Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 440
- 3,211
Nimepita maeneo ya Ubungo nikiwa naelekea kwenye harakati zangu, naona Polisi wamejaa kanisani kwa Gwajima baada ya yeye kutangaza atashiriki ibada ya Jumapili ya leo.
Wengi wapo barabarani wanafunga utepe. Kwakuwa speed ya gari ilikuwa kubwa sijafanikiwa kuchukua picha ya haraka.
Pia sijafanikiwa kuona upande wa pili wa kanisa ili kubaini kama wapo pia au la.
===
Askari waliovalia sare za Jeshi la Polisi wameweka ulinzi mkali katika Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Nyumba ya Ufufuo na Uzima), eneo la Ubungo Dar es salaam huku njia zote zinazowezesha Watu kufika kwenye kanisa hilo zikiwa zimezuiwa.
Ikumbukwe Juni 13, 2025, Naibu Katibu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church, Askofu Maximilian Machumu “Mwanamapinduzi” amesema taarifa kuwa Msajili wa Jumuiya za Kiraia, Emmanuel Kihampa amefungia Kanisa lao, si za kweli bali lililofungiwa ni Kanisa la Glory of Christ Church ambalo halina uhusiano na Kanisa lao, hivyo Jumapili hii wanatarajia kurejea Kanisani kuendelea na Ibada.
Baadhi ya waamini wamejitokeza maeneo ya karibu na Kanisa hilo lililopo Ubungo.
Polisi wafanya doria kwenye Kanisa la Gwajima kutawanya waamini wanaokusanyika
Pichani Mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika akilia baada ya kuzuiwa kuingia kwenye Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church (Nyumba ya Ufufuo na Uzima) lililopo eneo la Ubungo.
Baadhi ya waamini wanazuiwa na kuambiwa kwamba hawaruhusiwi kukusanyika eneo la karibu na Kanisa hilo, ambapo askari Polisi wanafanya doria kuwatawanya waamini wanaokusanyika katika makundi.
Pia soma