AshaDii: "JF Woman Of The Year 2011"

AshaDii: "JF Woman Of The Year 2011"

Mitishamba naamini kua kila mtu is entitled to an Opinion.... Post zoote humu ndani ziko postive humu ndani, Hio haina maana kua woote wanakubali. Naamini kuna wale wana wazo kama hili lako ila they don't have the guts kama zako kupinga. Nakupongeza kwa hilo na kufurahi pia for hatimae nimepata mtu ambae anaweza akanipunguza furaha nilio nayo na kuangalia the other side of the coin... Kama hutajali NITASHUKURU SAAANA Ukiniambia hasa kwa nini unaona sifai kuitewa Woy ila tu kwa hadhi ya MMU.... Natanguliza shukrani.... Pamoja Saana.
AshaDii, asiye kufahamu hakuthamini, mimi licha ya kwamba sikubaliani na kamwe sintokubaliana namna nomination ya JF The Man of the year 2011 alivyopatikana, lakini kuhusu wewe AshaDii kwenye nafasi hii unastahili na nakuzidisha hon gera zangu, na offer yangu bado iko palepale.
N:B. Siko hapa kimapenzi maana sitafuti mapenzi kwenye mtandao, na nikikuita dada maana yake ninaamaisha vivyo na kwamba nimekuheshimu kwa sababu unajiheshimu.
 
Hongera sana AshaDii,

Naamini comments zako hapa JF zinatufahamisha ulivyo mtu wa watu, kama unaweza kujitengenezea ufuasi kwa watu wasiokufahamu, just friends katika mtandao, sina shaka katika real life ndivyo ulivyo.Naamini walikuwepo wanawake wengine ambao walikuwa na michango mikubwa sana hapa JF katika kuliweka hai na moto jukwaa letu la JF lakini wewe umeweza kufikia tuzo hiyo kwa sababu ya Heshima!!(unawaheshimu sana wanaJF wenzako), huna matusi wala kejeli.

Mungu aendelee kukubariki na kukujalia hekima zaidi, ili uendelee kutoa somo kwa wanawake wengine wote hapa JF. Heshima yako kwa wanaJF wenzako imekuwa ni kubwa sana siku zote.

Heshima, heshima, heshima!!

Mwita Maranya what a post on a perfect day kwangu of sikukuu ya Wanawake.... Wanifanya niwe more proud to be a WOMAN..... THANK U and I am HUMBLED.

Kuhusu heshima naona niseme labda sababu pia nimebahatika kuheshimika na hao Members wenzangu, Na kama unavoelewa kila mwanadamu apenda aheshimiwe na pale ambap watoa/wapewa heshima ki hali halisi ina maana inabidi ureciprocate.... and that is what I do kaka. I respect as they respect me too and I am THANKFUL to all Members.... Wale ambao na interract nao mara kwa mara na wale ambao si interrect nao..... To me JF imekua kama Jamii fulani, hua naona kama nina two lives....lol

Nashukuru na kupokea dua yako, Na namuomba Mwenyezi Mungu atubariki soote na kutujaalia soote Kheri, baraka na kupata yale ambayo twatarajia ama zaidi ya hapo.

Pamoja saana Maranya.... Pamoja Saana dear...
 
Mitishamba naamini kua kila mtu is entitled to an Opinion.... Post zoote humu ndani ziko postive humu ndani, Hio haina maana kua woote wanakubali. Naamini kuna wale wana wazo kama hili lako ila they don't have the guts kama zako kupinga. Nakupongeza kwa hilo na kufurahi pia for hatimae nimepata mtu ambae anaweza akanipunguza furaha nilio nayo na kuangalia the other side of the coin... Kama hutajali NITASHUKURU SAAANA Ukiniambia hasa kwa nini unaona sifai kuitewa Woy ila tu kwa hadhi ya MMU.... Natanguliza shukrani.... Pamoja Saana.
Mimi si mnafiki kama wengine humu.
Kwa mfano umeshatoa mchango gani kwenye jukwaa la siasa? Kumbuka lile ndo jukwaa ambalo linaheshimika mno. Na hapa sizungumzii michango ya aina ya "naunga mkono hoja". Lakini kitu kingine, kuweka hili shindano huku mmu ni kuwavutia watu wa mmu ndo wawe wapiga kura zaidi wakati shindano linahusu jf yote. Kumbuka kuna watu wanatembelea majukwaa mengine na huwa hawapiti kabisa/wanapita mara chache sana huku mmu. Sasa iweje shindano linahusu jf yote halaf libandikwe mmu? Bila shaka ni mpango madhubuti kuhakikisha kuwa mtu wa huku anashinda.

