Arusha: Sabaya na wenzake wafikishwa Mahakamani. Kesi yaahirishwa baada ya mashahidi kukosekana Mahakamani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,354
Ole Sabaya mtu mwenye tuhuma zisizo na idadi , leo tena amefikishwa mahakamani huko Arusha akiwa amevaa Suti iliyopauka ili kusikiza kesi zinazomkabili.

Kesi za aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya (34) na walinzi wake watano, ambao wanakabiliwa na mashtaka sita na mawili ya ujambazi wa kutumia silaha zitaanza kusikilizwa leo.

Mashitaka mawili ambayo leo yanatarajiwa kuanza kusikilizwa ni ya ujambazi wa kutumia silaha ambayo mawakili wa Serikali, Tumaini Kwema, Abdallah Chagula na Tarsila Garvas walieleza kuwa upelelezi wake umekamilika.

Mashitaka hayo yatafikishwa leo mbele ya mahakimu wawili tofauti; Hakimu Mfawidhi, Martha Mahumbuga na Hakimu Mkazi Mkuu, Salome Mshasha.

-----UPDATE-----

Mahakama ha Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kesi inayomkabiri aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya mara baada ya mashahidi wa kesi ya unyanganyi wa kutumia silaha kutofika Mahakamani.

Mawakili wa Serikali waliiambia Mahakama kuwa Shahidi amepata udhuru na kuahidi kuwa atakuwepo siku nyingine itakayopangwa kesi hiyo.

Kesi imeahilishwa mpaka Tarehe Julai 16, 2021.

--
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha kesi ya Unyang'anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai , Mkoani Kilimanjaro,Lengai Ole Sabaya na wasaidizi wake wawili.

Kesi hiyo ya jinai namba 66/2021 ilikuja mahakamani hapo leo kwa ajili ya kusikilizwa,lakini ilishindwa kuendelea kutokana na shahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kufika mahakamani.

Mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo ,Salome Mshasha wakili wa Serikali, Tarcilla Gervas aliiomba mahakama hiyo kuahirisha shauri hilo kutokana na shahidi wao kutofika mahakamani,ambapo hakimu Mshasha aliahirisha shauri hilo hadi Julai 16 mwaka huu itakapokuja kwaajili ya kusikilizwa huku akisisitiza upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha mashahidi wao.

Awali wakili wa utetezi,Mosses Mahuna na Dancan Oolah wakiwakilisha washtakiwa wote watatu wamelalamikia upande wa mashtaka kupoteza muda wakati walishaiambia mahakama hiyo kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba Jambo hilo lisijirudie.

Washtakiwa wengine katika shauri hilo ni wasaidizi wa Sabaya,Silvester Nyegu (26) na Daniel Mbura(38) ambapo kwa pamoja wanaokabiliwa na kosa la Unyang'anyi wa kutumia silaha katika duka la mfanyabiashara Saad Mohamed baada ya kumpiga na kumtishia kwa silaha diwani wa kata ya Sombetini Bakari Msangi na Kumpora kiasi Cha shilingi 390,000.

Wakati huo huo kesi namba 27/2021ya uhujumu Uchumi, Utakatishaji fedha haramu,na Rushwa,inayomkabili Sabaya na wenzake saba imeahirishwa kutokana na upelelezi kutokamilika.

Wakili wa Serikali Tarcilla Gervas Mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Salome Mshasha alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kesi hiyo kuahirisha Hadi Julai 16 mwaka huu itakapokuja kwa ajili ya kutajwa

Akiongea nje ya mahakama wakili wa Serikali Tarcilla Gervas,alisema kuwa shauri hilo awali lilikuwa na washtakiwa Sita ila June 21mwaka huu,upande wa mashtaka umeongeza washtakiwa wengine wawili na kufikia nane.

Aliwataja washtakiwa hao ni Jackson Macha (24) na Nathan Msuya (31) wote wakati wa Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wengine ni Enock Togolani Mnkeni {41} Watson Stanley Mwahomange {27} John Odemba Aweyo na Syliverster Nyengu{26} .
 
Huyu atashinda kesi tena kwa ujinga wa maccm

Kama aliweza kushinda ile ya kitambulisho fake cha TISS.

Hakika ccm ni ile ile angalia alivyoanza kubadilisha suti

Ukute hata atokei maabusu huyu mwizi
Usichokijua sawa na usiku wa Giza,hivi watu humu jamiiforums mnajifanya kujua kila kitu kwann?

Ukiwa mahabusu unavaa nguo yoyote ile muelewe hilo acheni kujitia kujua kila kitu

Mfungwa ndio anavaa nguo maalum.

Huyo jambazi yupo mahabusu Wala hatokei popote, anatokea gerezani
 
Huyu atashinda kesi tena kwa ujinga wa maccm

Kama aliweza kushinda ile ya kitambulisho fake cha TISS.

Hakika ccm ni ile ile angalia alivyoanza kubadilisha suti

Ukute hata atokei maabusu huyu mwizi
Haki ya Mungu akishinda hii kesi raia watamalizana nae uraiani, ameumiza watu wengi sana
 
Back
Top Bottom