OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,344
Mimi nitachangia hili kama ifuatavyo! Awali Doctor alishaeleza taratibu ambazo zipo kwenye Canon Laws ambazo zilimuwezesha kuacha upadre na kuoa! Pili sio yeye tu ambaye amewahi kuwa padre hata sisi waumini wa kawaida sio rahisi sana kumpata mchumba mara moja na kumfanya mke wengi wetu tumejaribu hapa na pale na hatimaye kupata anayefaa!Na pia wapo wakristu wengi tuu ambao wamefunga ndoa kanisani kabisa lakini maisha yakashindikana ndoa zikavunjika!na muda wa uchumba hauna kikomo, kumbuka doctor amelitumikia kanisa muda mrefu sana ndio maana unaona kama amechelewa kuoa! Pointi kubwa ambayo huyu askofu uchwara ameizungumza na kuitilia mkazo ni kuwa Slaa ni mzinzi ana dhambi amewezaje kwenda kuhiji na mke wa mtu!!!! kuna majibu matatu kwa hoja hii la kwanza hata maandiko yanasema sisi sote ni wadhambi na tuepungukiwa na utukufu wa mungu hivo kumnyooshea mwenzako kidole kuwa ni mdhambi jitazame kwanza wewe!! Pili Yesu alisema kuwa hakuja kutafuta wenye haki bali wadhambi,..na mwenye afya hahitaji tabibu, kwa hiyo hata kama doctor ana dhambi kama anavodai huyu askofu uchwara basi kwenda kuhiji ni sahihi kabisa maana hapo ndio mahali pa kutubu na kuanza maisha mapya!!sasa watu wasafi, wasio na dhambi wanahitaji kwenda kuhiji??Tatu swala la mke wa mtu achilia mbali madai ya askofu uchwara huyu, aliyejidai kuwa ndio mwenye mke alifungua kesi (kwa msaada wa ccm) akidai kaporwa mke mahakama ime rule out kuwa alishapewa talaka sio mke wa mtu sasa huyu askofu uchwara ana refer mke wa mtu yupi??Mwisho namshauri huyu askofu uchwara arejee maandiko yafuatayo,..usihukumu usije kuhumiwa,,, kipimo kile umpimiacho mwenzako nawe utapimiwa hicho hicho,.na mwisho askofu uchwara kumbuka kutoa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo uweze kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzako!!