Kwani angewaacha waende zao huko South Africa angepungukiwa nini?
sheria zinawabana.

ila kuna mmoja raia wa Ethiopia anasema wanandugu zao Europe&U.S,ndugu zao kuwafanyia mpango wa kwenda huko ulaya kwa kutokea south Africa ni rahisi sana kuliko kuwafanyia mpango wakiwa Ethiopia au Erytria ni ngumu zaidi ya ngumu.
 
Kweli mkuu ajali kazini
Hao vijana nawaona sana tena unaona kabisa ni fresh wanavyozubaa zubaa
Wakifanikiwa wao mwisho wa safari ni Ulaya

Ila wakishikwa wanarudishwa halafu wanaanza upya tena
Ni majaaliwa kufika ila wapo wanaofika huku na kuwasaidia wenzao waje pia
Jamaa sio kachomwa ila kabeba wengi sana lakini pia kwa waswahili linawezekana
Pesa hzo huwa wanazitoa wapi maana Ni pesa ndefu Sana wanatumiaaa kufika S A
 
Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea na AyoTV Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji” ——— kaimu RPC Manyara. #MillardAyoUPDATES

View attachment 2943836
Mchawi wa taifa letu ni CCM wala hakunaga mwingine.
 
Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji”


Chanzo: Ayo TV
Gari halijapakwa rangi ya kijani, yeye hajavaa magwanda ya kijani, wahamiaji hawajavaa nguo za kijani, ana akili fupi.
Hata hivyo aliyempa hiyo gari iliyonunuliwa kwa pesa za DPW ndiye atakayelimaliza jambo letu.
 
Wauza Unga wengi wameacha hiyo biashara maana kifungo ni kirefu sana
Ila kuvusha wakimbizi ni
a slap on the wrist
Na inalipa kweli
Kuna wanaolipa safari moja mpaka $30,000
Duh! Hapo ni ku-cross Tz tu! Je, Kenya? Zambia? Zimbabwe? Botswan? Hadi kuingia SA how much do they pay? Kama wana ukwasi hivyo why wawe wahamiaji haramu? Kwanini wasifuate taratibu badala ya kuji-risk hivyo? Sielewi!
 
Nimesoma nikacheka, kinachonichekesha ni kwa namna mwandishi wa Ayo alivyowakwepesha CCM kwenye hii taarifa. Mara nyingi sana tumesema hii hulka ya CCM kuficha na kushabikia haya mambo na wamekua wakikataa. Waliwahi kumkataa hata yule shujaa aliyeuwawa na Polisi kuwa hakua Mjumbe wa CCM, yule waliyempachika jina la gaidi.

leo hii kakamatwa Mwana CCM akiwa tena na gari ya 2023 akiwa amebeba vipusa (wahamiaji haramu) kama kawaida, taarifa imekua twisted. CCM hebu jirekebisheni.

watu kama hawa ndio kutwa kuchwa wanasifia "Mama anaupiga mwingi" ili kuficha maovu yao...... hili lingetokea kwa CHADEMA lingeripotiwaje?

1711338476858.jpeg
 
Back
Top Bottom