Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 26,060
- 23,943
Baada ya Dereva Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma kukamatwa akiwa amebeba Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia katika gari aina ya Land Cruiser V8 likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM katika eneo la Minjingu mkononi Manyara, Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Mkoani Manyara Philon Kyetema leo amesema gari hilo, bendera pamoja na Dereva havina uhusiano wowote na Chama cha Mapinduzi.
“Gari lilikuwa na mlingoti na baada ya kufunuliwa ikakutwa bendera inayofanana na bendera ya Chama cha Mapinduzi maana yake ni kwamba huyu bwana Edward alijiandaa kuhadaa Vyombo vya ulinzi na usalama ili visimtie nguvuni lakini tunashukuru Askari Polisi wa Minjingu waliweza kumtilia shaka na kuzuia gari na ndani kukuta Wahamiaji hao 20, kesho tutawafikisha Mahakamani”
“Naomba kufafanua kwa Watanzania ninaomba wasihusishe gari hilo na bendera inayoonekana kwenye gari hilo haina uhusiano na Chama Tawala cha CCM, hilo gari lenyewe, bendera yenyewe pamoja na Dereva hawana uhusiano na Chama cha Mapinduzi”
Source: Millard Ayo
Taarifa ya Awali: Asafirisha wahamiaji 20 kwa V8 yenye bendera ya CCM