Askofu Kalikawe Bagonza: Uongozi na Uwanaharakati bahati mbaya unafunikwa na Propaganda za Kuelimishana

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
UONGOZI na UANAHARAKATI

Kuna mjadala mzuri unaendelea kuhusu UONGOZI na UANAHARAKATI. Bahati mbaya unafunikwa na propoganda na kupoteza fursa ya kuelimishana. Wapo wanaoponda uanaharakati kwa kudai wanaharakati si viongozi. Kundi la pili linatukuza uongozi kuwa hauna uanaharakati.

Mimi natamani mtu anitajie kiongozi mmoja asiye mwana harakati. Kisha anitajie mwanaharakati ambaye si kiongozi.

Kwa nini?
1. Kwa lugha ya kawaida uanaharakati maana yake ni imani au ushawishi (conviction and commitment) katika jambo fulani analolisimamia mtu na kulipigania. Msimamo huo ndio unaomtofautisha mtu huyo na watu wengine.

2. Kama dhana hii hapo juu ni sahihi, unawezaje kuwa na kiongozi asiyekuwa na msimamo au jambo analolisimamia?

3. Kiongozi asiye na harakati ni kama "boga boga" hivi, yupo yupo tu. Na mwanaharakati asiye na uongozi ni kama msafiri asiyejua aendako. Uanaharakati na uongozi haviachani. Taifa letu linahitaji vyote yaani viongozi wenye harakati (mzigo wa maono).

Kuushetanisha uanaharakati ni kushetanisha maendeleo. Hakuna maendeleo bila harakati (passion and commitment). Kutetea uongozi usio na harakati ndani yake ni kustawisha uzembe, umwinyi, umangimeza, mazoea kandamizi na uongozi usio na matokeo chanya. Tunapowatetea viongozi waliofanya mambo makubwa, tusiwatenge na harakati.

Bwana Yesu na Mitume wote maarufu wa dini zinazojulikana, walikuwa wana harakati. Uana harakati ni kutoridhika na hali ya mambo inavyokwenda na kuamua kuchukua hatua kuibadilisha. Uana harakati ni uchochezi mtakatifu.

Natamani kuwa mwana harakati. Kungekuwa na duka linauza harakati, ningeenda kununua. Bahati mbaya hakuna duka, hakuna dawa, bali uana harakati hupatikana kwa mtu kujenga nidhamu ya kutathmini, kujitambua, kuhoji na kuchukua hatua.
 
Huyu Bagonza ni askofu wa KKKT kule kwao Karagwe kwenye dayosisi yake ni dikteta ajabu!

Ana miaka 18 toka awe askofu, nilipata fursa ya kushiriki kongamano flani wili jana, jamaaana majivuno ajabu! Ni mkabila, huwezi amini kama huyu mtu amatumika madhabahuni, yani hana tofauti na viongozi wengine wa kisiasa hapa nchini.

Ana dharau sana viongozi wenzie wa kanisa anajiona yeye ndio msomi pekee

Anaongozwa na mihemko ya kisiasa zaidi.

Kiufupi huyu angejikita tu kuwa mwanaharakati kama mwenzie Lisu tu.
 
Huyu Bagonza ni askofu wa KKKT kule kwao Karagwe kwenye dayosisi yake ni dikteta ajabu!

Ana miaka 18 toka awe askofu, nilipata fursa ya kushiriki kongamano flani wili jana, jamaa ana majivuno ajabu! Ni mkabila, huwezi amini kama huyu mtu amatumika madhabahuni, yani hana tofauti na viongozi wengine wa kisiasa hapa nchini.

Ana dharau sana viongozi wenzie wa kanisa anajiona yeye ndio msomi pekee,!

Anaongozwa na mihemko ya kisiasa zaidi.

Kiufupi huyu angajikita tu kuwa mwanaharakati kama mwenzie Lisu tu.
Hahaha CCM mnalo mwaka huu!! Mtawa attack sana watu mwaka huu.
Wenye akili wote wanawakataa na uzuri ni kuwa wanauelimisha umma wawakatae pia.😂😂😂
 
Huyu Bagonza ni askofu wa KKKT kule kwao Karagwe kwenye dayosisi yake ni dikteta ajabu!

Ana miaka 18 toka awe askofu, nilipata fursa ya kushiriki kongamano flani wili jana, jamaa ana majivuno ajabu! Ni mkabila, huwezi amini kama huyu mtu amatumika madhabahuni, yani hana tofauti na viongozi wengine wa kisiasa hapa nchini.