Hivi mtu kama asipirini ana mchango gani kwenye majukwaa mengine?
Hata akiwa jukwaa la siasa bado anaweka posti za ki-mmu tu, halafu leo ndo useme jf man of the year?
Upuuzi mtupu wa kubebana na kupeana sifa zisizostahili kwa madhumuni ya kuopoa humu.

Nasisitiza, wewe na mwenzio hamkustahili kushinda tuzo hii kwa title iliyopo unless kama title inachange.

Hizo ndo pongezi zangu kwenu!
 
Miti Shamba utachekesha hata walionuna kama utampinga huyu AshaDii kwenye hili licha ya kwamba sikubaliani na hili shindano kwa jinsi lilivyokuwa na dosari za wazi, AshaDii ndio realy Woman of JF, take my word. na jukwaa la siasa unalodhani wewe kwamba ndio makini huyu mdada huwa anachangia sana, Jukwaa la siasa watu wengi wnalikimbia kwa sababu limejaa wajinga wajinga wengi.
 
I knew it.............matokeo yamenifurahisha unastahili huu u role model!

Pongezi zangu na familia yangu!
 
Siku ya wanawake duniani: Tanzania tumepiga hatua?

Privatus Karugendo

NIANZE makala hii kwa maoni ya mhariri wa gazeti moja la Ujerumani, gazeti la Stuttgarter Nachrichten, ambaye anawataka akina baba wathamini mchango unaotolewa na wanawake katika maendeleo ya jamii. Mhariri wa gazeti hilo anakumbusha kwamba wanawake ndiyo wazazi, ndiyo akina mama wa nyumbani na pia ni wafanyakazi. Mambo hayo matatu yanashikamana, anasema mhariri wa Stuttgarter Nachrichten. Kwa hiyo kila siku ingelikuwa siku ya wanawake duniani, laiti pangekuwa na mtazamo sahihi wa -kijamii”

Maneno yaliyonivutia kwenye nukuu hii ni; “Kwa hiyo kila siku ingelikuwa siku ya wanawake duniani…” na yale yasemayo kwamba; “Mhariri wa gazeti hilo anakumbusha kwamba wanawake ndiyo wazazi, ndiyo akina mama wa nyumbani na pia ni wafanyakazi.”

Tunapojiandaa kusherehekea siku ya wanawake duniani ni muhimu kuwa na maneno hayo hapo juu kichwani mwetu. Tuache utamaduni wa kusherehekea kwa vile ni ratiba au kwa vile wengine wanafanya hivyo. Ni muhimu kusherehekea tukitafakari chanzo cha sherehe zenyewe, chanzo cha mapambano haya ambayo lengo lake kubwa ni kutetea haki za wanawake.

Ni ukweli ulio mbele yetu kwamba kwa hapa Tanzania, kila siku ingekuwa ni siku ya wanawake duniani. Tunaishi na kushuhudia kila siku kwamba hapa Tanzania, wanawake ndiyo wazazi, ndiyo akina mama wa majumbani na pia ni wafanyakazi.

Wanawake wanalima, wanapika, wanachota maji, wanajifungua na kuwalea watoto. Wanawake wanatunza familia kwa kila hali. Kule vijijini wanawake hawana hata nafasi ya kuyafurahia maisha, kazi yao kubwa ni kuhakikisha familia inafurahi na kuishi kwa amani. Wasichana wanafanyiwa vitendo vibaya vya ukeketaji, kunyimwa nafasi ya kuendelea na masomo na kulazimishwa kuolewa mapema.

Wengine wakipona kuozwa mapema na wakati mwingine hawapati bahati ya kuolewa, wanakimbilia mijini na kuanza kujiuza. Wanaishi maisha ya taabu na shida, wanapata fedha kwa mateso makubwa na kuhakikisha fedha hizo zinarudi nyumbani kwenye familia zao ili kuwalea watoto wao na kuwatunza wazazi wao.

