Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 879
- 4,109
Natambua kuna sheria ya Uraia inayoniruhusu mimi kama RAIA wa Tanzania kuukataa uraia wangu wa Tanzania na kuwa RAIA wa nchi nyingine niipendayo.
Natambua kwamba katiba ya JMT na sheria za Ardhi zinakataza RAIA wa kigeni kumiliki ardhi isipokuwa kwa masharti maalumu kama uwekezaji na atakabidhiwa umiliki kwa muda flani.
Natambua pia kwamba RAIA wa kigeni anakatazwa na sheria kununua au kujenga nyumba Tanzania isipokuwa kwa kibali maalumu.
ISUES FOR DISCUSION
1. Je,ninapoukana uraia wa Tanzania ninaruhusiwa kisheria kuendelea kumiliki ardhi niliyokuwa nayo kipindi nikiwa RAIA wa Tanzania?
2. Kama siruhusiwi kuendelea kumiliki ardhi hiyo kama Mtanzania namkabidhi nani na kwa sheria gani?
3. Kama sheria na kanuni hazijasema kinapaswa kusurender ardhi na wapi nisarende ardhi; je nikibainika ninaimiliki hiyo ardhi naweza kushtakiwa?
4. Kama natakiwa kuikabidhi ardhi husika serikalini, je hadi sasa wizara ya ardhi ina ardhi kiasi gani ya watanzania walioukataa utanzania?
5. Endapo ardhi iliyopo ni ya urithi, wanapogawa mirathi mimi kama RAIA wa kigeni aliyekuwa Mtanzania naruhusiwa kupewa ardhi kama Sehemu ya mnufaika wa mirathi? Kwa sheria gani?
6. Je, ninaweza kurithisha ardhi yangu au ya urithi kwa mtu mwingine nisipokonywe?
Hii mada ni maalumu kwa waliosoma sheria za Uhamiaji, ardhi na katiba ya Jamuhuri. ..Lipo kundi kubwa la RAIA wa Kigeni wanaomiliki ardhi baada ya kuukana utanzania .Karibuni wajuvi