Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

uchaguzi uliogubikwa na udini.
Padri mstaafu vs Askofu gwajima.
mmoja anadaiwa kuchepuka, mwingine 'mshenga' wa mwanasiasa.
Viongozi wa dini katikati ya vijembe vya siasa za uchaguzi.
Maneno wnayoongea ni vizuri tuanze kuwakagua
viongozi wetu wa dini. Ni kweli hicho wanachohubiri ndio wanachomaanisha?
Ni zamu ya viongozi wa dini ndani ya ulingo wa siasa.

Napata kichefuchefu kwa haya yanayotokea. Ni msiba kwa jamii. Jamii inayoamini babu ambilikile Mwasapile ni mponyaji wa ukimwi. jamii inayoshabikia umbea na kuacha mambo ya msingi ya Taifa. iwavyo vyovyote hoja za ufisadi wa lowasa alizozeeleza Dr. Slaa hakuna wa kuzisafisha.
 
Me nmemuonea huruma babu jamani daaah ananyanyasika kweli nasikia kwa siku anapewa sh 5000 tu ya matumizi mweeeeeeee uonevu huu jaman
 
Bora UISLAM ukiwa Na DHAMBI zako unakaa peke yako Na MUNGU wako unatubu.. lakini mambo ya KUUNGAMA maaskofu wenyewe ndo kama hawa. mkikosana so ANAKUANIKA!!!!!
 
Gwajima ni mnafiki, kaeleza dr ni mzizi na alichukua mke wa mtu, lakini hasemi ya kwake na flora mbasha.
Askofu, tena anajiita kiongozi wa roho anarecord mazungumzo ya mtu ambaye amemfuata kufanya confession

Hio ndo dawa ya msaliti,ni kumrecord....
 
Gwajima ana haki kabisa ya kujitokeza kumjibu Dk Slaa kwa sababu Dk Slaa alimhusisha Gwajima pale Serena kwanza, alimhusisha Gwajima kuwa ndiye aliyemwambia kuwa maaskofu wamehongwa, hili halikupaswa kujibiwa na Askofu yeyote isipokuwa Gwajima na sasa amejibu kuwa hakuna Askofu aliyehongwa hivyo muwaache maaskofu! Nadhani Dk Slaa angejikita kupambana na Lowasa bila kumgusa Gwajima asingejitokeza!
Lakini hizo habari za maaskofu kuhongwa pia Dr. Slaa alielezwa na Tundu lissu kutoka kwa Gwajima.
 
Hivi bado una muona Gwajima kwamba ni mchungaji,Kweli Shetani amekupiga upofu.Huyo ni mtumishi wa Shetani kabisa.Biblia inasema "mtawafahamu kwa matendo yao." Matendo ya Gwajima sio ya mtoto wa Mungu kabisa.Sina haja kuyataja, unayajua.Biblia inaongeza kusema,"tokeni kati yao mkatengwe na nao."Toka huko,utaishia jehanam.

Mungu Akusamehe Hujui unalolitenda
 
Bora UISLAM ukiwa Na DHAMBI zako unakaa peke yako Na MUNGU wako unatubu.. lakini mambo ya KUUNGAMA maaskofu wenyewe ndo kama hawa. mkikosana so ANAKUANIKA!!!!!

..umeelewa chanzo au unakurupuka tu.!
 
naona watu mnamshambulia sana Gwajima..binafsi press conference yake alikuwa anclear the Air Mosi ni kuhusu shtuma kwamba ni Gwajima ndo alifanya mpango wa Lowassa kuja CDM wakti aliyeanzisha ni Slaa mwenyewe. Pili ni kuhusu kauli kuwa Slaa kaamua wilingly kuachana na siasa after CDM kumpokea Lowassa wakati kumbe ni Josephine ndo kashinikiza. Tatu kuhusu tuhuma za maaskofu kuohongwa na pia ka mnakumbuka ile press conference Slaa alisema kuna Bishop alipigaa simu mbele yake akiwa na Gwajima akitaka naye mgao as if Gwajima alikuwa anapioneer huo mgao. Gwajima hawezi kujibu kuhusu hoja za ufisadi za Lowassa maana hapo yeye c msemaji thou naona watu wanashadahia kuhusu ishu za ufisadi..hizo yampasa Lowassa ajibu n not Gwajima

Uko sahihi Mkuu pia Dr. Slaa anatakiwa akanushe kama aliyosema Gwajima si ya kweli.
Ila kwa vielelezo na ushahidi tuliousikia leo ni bora Dr. Slaa angekaa kimya tu kwani imejidhihirisha wazi kua tatizo ni shinikizo toka kwa Mkewe na inaonekana Gwajima anafahamu mambo mengi sana juu ya Dr. Slaa.
 
