Askari wa Ulinzi aokota Milioni 10. Apewa zawadi ya Laki 5

Inategemea na sehemu yenyewe ipo je. Wenda hilo eneo limezungukwa na CCTV unahisi hapo utakwepa kitu? Kimbia nazo uitwe mwizi, ama hizo ela zilikuwa zinapelekwa hapo hospital kwaajiri ya kuokoa maisha ya mgonjwa/wagonjwa
 
Hii stori ipo. Miaka yote tu mara mzungu mara padre
Nikiwa mdogo mzee aliwahi kunisimulia kisa cha padre aliedondosha burungutu la pesa kwa makusudi..alipita mkurima mmoja mwenye haliduni ambae hata mavazi yake ni ya kuunga unga..akawa ameliokota begi la fedha alilolidondosha padre na kuliludisha kwa padre..unaambiwa padre alimtandika vibao jamaa na hakumpa hata senti tano..na mwisho wa siku alimuambia utakufa masikini mbwa wewe😁😁😁
 
inategemea pia aina ya malezi aliyopitia mtu. mimi, kwa mfano, imani yangu inanitaka nirudishe nilichookota kwani nikichukua itakuwa ni sawa na kuiba tu. Kwa wengine, kitu cha kuiba kamwe hakiwezi kumpa amani ya maisha mpaka anaingia kaburini hata kama kitamwezesha kununua chochote kile duniani.
 
Nikiwa mdogo mzee aliwahi kunisimulia kisa cha padre aliedondosha burungutu la pesa kwa makusudi..alipita mkurima mmoja mwenye haliduni ambae hata mavazi yake ni ya kuunga unga..akawa ameliokota begi la fedha alilolidondosha padre na kuliludisha kwa padre..unaambiwa padre alimtandika vibao jamaa na hakumpa hata senti tano..na mwisho wa siku alimuambia utakufa masikini mbwa wewe😁😁😁
Stori tu hiyo, hakuna kitu km hicho
 
Tukiwa wadogo tuliimba, cha kuokota si cha kuiba, mwenye mali ndio mjinga

Kurudisha au kutorudisha kunategemea sana mazingira.
 
Ok kanuni zipo hivi. Ukiona mtu kadondosha kiasi hicho cha pesa na wewe umekiokota jua ni mother nature imefanya yake in favour of you. Na mara nyingi mtu carelessly anaanzaje kudondosha mzigo wa 10M? Easy come easy go Jua hata namna alivyo zipata sio namna nzuri (legal ways.) Okota tia kibindoni maisha yaendelee.
Alisikika jamaa mmoja hivi
Mimi kinachonushangaza ni kitendo cha mtu kutembea na cash 10 milioni kwenye zama hizi za banking facilities kila mtaa... Mfano huyo mlinzi angekausha na hizo pesa angelaumu kweli?
 
Askari wa kampuni ya ulinzi ya NG'e anaelinda JKCI.. Aisha twalibu..

Aliokota begi la mgonjwa aliedondosha eneo Hilo la hospitali lenye kiasi Cha pesa shilingi milioni kumi(10m)

Lakini mlinzi huyu alirudisha kiasi Hilo Cha pesa na mhusika hakumpa hata shilingi kumi.

Mkurugenzi mtendaji wa JKCL alimpatia shilingi laki Tano Kama zawadi ya uaminifu...

Je ungekuwa wewe ungerudisha hiyo pesa ili upewe zawadi ya uaminifu kwenye kazi yako ya laki tatu???? View attachment 2040303

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
Huyu ni mfano bora,kwamba watu waaminifu wapo,hasa pale hilo linatoka kwa mtu anayelinda watu na mali zao,kama alijua kwenye begi kuna hela na kuamua kurudisha.Mungu atambariki atafika mbali
 
Majuzi nilikuwa kwenye hiyo hospital ya magonjwa ya moyo ya JK. Sitoshangaa ikiwa hizo fedha ni kwa ajili ya malipo ya matibabu na vipimo. Kuna kipimo cha kukagua mishipa ya damu ya moyo kuona kama iko OK au imeziba ni sh milioni mbili. Kufanya hicho kipimo na kuzibua mirija total costs ni milioni sita. Hapo bado vipimo vingine, madawa, wodini etc
 
Usirudishe kwani ni hela yako? Hutakiwi hata kuumia maana ni hela ambayo haikuhusu..

Kuna dogo alikuwa na itikadi kama hizo, ooh mm nikiokota kitu sirudishi. Kesho yake tu kapanda gari simu akaisahau kwenye gari, watu wenye roho kama yake wakapita nayo. Akaja kwangu analaani vibaya eti kwanini aliyeokota hajamrudishia

Sent using Jamii Forums mobile app
Riziki ya mtu IPO mikononi mwa MTU.
 
Mimi kinachonushangaza ni kitendo cha mtu kutembea na cash 10 milioni kwenye zama hizi za banking facilities kila mtaa... Mfano huyo mlinzi angekausha na hizo pesa angelaumu kweli?
Hata mie najiuliza hilo kuna walakini, halafu mtu anakurudishia hata mia haumpi? kuna walakini kwenye hizo pesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom