Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

Askofu Methodius Kilaini naye alimegewa 80m za mbia wa IPTL

Mbona za richmond mzee mamvi kagawa misikiti na makanisa yote hamjawasema? Tena naona uyo kachukua ndogo m80? Lowasa kagawa 100m kwa mashekhe, ma padri na maaskofu wote hamkusikia? Ivo ni vijicent tuu mhashamu kachukua muacheni na yeye ale keki ya taifa maana sisi tumeshindwa kwa kukosa akili.
kwa masikitiko makubwa ninayo huzuni kuandika hapa kuwa mmojawapo wa waliomegewa pesa za mbia wa iptl ni askofu msaidiza wa jimbo la bukoba mhashamu askofu kilaini. Yeye alimegewa pesa hizo kutoka akaunti ya rugemalira iliyoko kwenye benk ya ukombozi.kwa mujibu wa statement ya mbia huyo wengine ni akina anna tibaijuka kama ilivyokwisha kuandikwa awali. Bila shaka mtaniuliza chanzo au source, source ni kuwa huu ni ukweli mtupu, siandiki kwa chuki za kidini kwa kuwa mimi pia ni mkatoliki, bali nimeandika hapa kwa kuwa baba askofu ni mtu wa mungu ajiokeze akanushe kama anaweza, au atueleze nia na madhumuni ya kupewa pesa hizo ili tumwelewe, kwa vyovyote vile simwelewi.
 
Mkuu cv ya huyu jamaa ni tapeli aliyekuja kujifanya International business consultant. Alishafanya kazi BoT miaka ya nyuma akaondoka kwa skendo. Baada ya hapo akawa ni mtu wa kufungua vikampuni hasa vya kufanya deals za ndani hapa akishirikiana na kampuni za nje. Alitumia kona zake alizoziestablish akiwa BoT na pia lobbying ya Wahaya wenzake waliokuwa kwenye positions kuwin deal za ndani. Alivyopata fedha, akapunguza kutumia ukabila akawa anasambaza noti. Kwa kifupi ni mchora madili makubwa mkali lakini anatumia ulaku wa viongozi kufanikisha madeal yake hasa kulegezewa kanuni, taratibu na sera za nchi.

Rugemalira siyo tapeli,ni msomi na mtu smart ambaye ametumia ujinga na uroho wetu kupenda mali kujipatia mafanikio. Wakati mnahangaika hapa yeye yupo busy kutafuta pesa zaidi.
 
Mbona za richmond mzee mamvi kagawa misikiti na makanisa yote hamjawasema? Tena naona uyo kachukua ndogo m80? Lowasa kagawa 100m kwa mashekhe, ma padri na maaskofu wote hamkusikia? Ivo ni vijicent tuu mhashamu kachukua muacheni na yeye ale keki ya taifa maana sisi tumeshindwa kwa kukosa akili.

Nani kakudanganya Lowassa anagawa pesa za Richmond? Niwaombe Watanzania wenzangu mjikite kuwawajibisha Watawala walio zembea mpaka tumefikia hapa.
 
Ivi mi nikitoa sadaka, na mchungaji asijue nimepataje iyo sadaka, mchungaji akiitumia, anapata dhambi?!

Kama kweli.hajii hawezi kupata dhambi. Ila kama anajua atakuwa ameshiriki uovu ikiwa hiyo pesa ilipatikana kwa njia ya uovu.
 
nani kakudanganya lowassa anagawa pesa za richmond? niwaombe watanzania wenzangu mjikite kuwawajibisha watawala walio zembea mpaka tumefikia hapa.

wewe utakuwa ni mnyarwanda kama sio banyamulenge. Hayo ma bilion aliyowapa mashekhe na maaskofu tanzania nzima achilia harambee na lowasa anavutikaga kuanzia 100m kwenye kila event achilia mbali bahasha za makanjanja kama pasco & co-bila kuwasahau twaweza je kazipata wapa? Kwa haraka haraka toka kajiuzulu uwaziri kashalipa na kuchangia zaidi ya 70b kazipata wapi? Pole yako
 
Rugemalira siyo tapeli,ni msomi na mtu smart ambaye ametumia ujinga na uroho wetu kupenda mali kujipatia mafanikio. Wakati mnahangaika hapa yeye yupo busy kutafuta pesa zaidi.
Hiki ni kizazi kilicholaaniwa kweli. Mtu tapeli unamwita smart? Whether ametumia ujinga wetu au kawa mjanja kuliko werevu wetu haiondoi utapeli wake. Ni tapeli na atabaki kuwa hivyo kwa matendo yake.
 