Ana dharau sana viongozi wenzie wa kanisa anajiona yeye ndio msomi pekee,!

Anaongozwa na mihemko ya kisiasa zaidi.

Kiufupi huyu angajikita tu kuwa mwanaharakati kama mwenzie Lisu tu.
Dada imeandikwa, usimshuhudie jirani yako uongo!
 
Hahaha CCM mnalo mwaka huu!! Mtawa attack sana watu mwaka huu.
Wenye akili wote wanawakataa na uzuri ni kuwa wanauelimisha umma wawakatae pia.
Umma una maslahi yake na viongozi wa dini wana maslahi yao.

Wakati uma unataka shule za bure wao viongozi wa dini wanataka shule private za kulipia.
Wakati uma unataka hospital za bei rahisi viongozi wa dini wanataka serikali private ili watoze pesa.
Wakati uma unataka vyuo vya serikali viwe vingi viongozi wa dini wanataka viwe vichache ili wadahili kwenye vyuo vyao.

Katika muktadha huo viongozi wa dini wachumia tumbo lazima wawe against na serikali yoyote.
 
Na kwa akili hizo za kijamaa Ndo mana mmesababisha matatizo makubwa ya ajira nchini. Mnapiga vita uwekezaji binafsi mkifikiri mnaweza kuajiri watanzania wote na matokeo yake ma elfu na mamilioni ya watanzania hawana ajira. Kwenye nchi zenye maendeleo ya kweli sekta binafsi ndo imeshika uchumi wa nchi.

Kwa akili zenu mfu hizi mnazidi kutupa sababu ya kuwachagua watu wenye Sera za itikadi za ubepari kwa sababu tunajua sekta binafsi itapewa kipaumbele na hatimaye hakutakuwa na Tatizo la ajira mlilolitengeneza kwa Sera zenu mfu za kijamaa
 
Huyu Bagonza ni askofu wa KKKT kule kwao Karagwe kwenye dayosisi yake ni dikteta ajabu!

Ana miaka 18 toka awe askofu, nilipata fursa ya kushiriki kongamano flani wili jana, jamaa ana majivuno ajabu! Ni mkabila, huwezi amini kama huyu mtu amatumika madhabahuni, yani hana tofauti na viongozi wengine wa kisiasa hapa nchini.

Ana dharau sana viongozi wenzie wa kanisa anajiona yeye ndio msomi pekee,!

Anaongozwa na mihemko ya kisiasa zaidi.

Kiufupi huyu angajikita tu kuwa mwanaharakati kama mwenzie Lisu tu.

Ni YEYE... akili kubwa.
 
Na kwa akili hizo za kijamaa Ndo mana mmesababisha matatizo makubwa ya ajira nchini. Mnapiga vita uwekezaji binafsi mkifikiri mnaweza kuajiri watanzania wote na matokeo yake ma elfu na mamilioni ya watanzania hawana ajira. Kwenye nchi zenye maendeleo ya kweli sekta binafsi ndo imeshika uchumi wa nchi.

Kwa akili zenu mfu hizi mnazidi kutupa sababu ya kuwachagua watu wenye Sera za itikadi za ubepari kwa sababu tunajua sekta binafsi itapewa kipaumbele na hatimaye hakutakuwa na Tatizo la ajira mlilolitengeneza kwa Sera zenu mfu za kijamaa
Hatujazuia uwekezaji lakini tunazuia ukiritimba na ubinafsi kwenye masuala yanayogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Ajira si zaidi ya uhai wa watu au elimu kwa wenye kipato duni ambao hawawezi kumudu gharama. Kumbuka wenye uhitaji wa huduma ni wengi kuliko wenye uhitaji wa ajira hizo.
 
Dada imeandikwa, usimshuhudie jirani yako uongo!
Mimi ni KKKT huyo askofu nmeona hizo tabia nlipokuwa karagwe juzi kwenye tamasha! Yule alivyo hata hirizi atakuwa nazo ni kadikteta kwenye dayosisi yake hakuna mwenye sauti, mtu ana miaka 18 kwenye uaskofu katika dayosisi moja unategemea nini?

Haamini katika maombi,!
Kuna askofu wa dayosisi ya jirani yake yeye ni mhaya ila Bagonza ni mnyambwa hawaelewani ni kama paka na panya.

Kwa Bagonza udokta wake ndio kila kiti wengine wote ni takataka!

Hata hivyo ni Magufuli tano tena

Haya niite tena dada maana kufanya hivyo ndio unamuongezea Lisu kura.
 
