Asiye raia wa Tanzania lakini alizaliwa Tanzania anaweza kumiliki ardhi?

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Naomba adm msiiweke kule kwenye jukwaa la sheria kwanza ila kila mtu atoe mawazo yake kwanza.

Kuna babu mmoja watoto wake wa kiume wote aliojaliwa wako Marekani zaidi ya miaka20 sasa. Walizaliwa Tanzania lakini wakahamia Marekani japo mara kwa mara wanakuja kumuona babu yao.

Kwa kuzaliwa wamezaliwa Tanzania lakini wakachukua uraia wa Marekani kutokana na sheria yetu hatuna kitu uraia pacha.

Swali linakuja je hawa watoto wake kisheria wanaruhusiwa kuja kumiliki mali za babu nyumba na viwanja na mashamba yakea aliyo nayo huku Tanzania?

Ila kila mwaka kwa kweli wanakuja kumuona baba yao na wanamtunza maana wanamtumiaga matumizi wakiwa huko nje.

Naomba msaada wa mawazo tafadhali
 
Wataalamu waje ila kwa sheria ya tz ukishaditch uraia kumiliki kitu kinaitwa ardhi wasahau.
 
Hata kama ukoo wako uko Tandahimba, ukishakuwa raia wa nchi nyingine automatically wewe siyo Mtanzania na hivyo huwezi kupata haki zako za kuzaliwa ikiwemo kumiliki ardhi.
 
Wanaweza kama watakuja kwa ajili ya uwekezaji haina shida hapo lazima wawe na mtaji wa kutosha mfano unaweza fungua kampuni na kadhalika.

Serikali inahitaji imadilisha sheria ambazo hazina tija kwa Taifa kama hii ya MTANZANIA aliye badilisha uraia na kupata uraia wa NCHI nyingine anapo rudi TANZANIA anakuwa kama mgeni mwingine anakuwa analimitation kwenye kufanya maendeleo kama vile kununua nyumba au ardhi au kufanya biashara ndogo ndogo ina mlazima au na permit hivi vitu havina tija kabisa kwani uraia wa KUZALIWA huwa haubadiliki hata siku mmoja.

Serikali inahitaji iwepe special status Kwa DIASPORA wote wawe na special IDENTIFICATION kama kitambulisho wanapo kuja TANZANIA waingie tu bila Visa na wafanye mambo ya maendeleo kama MTANZANIA mwingine tu isipo kuwa katika maswala ya Kupiga KURA au kugombea nafsi yoyote katika Serikali ndio wawe BAN kama NCHI nyingi za Africa wanavyo fanya kwa MADIASPORA wa NCHI zao kama Ghana ,Nigeria au Ethiopia, Kenya, Uganda nk.
 
Hapo ndio unaona maigizo ya viongozi wetu wanatoa matamko yanayo pingana na sheria
Nasheria zipo katika kulinda maslahi mapana ya nchi. Kama kuna haja ya kufanya amendments au ku overall sheria ifanyike ili mwisho wa siku nchi ipate ilichokusudia maana akina Ramadhani wako wengi.
 
kama nipo marekani ya nini nijisumbue kuja tanzania kumiliki ardhi hata kumiliki mbuzi sitaki nikiisha pata nafasi hiyo nikumshukuru mungu
 
Naomba adm msiiweke kule kwenye jukwaa la sheria kwanza ila kila mtu atoe mawazo yake kwanza.

Kuna babu mmoja watoto wake wa kiume wote aliojaliwa wako Marekani zaidi ya miaka20 sasa. Walizaliwa Tanzania lakini wakahamia Marekani japo mara kwa mara wanakuja kumuona babu yao.

Kwa kuzaliwa wamezaliwa Tanzania lakini wakachukua uraia wa Marekani kutokana na sheria yetu hatuna kitu uraia pacha.

Swali linakuja je hawa watoto wake kisheria wanaruhusiwa kuja kumiliki mali za babu nyumba na viwanja na mashamba yakea aliyo nayo huku Tanzania?

Ila kila mwaka kwa kweli wanakuja kumuona baba yao na wanamtunza maana wanamtumiaga matumizi wakiwa huko nje.

Naomba msaada wa mawazo tafadhali
Hawaruhusiwi. Sababu ni kuwa sio raia wa Tz. Watachukuliwa kama wawekezaji wengine kutoka nje, Ila hawatamiliki ardhi.
 
Back
Top Bottom