Binafsi ikidhihirika kuna ufisadi naacha ukatoliki wangu kwani mafisadi yanaongezeka mno kwenye kanisa langu
 
Kilaini hata kutolewa kwake dsm kulitokana na matendo yake kutoendana na yale anayohubiri!
 
nilidhani mpaka leo Baba askofu amekuwa amejibu hii hoja kuwa ni kwa nini alipokea mgawo wa 80m kwenye akaunti yake binafsi pesa zinazotiliwa shaka?
kukaa kwake kiimya ni kuzidi kuliumiza kanisa katoliki, ajue kuwa kanisa ni kubwa kuliko mimi na yeye
 
Njia sahihi kwake ni kujitokeza na kukiri au kukanusha. Ninachoona hapa mgawaji pesa alikuwa akitafuta influential persons na malengo yake hapa sijayajua. Huyu Rugemalira ni mtu wa namna gani? Wenye historia yake (cv) watuwekee hapa. Wabia / washiriki wake ni nani.....zahidi watafuta uraisi ili ni-conect dots kidogo... na nipate mwanga wa hapo baaadae juu ya nchi hii.
HUYU NI MTUTSI... nimesoma na mwanae kabisa ambaye hivi sasa ni SYSTEM AUDITOR WA TRA.
RUGE
RUGEMA(the late RPF COMMANDER)
RUGEMALILA..
hahahaaaa ni mchezo tu wa kuondo herufi na kuongeza nyingine lakini mwishowe ni watu walewale
 
Nani kakudanganya Lowassa anagawa pesa za Richmond? Niwaombe Watanzania wenzangu mjikite kuwawajibisha Watawala walio zembea mpaka tumefikia hapa.

Ndio maana na huyo kibaka wa richmond tunamuwajibisha kisayansi.
 
Watawa wote wa kanisa katoliki wanahudumiwa na kanisa hadi mwisho wa uhai wao. hivyo vipato vyao vyote ni mali ya kanisa kwani hawaruhusiwi kumiliki mali bali kanisa. sasa askofu kilaini hizo pesa kapokea kwa niaba ya nani? na kaweka kwenye akauti ya nani? kama amezitumia basi tujulishwe hayo matumizi ni ya kanisa au?
 
Ambacho nashindwa kuelewa hao waliochukua hela za huyo bwana wana kosa gani???

Wao wamepewa fedha kama zawadi tena fedha zilizokatwa na kodi TRA ulitaka wao wafanyeje? Njia iliyotumika mpaka kuzipata hizo fedha kama ni halali au lah anaijua mwenye fedha.

Hivi wewe rafiki yako akikupa fedha kama msaada utamuuliza kazitoa wapi?????

Mbona mnapenda kushikia watu mabango sana hata kwenye upuuzi? Mbona hamleti maelezo ya Mbowe naye kupewa zawadi?


Uko sahihi. Tatizo siyo aliyepewa pesa na Fulani. Tatizo letu ni nani alizichota toka akaunti husika. Tusianze kufuatilia aliyepewa na aliyepewa maana baadaye mtu ataandika watoto wa Tibaijuka walinunuliwa nyama, watoto wa Muhongo wanaendesha gari la baba yao, alilonunua kwa pesa za wizi, nk.

Tusiongeze wanufaika na kujikuta tunaharibu ushahidi kwa wezi. Tuambiwe nani alikuwa ktk njama za kuchoka. Kwa uhakika kabisa mtu kama Kilaini hawezi kuwa na madaraka ya kuzichota. Nani hao?
 
Baba rugemalera njoo utupe posho ya ku post humu jf baba.....
Jina lako li maarufu baba kwa kuwajali watu wa kada tofauti baba...unastahili tuzo baba kwa misaada yako ya kibini adamu ingawa ni vijipesa vya ugoro baba...

Kizuri kula na wenzio baba..tukumbuke wana jf...

Jamani fungueni akaunt mkombozi mkombolewe na mulokozi rugee malira
 
Mtu na hela zake, na matumizi yake haituhusu! Huyu Rugemalila yeye anakosa gani wakati ameuza hiza zake kihalali kwa PAP?...
 
ccm wanatamani hata wamtamani sana wapate nafasi ya kumhonga Mwenyezi Mungu. Yote wanayofanya ni kubaki madarakani kulinda ufisadi na maovu mengine wala si kuendeleza watanzania. Na sasa wanatumia wachina na wamarekani kututawala. wamarekani wanapewa madini na gesi wachina wanapewa biashara. ccm ni hatari kuliko chochote ulichowahi kusikia kuwa ni hatari.
 
Back
Top Bottom