Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Askofu Josephat Gwajima amjibu Dr. Slaa

Naona Gwajima anachonganisha zaidi.

Hachonganishi ila anasema ukweli il kuliokoa taifa kutokana na uozo wa vyombo vyetu vya usalama.

Vyombo vya Usalama sio vya CCM ni kwa ajili ya Taifa lote na watu wote wa nchi hii.
 
Exactly Mkuu,yan Ukawa Wanabaki Kushambulia Familia Ya Dr. Instead Ya Kujibu Hoja..Huyu Gwajima Atueleze Watz Kwanin Wewe Kiongoz Wadin Ujihusishe Na Siasa Tena Direct Kabisa?Hata Amiri Jesh Mkuu Anaweza Kuendeshwa Na Mkewe Sembuse Slaa,familia Ngap Kanisan Kwake Zinamatatizo Nazo Hzo Anazitangazaga Hadharan?

Unataka hoja gani mkuu uelezwe? Dr. Mihogo alimuhusisha Gwajima katika maelezo yake,so Gwajima amekuja kuelezea upande wa pili. The motive behind ya Dr. Mihogo ni kukosa "URAIS" wala siyo uchungu dhidi ya Ufisad. Gwajima ameweka wazi A to Z ya jinsi shinikizo la Dr. Mihogo lilipoanzia hadi kujitoa,siyo uongo wa kusema "Lowassa" ndiyo chanzo. Jaribu kupenda kusikia kile usichotaka kusikia.
 
Hadi nakuonea Huruma ndugu yangu. Pole sana hayo ni mapito tu. You will be OK after sometime. Maana naona umepanic sana.

Hii ni maigizo tu!
Kwanza tangu awali Slaa alikiri kuwa nyumba anayoishi alinunua kwa michango ikiwemo ya Mbowe!

Leo Gwajima anasema kuwa mke ndiye mwenye nyumba na alimfungia virago vyake!
How comes????

Slaa alikataa hajawahi kubadili mawasiliano yake
Je Gwajima kwanini sasa atoe SMS ya namba nyingine?

Hivi si huyu Gwajima aliyemnyang'anya Mbasha mke?
 
Gwajima inabidi aachene na uaskof aingie kwenye siasa.
 
  • Thanks
Reactions: nao
Gwajima hajajibu hoja zaidi ya vijembe umbeya
 
"Embu waza mtu ambae hujaoana nae, hamjafunga ndoa ana uwezo wa kukuzuia usiingie CHADEMA, je huyo mwanamke akiolewa akawa na cheti cha ndoa??"

~By Mch. Gwajima
 
Exactly Mkuu,yan Ukawa Wanabaki Kushambulia Familia Ya Dr. Instead Ya Kujibu Hoja..Huyu Gwajima Atueleze Watz Kwanin Wewe Kiongoz Wadin Ujihusishe Na Siasa Tena Direct Kabisa?Hata Amiri Jesh Mkuu Anaweza Kuendeshwa Na Mkewe Sembuse Slaa,familia Ngap Kanisan Kwake Zinamatatizo Nazo Hzo Anazitangazaga Hadharan?

reason ya Gwajima kuamua kuitisha press conference ni hoja zilizotolewa na Dr. Mihogo kua Gwajima ni mshenga
 
Hatuhitaji hayo anayoyazungumzia huyo,, Tunachohitaji ajibu yale yaliyotoka kwenye mdomo wa dr slaa na sio masuala binafsi ya familia ya dr,, dr alisema LOWASSA ni fisadi kwa sababu a,b na c na gwajima alikuwa mshenga mpaka akasema maaskofu 30 kati ya 34 wamehongwa sasa gwajima anatakiwa ayatolee haya ufafanuzi kwa ushahidi na sio kupiga porojo zilezile za akina mbatia, alete ushahidi kwanini LOWASSA sio fisadi na awalete hao maaskofu wale viapo na si hizi porojo..
 
Ndugu watanzania wote ungana nami kwa Taarifa za Uhakika kutoka katika Mkutano wa Waandishi wa Habari na Askofu Gwajima sasa hivi.

