Arusha: Mahakama yapanga Hukumu kesi ya Ole Sabaya, wenzake Mei 31, 2022

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga Mei 31, 2022 kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.

Katika kesi hiyo washitakiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Tarehe hiyo imetajwa leo Alhamisi Machi 31, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda anayesikiliza kesi hiyo.

Amesema kwa kuwa watuhumiwa hao wapo mahabusu kesi hiyo itatajwa Aprili 13, 2022 kabla ya kutolewa hukumu Mei 31.

"Mshitakiwa wa tatu ambaye hajasaini nampa siku moja kufanya hivyo, kesho awe amesaini na iletwe mahakamani. Kesi itatajwa Aprili 13, kwa sababu washitakiwa ni mahabusu na hukumu itatolewa Mei 31, 2022" amesema.

Hata hivyo Askari Magereza, Inspekta Ramadhan Misanga ameieleza mahakama kuwa Watson Mwahomange ambaye ni mshtakiwa wa tatu aliyekuwa akijitetea mwenyewe baada ya aliyekuwa wakili wake kujitoa, hajaweza kufika mahakamani hapo kwa sababu ni mgonjwa.

Aidha Hakimu Kisinda amemuongezea muda wa siku moja Mwahomange kuwasilisha hoja zake za majumuisho zikiwa zimesainiwa mahakamani hapo.

Source: Mwananchi
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imepanga Mei 31, 2022 kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita.
Serkali badala ihangaike na mfumuko wa bei ipo busy na watumishi wake

USSR
 
Ni funzo zuri sana kwa wajinga, malimbukeni na washamba wa madaraka wasioelewa maana ya uongozi. Bado Makonda (kunyim wtu kuishi), Kalemani (kushirikiana na wahalifu kwa kuondoa CCTV ili kuficha uhalifu), Dotto James (matumizi ya fedha za umma bila kufuata utaratibu), Siro, Mambosasa, Kingai, Mahita (ubambikiaji watu kesi).
 
Huyu chawa wa magu anaongezewa mvua ingine, still bado anazo kesi zingine
 
Ni funzo zuri sana kwa wajinga, malimbukeni na washamba wa madaraka wasioelewa maana ya uongozi. Bado Makonda (kunyim wtu kuishi), Kalemani (kushirikiana na wahalifu kwa kuondoa CCTV ili kuficha uhalifu), Dotto James (matumizi ya fedha za umma bila kufuata utaratibu), Siro, Mambosasa, Kingai, Mahita (ubambikiaji watu kesi).
Serikali Katu haitomstaki makonda kuhofia kubaki uchi.akiwa ni master minder wa wasiojulikana baada ya mfumo kumtupa na utekaji ukakoma.
 
Habari wakuu
Hatimaye ile kesi inayomkabiri aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Hai Ole sabaya ya uhujumu uchumu inakaribia kufika mwisho
Hukumu yake kutolewa 31 may mwaka huu

ikitokea tena Sabaya akahukumiwa miaka 30 jela, je hivi vifungo viwili atavitumikiaje kisheria?
30+30= 60 au ni vifungo vyote kwa pamoja?
 
Anatumikia hukumu zote kwa wakati mmoja.
 
Kesi ya sabaya ndio mafanikio ya awamu ya sita.

Mengine ni kuachiwa kwa wauza madawa maarufu.
 
a

napenda au sheria ndio ilivyo
Hizo ni kesi mbili zilizofunguliwa tofauti na kwenye Mahakama tofauti hivyo basi hata kifungo kitakuwa tofauti atapiga 30 yake ya mwanzo na hii atapiga 30 Sasa kwa sababu hukumu zimetoka wakati ukikaribiana anaweza kutoka baada ya kutumikia hukumu moja na muda ukabaki mchache wa kifungo kingine na wakaamua kumtoa tu.

Kimsingi hizi ni hukumu mbili tofauti sema sababu atazitumikia separately lakini kwa muda huohuo ukikaribiana.
 
Back
Top Bottom