Wanawake wamekuwa wakisimama kidete kulinda na kutetea dhana ya mshikamano wa dhati; uwazi unaojengeka katika utamaduni wa kusikiliza kwa makini na kwamba, wamekuwa wakitoa mchango mkubwa wa hali na mali katika maendeleo ya sekta ya elimu, afya na kilimo cha chakula kwa ajili ya familia na jamii zao. Ni watu wanaojitoa bila ya kujibakiza kwa ajili ya malezi na makuzi ya watoto ndani ya familia. Wanawake wameendesha mapambano bila kutumia silaha na wameshiriki kikamilifu kupata amani ya kweli, hata katika hali yao ya ukimya.

Ugomvi wa kupigania madaraka barani Afrika, ambao umeleta vita na kuzalisha wakimbizi haujawa sehemu ya wanawake hata mara moja. Ugomvi huu unaongozwa na wanaume. Ingawa Tanzania haijakumbukwa na ugomvi wa madaraka kiasi cha kuingia vitani, vitendo vya ufisadi na rushwa kubwa ambavyo vimelitesa taifa letu kiasi kikubwa vimekuwa vikiongozwa na wanaume.

Siku ya wanawake duniani ilianza kuadhimishwa mwaka 1911 wakati makundi ya wanawake nchini Marekani yalipokusanyika na kupinga udhalilishaji, ukandamizaji, uonevu na ubaguzi wa kijinsia hususan sehemu za kazi. Kuanzia wakati huo mataifa mbalimbali yalianza kuadhimisha siku hiyo kwa lengo la kupinga mfumo dume ambao uliwabagua wanawake kwa kuwanyima fursa za kusoma, kupata vyeo, mishahara mikubwa na haki ya kushiriki katika shughuli za maendeleo kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Siku ya wanawake duniani huadhimishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Machi 8, kila mwaka. Madhumuni ya maadhimisho haya ni kupima utekelezaji wa maazimio, matamko na mikataba mbalimbali ya kimataifa inayohusu masuala ya wanawake.
Madhumuni hayo mahususi ni pamoja na, kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuweka msisitizo na kuhamasisha jamii kuhusu kauli mbiu ya kimataifa wakati wa maadhimisho ya kila mwaka, kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali, asasi mbalimbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuwaendeleza wanawake, kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera, mipango na ahadi mbalimbali za kudumisha “Amani, Usawa na Maendeleo”.

Vilevile, maadhimisho haya hutoa fursa maalumu kwa taifa, mikoa, wilaya, mashirika ya dini, vyama vya siasa, mashirika ya hiari, jamii na wanawake, kupima mafanikio yaliyofikiwa kimaendeleo na kubainisha changamoto zilizojitokeza katika kufikia azma ya ukombozi na maendeleo ya wanawake na hivyo kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.

Hapa nchini maadhimisho haya yalifanyika kitaifa kuanzia mwaka 1997 hadi mwaka 2005 na baada ya hapo Serikali ilipitisha uamuzi kuwa yafanyike kila baada ya miaka mitano. Uamuzi huu ulipitishwa ili kutoa muda wa kutosha wa utekelezaji wa maazimio mbalimbali na kuweza kupima mafanikio ya utekelezaji wa shughuli hizo za kila baada ya miaka mitano.

Pamoja na umri mkubwa tangu kuanza kwa maadhimisho haya, bado tunachoshuhudia katika jamii zetu ni manyanyaso mbalimbali wanayofanyiwa akina mama duniani. Hali za kuwatumia kinamama katika mazingira ya kivita inasikitisha na kudai tena kutupiwa jicho. Takwimu zinaonesha wazi kuwa bado kuna idadi kubwa sana ya kinamama, na hasa walio katika umri wa ujana wanaendelea kunyimwa haki zao katika mazingira mbalimbali yanayotawaliwa na vita na vurugu.
Kwa muda mrefu sasa wanawake wamekuwa ni tabaka linalodai haki dhidi ya mfumo dume, haki ya usawa kijinsia katika elimu, kazi za kiuchumi na kijamii. Haishangazi kuona kuwa wanawake wamekuwa na vyombo vingi vinavyowatetea, zikiwemo asasi za kiraia na za kiserikali na mashirika ya sheria.

