Sakata la Askofu Gwajima: Simbachawene, Kilangi wawatupia mpira DCI, DPP

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,050
4,904
Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi amesema azimio la Bunge la kutaka vyombo vingine vimchukulie hatua Mbunge wa Kawe (CCM) Askofu Josephat Gwajima linatosha kumfanya Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kuanza uchunguzi wa shauri hilo.

Bunge liliazimia Gwajima na Mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa wasimamishwe kuhudhuria vikao vya mikutano miwili ya Bunge baada ya kuwatia hatiani kwa kusema uongo, kushusha hadhi na heshima ya Bunge.

Wakati wa kuhitimisha adhabu kwa wabunge hao, Spika Job Ndugai alisema Bunge limenawa mikono kwa upande wake, hivyo kinachotakiwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Kilangi kutazama namna wanavyoweza kufanya.

Ndugai alisema kama hawatamhoji mbunge huyo, basi wasishangae kuitwa mbele ya kamati ya maadili ambayo alisema itakuwa na kauli juu yao wenyewe si kazi ya Bunge tena.

Akizungumza katika viwanja vya Bunge baada ya azimio hilo kutolewa, Profesa Kilangi alisema jambo hilo litaangukia chini ya Mkurugenzi Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa sababu ni suala la uchunguzi.

Alisema uchunguzi unalenga kufahamu kama jinai imetendeka kwa shauri la Gwajima ama la.

“Akishafanya uchunguzi wake atalipeleka katika hatua inayofuata ambayo ni kwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP). Naye atapima kuona kama kuna jinai hapa na upo ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kuwa jinai,” alisema.

Alisema akishathibitisha kwamba kuna ushahidi wa kutosha kwa mamlaka yake atafungua kesi mahakamani.

“Lakini ni vyema kutambua mamlaka ya DPP ni mamlaka yasiyoingiliwa na taasisi yoyote, isiyoshinikizwa na taasisi yoyote, kwa hiyo na yeye atajiridhisha. Atakavyokuwa ameona na akiona kuna jinai imetendeka na ushahidi wa kutosha atalipeleka anavyoona inafaa,” alisema.

Alipoulizwa nani anakwenda kushtaki ili uchunguzi uanze, Profesa Kilangi alisema lipo azimio la Bunge linatosha kumfanya DCI kuanza uchunguzi.

Naye Waziri Simbachawene alisema maagizo ya Spika kuhusu kiongozi huyo ameyapokea, lakini hawezi kusema jambo lolote hadi atakaposhauriana na wataalamu wake.

Alisema hawakufanya haraka kumhoji Gwajima kutokana na suala hilo kuwa na mchanganyiko wa masuala ya dini.

“Ni kweli nimemsikia, lakini haya mambo yameunganisha na imani za kidini. Kabla sijasema jambo lolote lazima kwanza nijiridhishe kutoka kwa wenzangu kama tunaona iko haja ya kufanya hivyo ili tusije tukaingilia uhuru wa kuabudu,” alisema.

Hata hivyo, alisema akijiridhisha na kupata ushauri kuwa inawezekana kuhojiwa, basi watamuita na kumhoji ili kupata ukweli wa kauli zake.

Silaa asindikizwa na askari

Hata hivyo, jana Gwajima hakuwepo bungeni wakati mjadala wa suala lake ukiendelea, tofauti na Silaa aliyehudhuria na Spika Job Ndugai alimuamuru atoke nje ya ukumbi wa Bunge huku akiwaagiza askari wamsindikize mbali na viwanja vya Bunge.

Baada ya kauli hiyo, Silaa alisimama na kunyanyua mkoba wake mweusi na kuweka kitabu kimoja ndani ya mkoba huo kabla ya kuchukua simu zake na kutoka huku akiwa amesindikizwa na askari wawili.

Askari hao walimweka Silaa katikati na kuongozana naye hadi nje ya viwanja vya Bunge kwa kupitia lango kuu la kuingilia bungeni.

