Askofu Kalikawe Bagonza: Uongozi na Uwanaharakati bahati mbaya unafunikwa na Propaganda za Kuelimishana

UONGOZI na UANAHARAKATI

Kuna mjadala mzuri unaendelea kuhusu UONGOZI na UANAHARAKATI. Bahati mbaya unafunikwa na propoganda na kupoteza fursa ya kuelimishana. Wapo wanaoponda uanaharakati kwa kudai wanaharakati si viongozi. Kundi la pili linatukuza uongozi kuwa hauna uanaharakati.

Mimi natamani mtu anitajie kiongozi mmoja asiye mwana harakati. Kisha anitajie mwanaharakati ambaye si kiongozi.

Kwa nini?
1. Kwa lugha ya kawaida uanaharakati maana yake ni imani au ushawishi (conviction and commitment) katika jambo fulani analolisimamia mtu na kulipigania. Msimamo huo ndio unaomtofautisha mtu huyo na watu wengine.

2. Kama dhana hii hapo juu ni sahihi, unawezaje kuwa na kiongozi asiyekuwa na msimamo au jambo analolisimamia?

3. Kiongozi asiye na harakati ni kama "boga boga" hivi, yupo yupo tu. Na mwanaharakati asiye na uongozi ni kama msafiri asiyejua aendako. Uanaharakati na uongozi haviachani. Taifa letu linahitaji vyote yaani viongozi wenye harakati (mzigo wa maono).

Kuushetanisha uanaharakati ni kushetanisha maendeleo. Hakuna maendeleo bila harakati (passion and commitment). Kutetea uongozi usio na harakati ndani yake ni kustawisha uzembe, umwinyi, umangimeza, mazoea kandamizi na uongozi usio na matokeo chanya. Tunapowatetea viongozi waliofanya mambo makubwa, tusiwatenge na harakati.

Bwana Yesu na Mitume wote maarufu wa dini zinazojulikana, walikuwa wana harakati. Uana harakati ni kutoridhika na hali ya mambo inavyokwenda na kuamua kuchukua hatua kuibadilisha. Uana harakati ni uchochezi mtakatifu.

Natamani kuwa mwana harakati. Kungekuwa na duka linauza harakati, ningeenda kununua. Bahati mbaya hakuna duka, hakuna dawa, bali uana harakati hupatikana kwa mtu kujenga nidhamu ya kutathmini, kujitambua, kuhoji na kuchukua hatua.
Wapendao maarifa hujipatia ufahamu! Ukizoea kusifu na kuabudu binadamu mwezio, si rahisi kuelewa hekima hizi!
 
Huyu Bagonza ni askofu wa KKKT kule kwao Karagwe kwenye dayosisi yake ni dikteta ajabu!

Ana miaka 18 toka awe askofu, nilipata fursa ya kushiriki kongamano flani wili jana, jamaaana majivuno ajabu! Ni mkabila, huwezi amini kama huyu mtu amatumika madhabahuni, yani hana tofauti na viongozi wengine wa kisiasa hapa nchini.

Ana dharau sana viongozi wenzie wa kanisa anajiona yeye ndio msomi pekee

Anaongozwa na mihemko ya kisiasa zaidi.

Kiufupi huyu angejikita tu kuwa mwanaharakati kama mwenzie Lisu tu.
Maneno matupu,weka ushahidi wa hayo madudu yake,ukabila,majivuno,
 
Mimi ni KKKT huyo askofu nmeona hizo tabia nlipokuwa karagwe juzi kwenye tamasha! Yule alivyo hata hirizi atakuwa nazo ni kadikteta kwenye dayosisi yake hakuna mwenye sauti, mtu ana miaka 18 kwenye uaskofu katika dayosisi moja unategemea nini?

Haamini katika maombi,!
Kuna askofu wa dayosisi ya jirani yake yeye ni mhaya ila Bagonza ni mnyambwa hawaelewani ni kama paka na panya.

Kwa Bagonza udokta wake ndio kila kiti wengine wote ni takataka!

Hata hivyo ni Magufuli tano tena

Haya niite tena dada maana kufanya hivyo ndio unamuongezea Lisu kura.
Mkuu punguza munkhali,wewe umemsoma na kumkagua katika dakika tano ukajua ni mwovu?

Kwa hiyo wewe ulikuwa auditor wa kiroho au mali au vyote. Unafikiri ni maaskofu uchwara wa kujitangazia sifa pasipo kuwa na vigezo?

Au umeshindwa kuelewa kazi za askofu ni zipi?
Nikwambie kitu acha kutumika kishabiki kwa mambo ya kidunia.
 
Humjui Bagonza mkuu,!

Nenda Karagwe pale ndio utajua ni mtu wa aina gani,!
 
C
UONGOZI na UANAHARAKATI

Kuna mjadala mzuri unaendelea kuhusu UONGOZI na UANAHARAKATI. Bahati mbaya unafunikwa na propoganda na kupoteza fursa ya kuelimishana. Wapo wanaoponda uanaharakati kwa kudai wanaharakati si viongozi. Kundi la pili linatukuza uongozi kuwa hauna uanaharakati.

Mimi natamani mtu anitajie kiongozi mmoja asiye mwana harakati. Kisha anitajie mwanaharakati ambaye si kiongozi.

Kwa nini?
1. Kwa lugha ya kawaida uanaharakati maana yake ni imani au ushawishi (conviction and commitment) katika jambo fulani analolisimamia mtu na kulipigania. Msimamo huo ndio unaomtofautisha mtu huyo na watu wengine.

2. Kama dhana hii hapo juu ni sahihi, unawezaje kuwa na kiongozi asiyekuwa na msimamo au jambo analolisimamia?

3. Kiongozi asiye na harakati ni kama "boga boga" hivi, yupo yupo tu. Na mwanaharakati asiye na uongozi ni kama msafiri asiyejua aendako. Uanaharakati na uongozi haviachani. Taifa letu linahitaji vyote yaani viongozi wenye harakati (mzigo wa maono).

Kuushetanisha uanaharakati ni kushetanisha maendeleo. Hakuna maendeleo bila harakati (passion and commitment). Kutetea uongozi usio na harakati ndani yake ni kustawisha uzembe, umwinyi, umangimeza, mazoea kandamizi na uongozi usio na matokeo chanya. Tunapowatetea viongozi waliofanya mambo makubwa, tusiwatenge na harakati.

Bwana Yesu na Mitume wote maarufu wa dini zinazojulikana, walikuwa wana harakati. Uana harakati ni kutoridhika na hali ya mambo inavyokwenda na kuamua kuchukua hatua kuibadilisha. Uana harakati ni uchochezi mtakatifu.

Natamani kuwa mwana harakati. Kungekuwa na duka linauza harakati, ningeenda kununua. Bahati mbaya hakuna duka, hakuna dawa, bali uana harakati hupatikana kwa mtu kujenga nidhamu ya kutathmini, kujitambua, kuhoji na kuchukua hatua.
correct
 
Back
Top Bottom