Tangu shuleni wanawake wanapewa upendeleo, ukifika bungeni kuna viti maalumu vya wanawake, hiyo yote ni njia ya kuwawezesha wanawake. Lakini kwa nini wanawake wanatetewa kiasi hicho? Je, ni kweli wanawake hawawezi? Mimi nadhani sasa ifike mahali wanawake wajitokeze wapaze sauti yao wenyewe badala ya kusubiri kuwezeshwa.

Nasema hivi kwa sababu wanawake ni binadamu yule yule kwa hiyo, hana tofauti na mwanaume kiutendaji ukiacha tofauti ya jinsia tu. Mwanamke anaweza kufanya kazi zote zinazofanywa na wanaume bila kupendelewa, sasa kwa nini asubiri kuwezeshwa?

Tumeona wanawake wakiendesha hata magari ya mizigo, ndege, meli na treni. Siku hizi tunaona wanawake wakicheza hata mpira wa miguu. Hii inaonyesha kuwa wanawake wanaweza kila kazi. Kuendeleza upendeleo ni hali ya kuonyesha kwamba hawawezi na hii inawaathiri kisaikolojia.

Makala iliyopita niliandika juu ya wimbo wa Vick Kamata, unaosema kwamba wanawake wameolewa na CCM. Haya ni matokeo ya kuendeleza upendeleo kwao kiasi wanajiona duni mbele ya mfumo dume na kuutukuza kila wanapopata nafasi. Mfumo mzima unawanyima wanawake uwanja wa kujiamini na kujichukulia kama binadamu yeyote yule.

Kwa upande mwingine, hapa Tanzania, ukombozi wa mwanamke unakwamishwa na wanawake wenyewe. Kuna haja ya wanawake Tanzania kujifunza kutoka mataifa mengine. Sherehe kama hii ya siku mwanamke duniani iwe ni fursa ya kujifunza kutoka kwingine.

Tanzania ni lazima tupige hatua katika jitihada za kumkomboa mwanamke. Kuna kazi kubwa ya kuvunjilia mbali mfumo dume ambao kwa kiasi kikubwa umejengeka kiasi hata wanawake wanafikiri na kutenda “kimfumo dume”.
Akigombea mwanamke, wanawake wenzake wanakuwa mstari wa mbele kusema kwamba hawezi na wakati ukifika wa kupiga kura wanamnyima kura zao. Ipo mifano mingi ya wanawake kushindwa kuwaunga mkono wanawake wenzao na kuwapigia kura wanaume. Hali hii ni hatari.
Wanawake ni wajenzi wa amani, taswira ambayo imejionesha kwa namna ya pekee katika siku za hivi karibuni, katika medani za kitaifa na kimataifa, kwa wanawake watatu kutoka Bara la Afrika kupewa tuzo ya amani kwa mwaka 2011.

Wanawake katika nchi mbalimbali za Afrika wamekuwa mstari wa mbele kulinda na kudumisha misingi ya amani na utulivu, lakini mchango wao haukupewa uzito unaostahili kutoka katika jumuiya ya kimataifa.

Leymah Gbowee ni mwanamke ambaye alipambana kufa au kupona, ili kuhakikisha kwamba, vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyokuwa inavuma nchini Liberia kuanzia mwaka 2003, inafikia ukomo. Mama huyu anakumbukwa na jumuiya ya kimataifa kama mpigania amani.
Fatou Bensouda si mgeni sana katika masuala ya haki na amani kwenye mahakama ya kimataifa kwa ajili ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, iliyokuwa na makao makuu yake jijini Arusha, Tanzania. Bibi Jacqueline Moudeina alikuwa ni wakili wa kesi za dhuluma dhidi ya wanasiasa waliokumbana na ukatili wa utawala wa Rais Hussein Habre wa Chad. Ni mwanamke aliyehatarisha usalama na maisha yake.
Jumuiya ya kimataifa imetambua na inaendelea kuthamini mchango makini uliotolewa na wanawake wawili kutoka Liberia: Hawa ni Rais Ellen Johnson Sirleaf na Bibi Leymah Gbowee, pamoja na Tawwakkol Karman, mwanamke kutoka Yemen.