Umekumbuka kutumia dawa zako?endelea kuchukua tahadhari na kufuata ushauri wa madaktari na kunawa mikono kwa maji tiririka
Mimi ni KKKT huyo askofu nmeona hizo tabia nlipokuwa karagwe juzi kwenye tamasha! Yule alivyo hata hirizi atakuwa nazo ni kadikteta kwenye dayosisi yake hakuna mwenye sauti, mtu ana miaka 18 kwenye uaskofu katika dayosisi moja unategemea nini?

Haamini katika maombi,!
Kuna askofu wa dayosisi ya jirani yake yeye ni mhaya ila Bagonza ni mnyambwa hawaelewani ni kama paka na panya.

Kwa Bagonza udokta wake ndio kila kiti wengine wote ni takataka!

Hata hivyo ni Magufuli tano tena

Haya niite tena dada maana kufanya hivyo ndio unamuongezea Lisu kura.
 
Hatujazuia uwekezaji lakini tunazuia ukiritimba na ubinafsi kwenye masuala yanayogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Ajira si zaidi ya uhai wa watu au elimu kwa wenye kipato duni ambao hawawezi kumudu gharama. Kumbuka wenye uhitaji wa huduma ni wengi kuliko wenye uhitaji wa ajira hizo.
Hao wenye kipato duni mnawapa elimu gani bora????

Shule zenu hizi zilizokosa vifaa, madawati, miundombinu bora na mitaaala yenu ya ajabu hii ndo elimu mnayowapa wenye kipato duni????

CCM mna akili duni sana. Mmeharibu elimu yetu, mnazuia uwekezaji makini na ushindani kwenye elimu ili tupate watu bora wa kuweza kushindana hata kwenye masoko ya ajira ya kimataifa alafu mnaleta maneno ya kujifanya mnawajali masikini hapa???? Wahuni tu nyie
 
Naziogopa sana hizi akili za TUKOSE WOTE TUUU. Ni roho gani hii? Uzuie maduka ya watu binafsi kabla hujaandaa la ujamaa chini ya uongozi wa kijamaa!! What a hell man. Uzuie elimu au vyuo vya private kisa; Watu wanatoza kodi/ada kubwa wanyonge wasioweza kuilipa. Je, dawa ni kufunga hivyo vyuo au kuanzisha kingine chenye uwezo huo halafu ukakiendesha kwa ada ndogo?? Nadhani mawazo yako ni uzezeta huo na mwisho ni TUMEKOSA WOTE HAKUNA WA KUMCHEKA MWINGINE. What a hell man. Njia ya kudumu kwenye uchumi wa kati ni kuruhusu ushindani huku sisi tukijiimarisha zaidi kwenye fani
 
Hao wenye kipato duni mnawapa elimu gani bora????

Shule zenu hizi zilizokosa vifaa, madawati, miundombinu bora na mitaaala yenu ya ajabu hii ndo elimu mnayowapa wenye kipato duni????

CCM mna akili duni sana. Mmeharibu elimu yetu, mnazuia uwekezaji makini na ushindani kwenye elimu ili tupate watu bora wa kuweza kushindana hata kwenye masoko ya ajira ya kimataifa alafu mnaleta maneno ya kujifanya mnawajali masikini hapa???? Wahuni tu nyie
Sasa kushindwa kabisa kwenda shule na kwenda huko kwenye mitaaala ila sio bora kipi kina afadhali? Kumbuka hata Mkapa alianzia kusoma kwenye kibanda cha udongo.
 
Huyu Bagonza ni askofu wa KKKT kule kwao Karagwe kwenye dayosisi yake ni dikteta ajabu!
Ana miaka 18 toka awe askofu, nilipata fursa ya kushiriki kongamano flani wili jana, kajamaa kana majivuno ajabu! Ni mkabila, huwezi amini kama huyu mtu amatumika madhabahuni, yani hana tofauti na viongozi wengine wa kisiasa hapa nchini.

Ana dharau sana viongozi wenzie wa kanisa anajiona yeye ndio msomi pekee,!

Anaongozwa na mihemko ya kisiasa zaidi.

Kiufupi huyu angajikita tu kuwa mwanaharakati kama mwenzie Lisu tu.
Naona kisu cha Bagonza kimegonga mfupa haswaa
 
We hovyo sana yaani serikali iache kujenga mashule na hospital kwa sababu wao wanajenga vyao??

Mbona serikali haijawazuia, ila wao wanaleta nongwa tu sababu wanaona serikali inajenga vya kwake na vyenye ubora zaidi.
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom