Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Magazeti ya kesho, yapigwe marufuku mtu kununua magazeti zaidi ya matatu.

Watu wengi wamekosa hotuba ya leo kwa sababu sehemu kadhaa zilikosa umeme. Hivyo, kesho muuza magazeti ukiruhusu mtu anunue mengi kwa mkupuo, wakati hujui anapeleka wapi, kuna hatari ya kuwa yamenunuliwa na mtu ambaye hataki hotuba ya Askofu Gwajima isambae na huenda anafanya kampeni yachomwe moto huko anakoyapeleka.

Ni lazima tuwe wabunifu ku-preempty technicalities kama hizi.

Viva Askofu Gwajima, viva mwana-JF kwa kunielewa.

ahahahahaaaaa, hilo nalo neno?
 
Hivi gwajima ana utakatifu UPI wa kusema wengine,majini yke ndo yanamdaidia kumuongoza lowasa anazani hatujui,

Kwani wewe huwa unatumia utakatifu UPI mpaka huwa unasema wengine!
 
Na heri uwe mpumbavu na lofa kama unaamini mtu mwenye kashfa kubwa ya ufisadi atafanya hayo unayotegemea pole

Slaa alisema CCM ni choo...
Anyway, waliotajwa na Slaa kwamba ni mafisadi walikuwa 11, Hao 10 wako wapi..?? Au mtu anaonekana fisadi zaidi akiwa nje ya CCM..??? Huyo Magufulu ana haya yafuatayo..
1. Alitulipisha wale samaki wa Magufulu...
2. Alitulipisha kwa mwenye kituo cha mafuta cha Total pale Mlimani city
3. ALitulipisha hela kwa mwenye kituo cha mafuta kule Mwanza kwa ubomoaji
4. Nyumba za Serikali zilizouzwa ana kashfa nazo...
5. Ripoti ya CAG ilionyesha kupigwa kwa hela ya barabara kwa maelezo kwamba wamelipwa wakandarasi
 
Gwajima hakwenda kujibu ishu za Ufisadi kwa sababu sio ishu aliyoshambuliwa kwayo na slaa

Alikua anajibu ishu ya yeye kuitwa mshenga na kuwa yeye ndiye aliyemwombea Lowasa kuingia CHADEMA

Nashukuru kwa kumwelewesha Samurai kwani hajamwelewa Gwajina.
 
Binafsi siamini kama hizo ni busara za kiongozi wa kanisa. GWAJIMA anatusaidia wa TZ kufanya maamuzi sahihi. Ikiwa WALUTERI nyuma yao kuna viongozi kama hawa. nchi itaingia katika SHIDA.
 
Gwajima kuoji uadirifu wa slaa yeye anauadirifu UPI? Wakati anatumia miujiza ya kipepo,na ndo msaada wa lowasa kungaisha nyota take,
 
Viongozi wa dini waache kuwagawa watu, viongozi wa madhehebu mengi tu wameamua kukaa kimya ili kuepusha mifarakano miongoni mwa waumini wao.
 
Ndugu watanzania wote ungana nami kwa Taarifa za Uhakika kutoka katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Askofu Gwajima sasa hivi.

Vituo vya TV vilivyoko hewani ni Channel 10 na Sibuka TV

More updates to follow!

12:28 PM
Waandishi wa habari waliofika mpaka ni kutoka:
Radio:
BBC, DW, RADIO ONE, CLOUDS FM, EAST AFRICA RADIO, WAPO RADIO na E-fm

Television:
Clouds Tv, Channel 10, Mlimani Tv, EA TV na Sibuka Tv

Bado waandishi wanaingia kwa wingi!

UPDATE
Askofu Gwajima ameshafika hapa Landmark Hotel, wageni na waandishi wanamsubiri Ukumbini
=========

Mshenga ndio huwa anatumwa na mposaji, kwa hio siri zote za mposaji anazo mshenga lakini alikosea tu kwamba, mimi kusaidia kumleta mzee Lowassa CHADEMA ni kazi ya Mungu kwa sababu Biblia inasema heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Kwa hio, kwa desturi wanasiasa huwa hawaelewani mpaka wapate mtu wa kuwaleta pamoja kwa sababu wanasiasa wanageukana muda wowote.

Kwa sababu hio mimi nilisimama pale sio kwa sababu ni bora kuliko wengine lakini kwa sababu nilikuwa mtu sahihi kwa wakati ule kuwaleta pamoja hawa wanasiasa wawili na wengine ili kusudi tukomboe taifa letu kama ilivyokuwa kiu ya Dk. Slaa. Kwa hio nikawakutanisha pamoja, nilianza na Dk. Slaa mwenyewe mpaka ikafika sasa Slaa mwenyewe akaniita twende tukamwone mwenyekiti, tukaonana na mwenyekiti kukawa na mazungumzo ya muda mrefu baadae wakakubaliana vizuri.

Mpaka tarehe 26/07/2015 siku ambayo mheshimiwa Edward Lowassa alikuwa anaingia CHADEMA, kulikuwa na mkutano uliofanyika pale bahari beach hotel, kwa hio usiku ule Mheshimiwa Lowassa alikuwa anakuja kuingia CHADEMA kwa maana ya kuonana na kamati kuu ya CHADEMA. Na kwa sababu mimi namediate niko katikati, ni vizuri niwepo ili nihakikishe mheshimiwa Edward Lowassa ameingia CHADEMA kwa usahihi, hajaonewa na hajamuonea Dk. Slaa.

Tulikwenda mpaka kamati kuu ya CHADEMA, nataka niongee kwenye platform ya mtumishi wa Mungu kwa sababu wanasiasa wanaweza kudanganya lakini mimi nilikwenda mpaka nikawaomba watu wa CHADEMA, mimi si mmoja ya kamati kuu ya CHADEMA, nawaomba mniruhusu niingie kamati kuu ili nihakikishe mheshimiwa Edward Lowassa amefika salama.

Na hili jambo ni la kawaida, mtu anaweza kusema ulikuwa mchungaji ulifanyaje hivyo! Siku zote wanaogombea Urais, siasa, vyeo, nafasi, power, ukurugenzi wanaanzia kwa waganga wa kienyeji, wanazindikwa, wanachanjwa chale. Ni jambo zuri kama mtu ameanzia kwenye nyumba za ibada. Na mtu hatakiwi aone jambo hili ni baya, ni zuri kuliko yote badala ya kuanzia kwa waganga wa kienyeji, ameanzia kwenye nyumba ya ibada.


Gwajima anaonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu kustaafu kwake siasa

Gwajima: Kama Dr. Slaa anakaja aje atoke hapa akane aone mambo ya mshenga yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.

Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe rose garden. Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. Alisema ameshawaambia watu yeye atakuwa first lady, siku iliyofata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.

Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi tena. Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hio sio kwa mumuone Slaa mbaya. Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea milele.

Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.

Mchungaji Max: Ilifika mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo, yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. Mpaka juzi nilikuwa nawasiliane nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi kuchomoka.

Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa mkewe, Dr tumeshampoteza.

Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia, nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi kuona mambo haya. Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini, mashetani yalikuwa yanamrudia.

Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna tatizo limetokea.

Slaa Serena alisema kwenye mkutano wa CHADEMA watu waliletwa na malori na mabasi, mlioenda mjiulize ni kweli? Mtu anaesema uongo wa mchana, anasema Gwajima anasema maaskofu wa katoliki wamepewa hela. Kanisa katoliki ndio kanisa credible sana duniani.

Kwanini Slaa amesema! Kwanza kuwaondolea credibility, maaskofu hawa wamemsomesha, leo maaskofu 30 anawasingizia. Kwa mtu unaemuamini Slaa unaweza kusema anasema kweli lakini nimekuonyesha mazingira kwanini!

Anatukana maaskofu wa protestant na katoliki, nani aliemtuma! Slaa aliulizwa unalindwa na usalama wa taifa? Alisema kweli, watu wa usalama wanambeba kwenda Serena, Azam na Star Tv kutukana maaskofu. Maaskofu hawaruhusiwi kujihusisha na siasa lakini ni wapiga kura, Je, atakupa kura! Je waumini wao watakupa kura! Strategy hii imeshindikana wafikirie nyingine. Bahati mbaya hii ilikuwa silaha yao ya mwisho.

Mababa askofu wa kanisa katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa, anasema nilikuwa nazunguka kwenye ndege na Lowassa. Mimi nina ndege yangu na siombi kibali kuzungumza mtu.

Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie ndio mnatukana maaskofu, usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee kampeni zake kwa amani.

Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha, nitasema Slaa alivyokutana na watu wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama mtapomuongoza tena huyo mtu wenu wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na macho yenu hamtafungua tena

Uadalifu wa Slaa
Gwajima: Alisema baba askofu lazima mtubu, najiuliza yeye ni msafi kuliko sisi? Slaa aliacha wito ambalo ni tatizo tayari, zaidi ya kuacha wito ukaoa! Nikija tena nitaleta watoto aliowazaa na uhusiano wa yeye kutoka. Ukaa na mke na watoto ukatelekeza, haitoshi ukaenda kuoa mke wa mtu mwingine. Kamili akaweka zuio mahakamani.

Slaa alisema Ridhwani nauza madawa ya kulevya, leo Slaa ndio anao aliowasema, anaemuongoza Slaa akome na akome kabisa. Watu wa usalama kazi yenu ni kulinda nchi iwe na amani na sio kuichafua.

Kinachosumbua ni wakati na majira, 20 kabla ya kristo kulikuwa ana mtu aliehubiri ubudha, akaijaza Ubudha kwa sababu yalikuwa majira yake. Baada ya hapo, karne ya kwanza alitokea Yesu kristo na kukutana na upinzani wa ajabu, ukifika wakati waksema wamemkamata.

