Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 741
- 479
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma Septemba 3, 2023 Jijini Dar Es Salaam amefungua mashindano ya mchezo wa rede (Gwajima Rede cup) katika jimbo la Kawe.
Akizungumza wakati wa kufungua mashindano hayo, Mwinjuma amesema Serikali inathamini michezo ya aina zote, ambapo ameeleza kuwa, mchezo wa Rede ni miongoni mwa michezo ya jadi ambayo inapewa kipaumbele na itaendelea kuwekewa mazingira bora ili jamii iifurahie mchezo huo.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Askofu Josephat Gwajima yanahusisha timu nane kutoka katika kata za jimbo hilo.