Hawa ndio waliojinyakulia tuzo ya amani kwa mwaka 2011 na kwamba, kuanzia sasa dhamana na mchango wa wanawake kutoka sehemu mbalimbali za dunia utaendelea kuheshimiwa na kuthaminiwa. Wanawake hawapaswi kuwa ni waathirika wa vita na manyanyaso ya kijamii, bali wadau wakuu katika mchakato mzima unaopania kulinda na kudumisha misingi ya haki na amani duniani.

Itakumbukwa kwamba, mwanamke wa kwanza kupata tuzo ya amani kimataifa ni Hayati Professa Wangari Mathaii kutoka Kenya. Aliendesha kampeni ya kijani kibichi nchini Kenya; jambo ambalo lilizua msigano mkubwa na viongozi wa kisiasa nchini Kenya, kiasi hata cha yeye ‘kuonja’ taabu na suluba za gereza.
Lakini, akasimama kidete kulinda na kutetea haki za msingi za binadamu na matunda ya juhudi hizi yanaendelea kuonekana si tu nchini Kenya, bali kwa wapenda amani na watunza mazingira kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Wanawake wa TANU, wakiongozwa na Bibi Titi Mohamed ni miongoni mwa wanawake waliochangia kiasi kikubwa Uhuru wa taifa letu. Baada ya uhuru, wanawake hawa walitupwa pembeni. Hawakupata vyeo, hawakuandikwa kwenye kumbukumbu ya historia ya Tanzania. Lakini wanawake hawa, pamoja na uwezo mkubwa waliokuwa nao, hawakuingia msituni kudai haki zao.

Walikaa kimya, waliendelea kulima na kufanya kazi ili kuwalea na kuwalinda watoto wa Tanzania. Wanawake wa TANU ni mfano mzuri wa maneno niliyoanza nayo: “Kila siku ingekuwa siku ya wanawake duniani….” Maana hawa …. “ ndiyo wazazi, ndiyo akina mama wa majumbani na pia ni wafanyakazi”.

SOURCE: Raia Mwema

JE, TANZANIA TUMEPIGA HATUA?
 
Ila bado sijaelewa kitu kimoja na naomba mtu asinichukulie katika negative manner, hivi ni kwa nini post hii ina hongera zaidi ya 110 wakati kura halisi zilizopigwa hazifiki hata nusu ya post hizi?
Sihitaji upambe kwenye swali hili tafadhali.

Your name has the rite kuuliza kama ulivo uliza kwenye post hii... Ungesema waitwa JB WISE Ingekua kwamba you know everything, JB WISER means you are becoming wiser by the minute and the day... Huna haja ya kuomba msamaha.... WHY you want to know??

  1. Baadhi ya sababu zinaingiliana na zile nilikupa kwa Ndetichia.... Kua mtu anakata tamaa ama kua encouraged. Kama mtu wake kabaki saana nyumba ahisi kura yake wont make a difference. Kama mtu wake yupo mbele anaona kua no need kisha shinda.... Mtazamo ambao ni both so wrong.
  2. Wengine humu wapo kuchakachua na kujibishana posts (sio kwa nia mbaya tumezoea hilo MMU)
  3. Post nyingine ni kama hii.... JB Usha nipongeza na wataka kunipa zawadi. Hadi mimi tufikie makubaliana waweza kuta there are 10 posts between us...
  4. Sio kila anae pongeza alibahatika kupata nafasi ya kupiga kura....

Hayo ni baadhi ila naamini yanatosha kwa sasa kupata jibu why posts nyingi kuliko idadi ya wapiga kura.
 
AshaDii, asiye kufahamu hakuthamini, mimi licha ya kwamba sikubaliani na kamwe sintokubaliana namna nomination ya JF The Man of the year 2011 alivyopatikana, lakini kuhusu wewe AshaDii kwenye nafasi hii unastahili na nakuzidisha hon gera zangu, na offer yangu bado iko palepale.
N:B. Siko hapa kimapenzi maana sitafuti mapenzi kwenye mtandao, na nikikuita dada maana yake ninaamaisha vivyo na kwamba nimekuheshimu kwa sababu unajiheshimu.