Kweli ukiizika ina tabia ya kufufuka na ukiizika haiwezi kufa tena, akaja kutokea Mtume Muhammad japo alipata upinzani mkubwa leo Uislam umeenea sana. Nami niseme mfate majira, msishindane nayo. Tanzania ni kubwa kuliko watanzania.


UPDATE
Askofu Gwajima amemaliza Press Conference na waandishi wa habari na alipokua akiondoka na gari yake aina ya Hummer watu wengi wakijipanga kando ya barabara huku bodaboda wakimfuata kwa nyuma wakiimba kuwa yeye ni JEMBE na kumpigia makofi
Hapo kwenye nyekundu, naona hili ni shambulizi limepelekwa kwa viongozi wa kanisa katoliki, na naona huyu jamaa ana jambo na viongozi wa kikatoliki baada ya kumporomoshea matusi kiongozi mkuu wa kanisa hilo , sasa anawashambulia makasisi wa kanisa hilo kwa staili nyingine. Huyu mtu ni hatari kwa amani ya nchi yetu.
 
mkristo wa kweli na mchungaji wa kweli mbele za mungu anayajua haya....

Mathayo 18

1 saa ile wanafunzi wakamwendea yesu
wakisema,
2 ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa
mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka
katikati yao,
3 akasema, amin, nawaambia,
msipoongoka na kuwa kama vitoto,
hamtaingia kamwe katika ufalme wa
mbinguni.
4 basi, ye yote ajinyenyekeshaye
mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye
aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
5 na ye yote atakayempokea mtoto mmoja
mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea
mimi;
6 bali atakayemkosesha mmojawapo wa
wadogo hawa waniaminio, yamfaa
afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia,
na kutoswa katika kilindi cha bahari.
7 ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya
mambo ya kukosesha! Maana hayana budi
kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake
mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!
8 basi mkono wako au mguu wako
ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe;
ni afadhali kuingia katika uzima hali
umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko
kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na
kutupwa katika moto wa milele.
9 na jicho lako likikukosesha, ling'oe,
ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia
katika uzima una chongo, kuliko kuwa na
macho mawili, na kutupwa katika jehanum
ya moto.
10 angalieni msidharau mmojawapo
wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya
kwamba malaika wao mbinguni siku zote
huutazama uso wa baba yangu aliye
mbinguni.
11 [kwa maana mwana wa adamu alikuja
kukiokoa kilichopotea.]
12 mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia,
mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa
na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta
yule aliyepotea?
13 hata akipata kumwona, amin,
nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko
wale tisa na tisini wasiopotea.
14 vivyo hivyo haipendezi mbele za baba
yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa
wadogo hawa apotee.
15 na ndugu yako akikukosa, enenda
ukamwonye, wewe na yeye peke yenu;
akikusikia, umempata nduguyo.
16 la, kama hasikii, chukua pamoja nawe
tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa
vya mashahidi wawili au watatu kila neno
lithibitike.
17 na asipowasikiliza wao, liambie kanisa;
na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako
kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.



mithali 25:9
ujitetee na mwenzako peke yake; bali
usiifunue siri ya mtu mwingine.

well said
 
Hivi bado una muona Gwajima kwamba ni mchungaji,Kweli Shetani amekupiga upofu.Huyo ni mtumishi wa Shetani kabisa.Biblia inasema "mtawafahamu kwa matendo yao." Matendo ya Gwajima sio ya mtoto wa Mungu kabisa.Sina haja kuyataja, unayajua.Biblia inaongeza kusema,"tokeni kati yao mkatengwe na nao."Toka huko,utaishia jehanam.

Mtumishi wa SHETANI nimjuae mimi ni ccm. Tanzania bila ccm inawezekana, Tushirikiane kumtokomeza huyu MKOLONI MWEUSI ccm aka FISIEM.
 

Attachments

  • attachment-18.jpeg
    attachment-18.jpeg
    7.3 KB · Views: 673
Kiongozi wa kiroho anazungumzia matatizo ya ndoa za watu kwasababu ya siasa ......Alafu badala ya kuja kukanusha maswali ya Dr Slaa anakuja kusema mambo ya ndani ....haya ndio matatizo ya uaskofu wa kupeana na mkeo .....maadili zero ....

Mtazamo ni kweli kabisa, na sisi tulivyo majuha tunashangilia tu. kama yeye Gwajima ni kiongozi wa kiroho, na hata kama anajua matatizo ya ndoa ya Slaa hakupaswa kuzungumzia hadharani tena kwa kumkomoa . Yeye mbona bado anayo skendo tena mbichi ya kuvunja ndoa ya muumini wake? Yeye atuambie kweli ni mshenga? na anahusikaje na shutuma za Slaa?
 
Back
Top Bottom