Askari wa Ulinzi aokota Milioni 10. Apewa zawadi ya Laki 5

Usirudishe kwani ni hela yako? Hutakiwi hata kuumia maana ni hela ambayo haikuhusu..

Kuna dogo alikuwa na itikadi kama hizo, ooh mm nikiokota kitu sirudishi. Kesho yake tu kapanda gari simu akaisahau kwenye gari, watu wenye roho kama yake wakapita nayo. Akaja kwangu analaani vibaya eti kwanini aliyeokota hajamrudishia

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungemkumbusha tuu kuwa Cha kuokota hakirudishwi kama yeye alivyosema.
 
inategemea pia aina ya malezi aliyopitia mtu. mimi, kwa mfano, imani yangu inanitaka nirudishe nilichookota kwani nikichukua itakuwa ni sawa na kuiba tu. Kwa wengine, kitu cha kuiba kamwe hakiwezi kumpa amani ya maisha mpaka anaingia kaburini hata kama kitamwezesha kununua chochote kile duniani.
Ulitakiwa upewe uraisi baada ya Nyerere ila ni bahati mbaya tu😂
 
Askari wa kampuni ya ulinzi ya NG'e anaelinda JKCI.. Aisha twalibu..

Aliokota begi la mgonjwa aliedondosha eneo Hilo la hospitali lenye kiasi Cha pesa shilingi milioni kumi(10m)

Lakini mlinzi huyu alirudisha kiasi Hilo Cha pesa na mhusika hakumpa hata shilingi kumi.

Mkurugenzi mtendaji wa JKCL alimpatia shilingi laki Tano Kama zawadi ya uaminifu...

Je ungekuwa wewe ungerudisha hiyo pesa ili upewe zawadi ya uaminifu kwenye kazi yako ya laki tatu???? View attachment 2040303

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
Uaminifu ni kitu bora kuliko pesa hata mimi ningerudisha
 
Huyu ni mfano bora,kwamba watu waaminifu wapo,hasa pale hilo linatoka kwa mtu anayelinda watu na mali zao,kama alijua kwenye begi kuna hela na kuamua kurudisha.Mungu atambariki atafika mbali
Sema kwa mazingira ya hospitali ni jau😂 kusepa na kitita! Ingekuwa labda airport au sehemu ya bar aah unatembea na chaki tu! Naenda kusunda mzigo chimbo kisha narudi natulia zangu!

Waliobia watu mabilion mbona wapo na wanapeta tu kwenye ma V8 na wanaishi mpaka wanafia madarakani! Nyie wezi wa kuku mnateketea kwa petrol! Itakuwa hio million 10!
 
Kati ya mgonjwa na huyu askari nani alikua anahitaji hiyo million kumi? doing the right thing ni hulka ya Kiungu ambayo haihitaji malipo
Aliyedondosha ni ndugu wa mgonjwa siyo mgonjwa, huyo kaja kumwona mgonjwa ndo maana hakumpa hata mia.
 
Hapo kuna CCTV alijua fika kuwa akichukua wakija kufuatilia watajua ni yeye amechukua.
 
Hizo ni kick! Kulikuwa na ulazima gani ya kuita wandishi wa habari
 
Kuna uzi mmoja unasema "Acha kusaidia masikini acha wafe" yule mwandishi yuko sahihi.
 
Ok kanuni zipo hivi. Ukiona mtu kadondosha kiasi hicho cha pesa na wewe umekiokota jua ni mother nature imefanya yake in favour of you. Na mara nyingi mtu carelessly anaanzaje kudondosha mzigo wa 10M? Easy come easy go Jua hata namna alivyo zipata sio namna nzuri (legal ways.) Okota tia kibindoni maisha yaendelee.
Alisikika jamaa mmoja hivi
Easy come easy go. Unataka kusema hata huyu . kwa namna hiyo zisingeenda fanya kazi halali?
 
Askari wa kampuni ya ulinzi ya NG'e anaelinda JKCI.. Aisha twalibu..

Aliokota begi la mgonjwa aliedondosha eneo Hilo la hospitali lenye kiasi Cha pesa shilingi milioni kumi(10m)

Lakini mlinzi huyu alirudisha kiasi Hilo Cha pesa na mhusika hakumpa hata shilingi kumi.

Mkurugenzi mtendaji wa JKCL alimpatia shilingi laki Tano Kama zawadi ya uaminifu...

Je ungekuwa wewe ungerudisha hiyo pesa ili upewe zawadi ya uaminifu kwenye kazi yako ya laki tatu???? View attachment 2040303

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app

Kwa Hali ya sasa huwezi okota bag Kwenye premises za kijanja iwe Siri, bora nusu Shari kuliko Shari kamili
 
Easy come easy go. Unataka kusema hata huyu . kwa namna hiyo zisingeenda fanya kazi halali?
Zingefanya ila zingeisha haraka ila lengo la kwanini zimekuja kwako lingetimia. Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa labda lengo la hizo fedha kuja kwa huyo mlinzi ni

1. Apate laki tano aliyo ipata kazini kwake
2.uaminifu uongezeke kazini kwake
3. Labda siku za usoni uaminifu huo utatumika kumpandisha cheo n.k

Hakuna jambo hutokea kwa bahati mbaya ilimradi dunia inazunguka basi na mambo yake yanazunguka vile vile tena kwa mpangilio ambao upo juu ya ufahamu wetu
 
Uaminifu unalipa,huenda huo ni mtihani tu alikua kapewa na Mungu,

Unayesema ingekua wewe usingerudisha,hebu jaribu kukaa upande ambao ingekua wewe ndio umepoteza hizo hela.
 
Zingefanya ila zingeisha haraka ila lengo la kwanini zimekuja kwako lingetimia. Kwa ufafanuzi zaidi ni kuwa labda lengo la hizo fedha kuja kwa huyo mlinzi ni

1. Apate laki tano aliyo ipata kazini kwake
2.uaminifu uongezeke kazini kwake
3. Labda siku za usoni uaminifu huo utatumika kumpandisha cheo n.k

Hakuna jambo hutokea kwa bahati mbaya ilimradi dunia inazunguka basi na mambo yake yanazunguka vile vile tena kwa mpangilio ambao upo juu ya ufahamu wetu
Safi sana Mkuu,nimeipenda hii.
 
Back
Top Bottom