Natumia Airtel JB..... Asante saana kwa kweli I am humbled.... Ubarikiwe. Pamoja Saana.
 
jeeeeibiiii waizaaa unaoooo hiloo babuu....!limekukaabaaaaaaa!hoooryaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!......wanasema "mwenye chake mpe babuuuuu"....

subiri mwakani utagombea na mimi
 
Miti Shamba utachekesha hata walionuna kama utampinga huyu AshaDii kwenye hili licha ya kwamba sikubaliani na hili shindano kwa jinsi lilivyokuwa na dosari za wazi, AshaDii ndio realy Woman of JF, take my word. na jukwaa la siasa unalodhani wewe kwamba ndio makini huyu mdada huwa anachangia sana, Jukwaa la siasa watu wengi wnalikimbia kwa sababu limejaa wajinga wajinga wengi.
Hivi nyinyi huku mmu kushinda kutaniana siku nzima ndo mnasema hili jukwaa lina watu makini...you must be kidding.
Nakubali jukwaa la siasa laweza kuwa na baadhi ya watu ambao si GT, lakini huku ni zaidi.
Hebu angalia kwa siku huku mmu kuna post ngapi za kipuuzi, kama sio maskhara kutwa kucha.

Nadhani mnashindwa kutofautisha kati ya kushinda mmu na kutoa mawazo chanya hata kama unakuja jf mara moja kwa mwaka!

Nasisitiza huyu na mwenziye hawakustahili hiyo tuzo kwa title iliyopo.
 
jeeeeibiiii waizaaa unaoooo hiloo babuu....!limekukaabaaaaaaa!hoooryaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!......wanasema "mwenye chake mpe babuuuuu"....

subiri mwakani utagombea na mimi
Hahaaha homu boyi mwakani tugombee
 
jeeeeibiiii waizaaa unaoooo hiloo babuu....!limekukaabaaaaaaa!hoooryaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!......wanasema "mwenye chake mpe babuuuuu"....

subiri mwakani utagombea na mimi
Uko kwenye bendi ipi ya taarabu!!?? uko Jahazi au TOT?
 
Hivi nyinyi huku mmu kushinda kutaniana siku nzima ndo mnasema hili jukwaa lina watu makini...you must be kidding.
Nakubali jukwaa la siasa laweza kuwa na baadhi ya watu ambao si GT, lakini huku ni zaidi.
Hebu angalia kwa siku huku mmu kuna post ngapi za kipuuzi, kama sio maskhara kutwa kucha.

Nasisitiza huyu na mwenziye hawakustahili hiyo tuzo kwa title iliyopo.
Hahaha jomba ndo demokrasia
Hii
 
Hivi nyinyi huku mmu kushinda kutaniana siku nzima ndo mnasema hili jukwaa lina watu makini...you must be kidding.
Nakubali jukwaa la siasa laweza kuwa na baadhi ya watu ambao si GT, lakini huku ni zaidi.
Hebu angalia kwa siku huku mmu kuna post ngapi za kipuuzi, kama sio maskhara kutwa kucha.

Nadhani mnashindwa kutofautisha kati ya kushinda mmu na kutoa mawazo chanya hata kama unakuja jf mara moja kwa mwaka!

Nasisitiza huyu na mwenziye hawakustahili hiyo tuzo kwa title iliyopo.

Hivi unafahamu katika wale wajinga wa MMU ni pamoja na wewe!! maana ni zaidi ya saa nzima sasa upo hapa MMU kujibishana na wajinga wenzako!
 
hahahahahahhhaaaa kimeeyyyyy....!

halooooooooooo ooohhhhh!...wanasema wenyewe "mwanamke hasingiziwi mimba babu weeeee...."

mwakani mimi kimey na huyu jamaa sijui wiser..
 
ADii
Hongera kwa kuwakilisha vema. Unastahili tuzo kwa michango yako iliyokamilika kila idara.Ningekuwa na mamlaka basi ningekutunukia taji kila jukwaa unalochangia. Nakutakia IWD njema.
 
Back
Top Bottom