TU.

Halafu utakuta WAUMINI wa Jimbo lake wakimuona anakuja Wanampigia vigelegele na kumvisha MASHADA YA MAUA KA BIBI HARUSI.

Makatonta Ovyo sana.
 
Naomba nisaidiwe kitu mimi siyo mkabila lakini kwanini huyu Rugemalila asilimia 99% ya aliowapa pesa ni wahaya wenzake? Kulikoni hapo?

Ndiyo watu anaowafahamu. Huoni wengine wakidai ni kaka yao na wenginr wakisema wamekua na kusoma pamoja shule za msingi. Yamkini hata Kilaini ndye alikuwa padre aliyefunga ndoa yake au ni mjomba wake.
 
wagalatia mtatumalizia kodi zetu.

Wamalize mara ngapi.

Mkuu we hujiulizi hawa MAASKOFU unawakuta wana vitambi ka wafanyakazia wa TEE ARA EI Wakati Waumini wao wanasema kuwa HAWALIPWI Mishahara bali wanashiba neno la yesu tu.

Sasa km Milion 80 mtu HANA MSHAHARA siku wakipangiwa mishahara hawa Itakuwaje nchi hii MASKINI?

Hebu Tumuulize Padri Slaa mbona yuko KIMYA KABISA kuhusu suala hili?
Kulikoni CHADEMA? Mbona KIMYA?
 
Jukwaa hili ni kubwa sana na linahitaji heshima yake ili liendelee kuwafaa watanzania.Haifai mtu kuleta uzi bila kuwa na chanzo cha kuaminika na kusisitiza eti chanzo ni mimi mwenyewe.Kama chanzo ni wewe mwenyewe kwanini usiweke ushahidi hapa jamvini?

Msitake tuanze kujaji watu bila ya ushahidi,kwa kufanya hivyo hatutakwepa dhambi ya kuchafua watu kwa maslahi ya wachache.

Mleta uzi, weka ushahidi hapa...acha umbea na majungu hili ni jukwaa muhimu sana kwa watanzania na wengine hulichukulia kama ''Authority "',so ukileta majungu hapa utakuwa hauisaidii Tanzania
 
Mimi ni mkatoliki kabla hata sijazaliwa na bila shaka nitakufa nikiwa hivyo, ila Askofu Kilaini huwa naona ni mropokaji na mpotoshaji mkubwa, hasa alipotumia Altare ya Bwana (2005) kumpigia kampeni JK akisema ni chaguo la Mungu. Leo hii hawezi tena kukaa na kuthibitisha yale aliyokuwa anayaropoka.

We km Utakufa MKATOLIKI au MGALATIA hio haituhusu hapa.
Labda ukamwambie Mkeo.

Cha ajabu ni kuwa UMEKASIRISHWA na ASKOFU Kumpigia Kampeni JK ktk KANISA lkn Kwa YEYE Kuchota PESA ZA WALIPA KODI wala HILO HALIJAKUKERA KABISA!

Ama kweli Wewe ni CHAGUO LA SHETANI mwizi wa HAKI.

DUhhh!
 
WanaJF,

Kuna list imeweka humu mjengoni ya walioshiba pesa za escrow. Baadhi ya majina mengine yanatajwa lakini hatujayaona huko. Je; na wao wanahusika?
 
ndugu wana jf, nimesikitika sana kuona baba askofu wa jimbo la bukoba kahusika wa wizi wa pesa za escrow,
sisi waamini katika kainisa hili tutakuwa nawe katika kipindi hiki kigumu, kwa kuwa hatutazami zambi zako bali twatazama imani ya kanisa lako, ila tumeumia sana sana
 
mkuu naomba kama hutajali orodha ya hawa waliojichotea hizi pesa
 
Hivi kaiba au kapewa kwenye mradi wa ujenzi wa shule? Make watanzania kwa majungu hamjambo.

Hivi fedha iliyokatwa kodi TRA na Waziri mkuu akaithibitisha Bungeni kuwa sio fedha ya umma bali ni ya wabia, wewe raia wa kawaida usiyekuwa na information za uhakika serikalini kama ilivyo kwa Kilaini unatolea wapi ujasiri wa kuhoji chanzo cha fedha hiyo? Hiyo pesa unaanzia wapi kuitilia wasiwasi kama sio safi??? Acheni tabia ya kupenda kuandika-andika ujinga msioujua hata mtiririko wa chanzo chake ni kipi.

Me nadhani tusione ni sifa kila wakati kuletaleta vi mada vya kijingajinga hapa jf kisa umekosa kazi za kufanya huko majumbani... unaweza ukaamua kupumzika tu hata uani.
 
Back
Top Bottom