Bora UISLAM ukiwa Na DHAMBI zako unakaa peke yako Na MUNGU wako unatubu.. lakini mambo ya KUUNGAMA maaskofu wenyewe ndo kama hawa. mkikosana so ANAKUANIKA!!!!!
Na hakuna maandiko yanayoonyesha ukikosa uende kwa baba askofu au mchungaji au padre kutubu. Bali ujifungie chumbani ili naye baba akuonaye sirini akusamehe ikiwa ni pamoja na kufunga na kuomba.
 
Napata kichefuchefu kwa haya yanayotokea. Ni msiba kwa jamii. Jamii inayoamini babu ambilikile Mwasapile ni mponyaji wa ukimwi. jamii inayoshabikia umbea na kuacha mambo ya msingi ya Taifa. iwavyo vyovyote hoja za ufisadi wa lowasa alizozeeleza Dr. Slaa hakuna wa kuzisafisha.

..hoja zipi?! zile za Mwakyembe alivyo muhukumu lowassa bila kumpa nafasi ya kujitetea ili kumlinda JK au kuna nyingine.?!
 
Ndugu watanzania wote ungana nami kwa Taarifa za Uhakika kutoka katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Askofu Gwajima sasa hivi.

Vituo vya TV vilivyoko hewani ni Channel 10 na Sibuka TV

More updates to follow!

12:28 PM
Waandishi wa habari waliofika mpaka ni kutoka:
Radio:
BBC, DW, RADIO ONE, CLOUDS FM, EAST AFRICA RADIO, WAPO RADIO na E-fm

Television:
Clouds Tv, Channel 10, Mlimani Tv, EA TV na Sibuka Tv

Bado waandishi wanaingia kwa wingi!

UPDATE
Askofu Gwajima ameshafika hapa Landmark Hotel, wageni na waandishi wanamsubiri Ukumbini
=========

Gwajima anaonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu kustaafu kwake siasa

Gwajima: Kama Dr. Slaa anakaja aje atoke hapa akane aone mambo ya mshenga yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.

Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe rose garden. Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. Alisema ameshawaambia watu yeye atakuwa first lady, siku iliyofata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.

Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi tena. Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hio sio kwa mumuone Slaa mbaya. Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea milele.

Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.

Mchungaji Max: Ilifika mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo, yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. Mpaka juzi nilikuwa nawasiliane nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi kuchomoka.

Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa mkewe, Dr tumeshampoteza.

Gwajima: Siku moja nilikuwa Korea, Slaa alisema mkewe amedondoka amezimia, nikaomba kwenye simu mkewe akaanza kupiga kelele, nilimwambia Dr. Slaa sijawahi kuona mambo haya. Nilikuwa namsindikiza mke wangu kwenda London, cha kushangaza nikamkuta mke wa Dr Slaa airpot amekuja kusindikiza, umeambiwa na nani! Akasema nimejisikia tu! Baada ya check in, kurudi mke wa Dr. Slaa alidondoka chini, mashetani yalikuwa yanamrudia.

Siku nyingine Slaa alinipigia simu mkewe amedondoka, haya ni mashetani, Slaa anaongozwa na mwanamke wa aina hii. Ikulu pangekalika? Slaa si yeye, kuna tatizo limetokea.

Slaa Serena alisema kwenye mkutano wa CHADEMA watu waliletwa na malori na mabasi, mlioenda mjiulize ni kweli? Mtu anaesema uongo wa mchana, anasema Gwajima anasema maaskofu wa katoliki wamepewa hela. Kanisa katoliki ndio kanisa credible sana duniani.

Kwanini Slaa amesema! Kwanza kuwaondolea credibility, maaskofu hawa wamemsomesha, leo maaskofu 30 anawasingizia. Kwa mtu unaemuamini Slaa unaweza kusema anasema kweli lakini nimekuonyesha mazingira kwanini!

Anatukana maaskofu wa protestant na katoliki, nani aliemtuma! Slaa aliulizwa unalindwa na usalama wa taifa? Alisema kweli, watu wa usalama wanambeba kwenda Serena, Azam na Star Tv kutukana maaskofu. Maaskofu hawaruhusiwi kujihusisha na siasa lakini ni wapiga kura, Je, atakupa kura! Je waumini wao watakupa kura! Strategy hii imeshindikana wafikirie nyingine. Bahati mbaya hii ilikuwa silaha yao ya mwisho.

Mababa askofu wa kanisa katoliki hawakupewa rushwa wala mimi sijapewa rushwa, anasema nilikuwa nazunguka kwenye ndege na Lowassa. Mimi nina ndege yangu na siombi kibali kuzungumza mtu.

Usalama wa taifa sio wa CCM, mnatafasiriwa nyie ndio mnatukana maaskofu, usalama wa taifa mnamuharibia Magufuli, mwacheni aendelee kampeni zake kwa amani.

