Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
UONGOZI na UANAHARAKATI
Kuna mjadala mzuri unaendelea kuhusu UONGOZI na UANAHARAKATI. Bahati mbaya unafunikwa na propoganda na kupoteza fursa ya kuelimishana. Wapo wanaoponda uanaharakati kwa kudai wanaharakati si viongozi. Kundi la pili linatukuza uongozi kuwa hauna uanaharakati.
Mimi natamani mtu anitajie kiongozi mmoja asiye mwana harakati. Kisha anitajie mwanaharakati ambaye si kiongozi.
Kwa nini?
1. Kwa lugha ya kawaida uanaharakati maana yake ni imani au ushawishi (conviction and commitment) katika jambo fulani analolisimamia mtu na kulipigania. Msimamo huo ndio unaomtofautisha mtu huyo na watu wengine.
2. Kama dhana hii hapo juu ni sahihi, unawezaje kuwa na kiongozi asiyekuwa na msimamo au jambo analolisimamia?
3. Kiongozi asiye na harakati ni kama "boga boga" hivi, yupo yupo tu. Na mwanaharakati asiye na uongozi ni kama msafiri asiyejua aendako. Uanaharakati na uongozi haviachani. Taifa letu linahitaji vyote yaani viongozi wenye harakati (mzigo wa maono).
Kuushetanisha uanaharakati ni kushetanisha maendeleo. Hakuna maendeleo bila harakati (passion and commitment). Kutetea uongozi usio na harakati ndani yake ni kustawisha uzembe, umwinyi, umangimeza, mazoea kandamizi na uongozi usio na matokeo chanya. Tunapowatetea viongozi waliofanya mambo makubwa, tusiwatenge na harakati.
Bwana Yesu na Mitume wote maarufu wa dini zinazojulikana, walikuwa wana harakati. Uana harakati ni kutoridhika na hali ya mambo inavyokwenda na kuamua kuchukua hatua kuibadilisha. Uana harakati ni uchochezi mtakatifu.
Natamani kuwa mwana harakati. Kungekuwa na duka linauza harakati, ningeenda kununua. Bahati mbaya hakuna duka, hakuna dawa, bali uana harakati hupatikana kwa mtu kujenga nidhamu ya kutathmini, kujitambua, kuhoji na kuchukua hatua.