Vituo vya TV vilivyoko hewani ni Channel 10 na Sibuka TV

More updates to follow!

12:28 PM
Waandishi wa habari waliofika mpaka ni kutoka:
Radio:
BBC, DW, RADIO ONE, CLOUDS FM, EAST AFRICA RADIO, WAPO RADIO na E-fm

Television:
Clouds Tv, Channel 10, Mlimani Tv, EA TV na Sibuka Tv

Bado waandishi wanaingia kwa wingi!

UPDATE
Askofu Gwajima ameshafika hapa Landmark Hotel, wageni na waandishi wanamsubiri Ukumbini
=========

Gwajima anaonyesha meseji aliyotumiwa na Dr. Slaa kuhusu kustaafu kwake siasa

Gwajima: Kama Dr. Slaa anakaja aje atoke hapa akane aone mambo ya mshenga yalivyo, watu wanashangaa Slaa anaweza kufanya haya! Si yeye ni mama. Slaa alikuwa adili, sasa uzoefu wa ndoa hana, bora sisi wachungaji tunaoa.

Nilimpa maneno ya matumaini, nitamtafuta mkewe niongee nae, nilimtafuta mkewe rose garden. Nilianza mimi kumbembeleza amruhusu baba aendelee na hayo maelezo nimeyarokodi na mimi ni mtu wa kurekodi. Alisema ameshawaambia watu yeye atakuwa first lady, siku iliyofata tarehe 28, nilimuita yule mama Kibo complex.

Tukakaa ndani ya gari yake, nilikuwa mimi na mtu mwingine, niliendelea kurekodi tena. Ilikuwa ni siku Lowassa anapokea kadi bahari beach, nawaonyesha hio sio kwa mumuone Slaa mbaya. Saa nane mchana akasema nimekubali Slaa arudi aingie kazini kwa sharti mkutano wa kumpokea Lowassa ufutwe. Nikamwambia hilo halitatokea milele.

Watu wengi sana wametumwa kuongea na yule mama, akiwemo mzee Ndesamburo ambae alishindwa kumpata yule mama, kumbe yule mama anaongea kwa karibu sana na mchungaji Max hivyo akampeleka Ndesa.

Mchungaji Max: Ilifika mahali chama kiliacha majukumu yote kumpata yule mama kuongea na Ndesamburo, yule mama alisema CHADEMA wanacheza mpaka waongee nami, alisema CHADEMA ni waongo na wanafiki, kwanini watufanya mpaka tumekosa urais. Mpaka juzi nilikuwa nawasiliane nae lakini maongezi yake kwa ujumla anasema kwanini wameachwa kugombea Urais, kwa jinsi alivyokuwa anaongea nikajua hata Dokta hawezi kuchomoka.

Slaa alisema Josephine amemfungia Serena, ukweli mimi naufahamu, ishu ipo kwa mkewe, Dr tumeshampoteza.

Gwajima:


UPDATE
Askofu Gwajima ahoji..."Kama Dr Slaa anaongozwa na kuendeshwa na mke wake kiasi hiki, Je angekua Rais nchi ingeongozwa na mke wake?"

Askofu pia anasema ....."Dr Slaa wa leo sio Dr Slaa wa mwaka mmoja uliopita!"

UPDATES
Askofu Gwajima awaonya Usalama wa Taifa kuegemea upande mmoja wa Chama cha Mapinduzi katika kampeni za Uchaguzi zinazoendelea asema hiki ni chombo cha dola kinatakiwa kusimamia watu wote na sio kuwa upande wa CCM

Gwajima ndo afisa habari wa chadema kumbe!!
 
Hili la Ridhwani Kuuza Madawa ya Kulevya sijalipenda Wakuu ... Hiyo ilikuwa unnecessary information ..
 
Duh Tslaa heri angejinyamaziaga tu...,
Haaa.mbona wamekata matangazo ghafulaaa?!
 
Baada ya kutajwa Ridhwan Kikwete Channel 10 imezimwa ... Dah! Kazi ipo Mwaka huu
 
Back
Top Bottom