Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,010
- 9,875
Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CCM, Askofu Josephat Gwajima amesema ana jina la kiislamu ambalo ni Rashidi Gwajima.
Amesema alipata jina hilo baada ya kutelekezwa kwenye msikiti ambapo pia alisema waislamu ndio waliomsomesha katika miaka yake ya awali.
Kutokana na suala hilo Gwajima amesema alipata sababu ya kuusaidia uislamu hata alipokwenda Dar aliwasaidia kujenga visima vya maji.
Gwajima aliyasema hayo alipokuwa kwenye Mahafali ya darasa la saba ya shule ya Al Irshaad.