Siku nitakayorudi kumjibu Slaa akinisemesha, nitasema Slaa alivyokutana na watu wa usalama wa taifa Afrika kusini. Usalama mtapomuongoza tena huyo mtu wenu wenu atukane maaskofu, nitawalipua na bomu na macho yenu hamtafungua tena

Uadalifu wa Slaa
Gwajima: Alisema baba askofu lazima mtubu, najiuliza yeye ni msafi kuliko sisi? Slaa aliacha wito ambalo ni tatizo tayari, zaidi ya kuacha wito ukaoa! Nikija tena nitaleta watoto aliowazaa na uhusiano wa yeye kutoka. Ukaa na mke na watoto ukatelekeza, haitoshi ukaenda kuoa mke wa mtu mwingine. Kamili akaweka zuio mahakamani.

Slaa alisema Ridhwani nauza madawa ya kulevya, leo Slaa ndio anao aliowasema, anaemuongoza Slaa akome na akome kabisa. Watu wa usalama kazi yenu ni kulinda nchi iwe na amani na sio kuichafua.

Kinachosumbua ni wakati na majira, 20 kabla ya kristo kulikuwa ana mtu aliehubiri ubudha, akaijaza Ubudha kwa sababu yalikuwa majira yake. Baada ya hapo, karne ya kwanza alitokea Yesu kristo na kukutana na upinzani wa ajabu, ukifika wakati waksema wamemkamata.

Kweli ukiizika ina tabia ya kufufuka na ukiizika haiwezi kufa tena, akaja kutokea Mtume Muhammad japo alipata upinzani mkubwa leo Uislam umeenea sana. Nami niseme mfate majira, msishindane nayo. Tanzania ni kubwa kuliko watanzania.


UPDATE
Askofu Gwajima amemaliza Press Conference na waandishi wa habari na alipokua akiondoka na gari yake aina ya Hummer watu wengi wakijipanga kando ya barabara huku bodaboda wakimfuata kwa nyuma wakiimba kuwa yeye ni JEMBE na kumpigia makofi

mkuu naweza pata clip ya hii kitu. if you are interested check me P.m
samahani kwa usumbufu Asante..
 
Magazeti ya kesho, yapigwe marufuku mtu kununua magazeti zaidi ya matatu.

Watu wengi wamekosa hotuba ya leo kwa sababu sehemu kadhaa zilikosa umeme. Hivyo, kesho muuza magazeti ukiruhusu mtu anunue mengi kwa mkupuo, wakati hujui anapeleka wapi, kuna hatari ya kuwa yamenunuliwa na mtu ambaye hataki hotuba ya Askofu Gwajima isambae na huenda anafanya kampeni yachomwe moto huko anakoyapeleka.

Ni lazima tuwe wabunifu ku-preempty technicalities kama hizi.

Viva Askofu Gwajima, viva mwana-JF kwa kunielewa.
 
Gwajima anasema mini yeye ni misukule take,anazani hatujui
 
Mi nadhani upumbavu ni kuamini kwamba...
1. Magufuli anashangaa Tanga hadi Mtwara hakuna kiwanda kikubwa cha samaki... ANAMSHANGAA NANI..??? CCM, wananchi au JK..??
2. Magufuli anashangaa duka la nje ya hospitali kuna dawa wakati hospitali haina dawa... ANAMSHANGAA NANI..??? CCM, wananchi au JK..??
3. Magufuli anashangaa wiki ya maji wakubwa wana maji na wadogo hawana hata tone... ANAMSHANGAA NANI..??? CCM, wananchi au JK..??

KWA VILE NILIAMINI GRID YA TAIFA INGEJENGWA SONGEA, KAGERA NA KIGOMA, NA HAIJAJENGWA, NITAKUWA MPUMBAVU NA LOFA KAMA MTU WA KUTOKA CHAMA KILE KILE ANATOA AHADI VILE VILE


Na heri uwe mpumbavu na lofa kama unaamini mtu mwenye kashfa kubwa ya ufisadi atafanya hayo unayotegemea pole
 
Mimi simuelewi kabisa huyu Gwajima, sasa yy ni mchungaji/au ni kada wa Chadema, anaongea mambo ya kisiasa kabisa na kutetea hija za kisiasa wakati yeye ni mtu wa dini, au ndo ametumwa na CHADEMA katika harakati za kuzima hoja za Slaa, anajimaliza kabisa kiroho, na wala waumini wenye uelewa wasigeweza kumuamini tena....ya kaisari mwachie kaisari na ya Mungu ampe Mungu


Ulitakiwa uhoji hili ulipomuona pale uwanja wa Sheik Abeid Karume Arusha. Chopa ilipozinduliwa na mbona bado yuko? inamaanaa EL ni swahiba wake na yeye ndio yule POPOTE ALIPO NA YEYE YUPO UKO HAPO?
 
Back
Top Bottom