Chanzo: Mwananchi
 
Samia mwenyewe kapigwa KO huko kawe........

Haya mambo magumu sana na shida nikwamba anauliza chanjo wakati anaowahutubia hawana sosho distansi......
 
Na ni leo tu mama katoka kutia Utata pale kawe..hili sakata litaiacha vibaya sana Serikali hii ya Samia
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Ndugai anapenda ligi bala
Ona sasa complications anazozisababisha. Yeye kama kakuta kuna tatizo kwenye jurisdication yake angedeal nayo hapo kwake basi na sio kuzishinikiza mamlaka zingine! Mbona wengine hawamshinikizi yeye?!
 
Kuna kitu kinachoitwa Nia ya kushitaki (Intention to prosecute).
Viongozi wengi na vyombo vya Dola hushiriki uhalifu dhidi ya uma na hivyo kuwalinda wahalifu kwa maslahi yao kwa jina la uma au taifa (maslahi ya taifa).
Kinachoonekana ni kukosekana kwa nia kwa sababu wanazozijua wao.
Ni muhimu sana kutofautisha viongozi, serikali na taifa hasa wakati wa kuchambua maslahi ya taifa.
 
Ndugai anapenda ligi bala
Na Gwajiboy anapenda ligi balaa!
labda nitoe maoni kidogo.....
swala la Gwajiboy halina jinai yyte ile waache kuzunguka mbuyu......
Ila kwenye madai wanamshitaki vizuri...
kama aliwataja watu (viongozi wa serekali)kwa majina walipokea rushwa basi wanaweza kumshtaki kwa madai katika ubinafsi wao kwa defamation.....
otherwise sioni kosa la jinai
 
Huyu Ndungai atatuletea mgogoro nchini usiokua na ulazima yoyote yaani anapenda kuonyesha umwamba usiokua na faida yoyote. Anapenda kulitumia bunge kublack mail watu.
Labda mama arudie Ile kauli yake kua waache kudemka ndo atasikia.
Uko sahihi anajiona Mungu mtu hata kuingilia mihimili mingine kulazimisha ichukue maamuzi.
Uzuri Leo mama kaupima upepo wa Gwajiboy oyee.
 
Na Gwajiboy anapenda ligi balaa!
labda nitoe maoni kidogo.....
swala la Gwajiboy halina jinai yyte ile waache kuzunguka mbuyu......
Ila kwenye madai wanamkamata....
kama aliwataja watu (viongozi wa serekali)kwa majina walipokea rushwa basi wanaweza kumshtaki kwa madai defamation.....
otherwise sioni kosa la jinai
Hakutaja jina kumbe Gwajiboy Yuko huru Kama molecules.🤣🤣🤣
 
Kwa hyo wamekutana wote wapenda ligi!

Lakin Sirro pamoja na mapungufu yake, alishauri walimalize hili kwa njia ya mazungumzo, bt nashangaa bado wanan'gan'gana nalo!

Au Gwajigirl anampushi faru Ndugai akiwasheee!
Sirro pamoja namapungufu yake ni mstaarabu Sana.

Nakumbuka alipokuwa RPC Mwanza matokeo ya uchaguzi Wenje akidaiwa kuongoza wananchi walitaka kuchoma Moto aliwatuliza vizuri Sana,na Wenje alishinda.
 
Na Gwajiboy anapenda ligi balaa!
labda nitoe maoni kidogo.....
swala la Gwajiboy halina jinai yyte ile waache kuzunguka mbuyu......
Ila kwenye madai wanamshitaki vizuri...
kama aliwataja watu (viongozi wa serekali)kwa majina walipokea rushwa basi wanaweza kumshtaki kwa madai katika ubinafsi wao kwa defamation.....
otherwise sioni kosa la jinai
Gwajiboy kawashika vizuri, uzuri yule siyo muoga
 
..Gwajima angekuwa mpinzani kusingekuwa na danadana za kumkamata tunazozishuhudia sasa hivi.
 
Back
Top Bottom