Arusha imekuzwa kuliko ilivyo!! ( Overrated )

Arusha imekuzwa kuliko ilivyo!! ( Overrated )

WATU WENGI WANAOSEMA UKWELI WA ARUSHA, KWA UPANDE WA INFRASTRUCTURENA GENERAL CIVILIZATION WANASHAMBULIWA SANA KWA LUGHA CHAFU SIZIZO NA UKWELI WALA UTAFITI. UKWELI NI KWAMBA ARUSHA NI MAHALI PA KAWAIDA SANA, UNPLANNED, WATU WAKE WAKO ARROGANT, UN- EXPOSED na WAKO UNNECESSARILY REACTIVE. KWA KIFUPI SI MAHALI PAZURI PA KUISHI,... its simply chaotic!!!!
Ni wapi Tz hii kuko planned na infrastructure ya kueleweka?? Kama unazungumzia vigezo hivyo Tz hakutakuwa na jiji.... Tuachieni Arusha yetu na wewe mtoa mada siku nyingine hakikisha una fuba za kueleweka uweze kufanya shopping bila kulia lia, na badala ya kwenda kulala guest za Ngaleloo na Lengijave ulale sehemu za maana. Muhimu ukipanga tena safari tunisha mfuko
 
Ndio ukweli jamani!
Huitaji mwenyeji kujua kuwa mji Fulani mzuri! Arusha haijapangwa kabisa!
In 10 years Dodoma itakuwa nzuri kuliko mji wowote Tanzania! Ila in 100 years Arusha haitoweza kuwa hata kama Moshi! Mji haukui kwa kuwa haupangiki, it is between mji na kijiji! Mashamba, mifugo na makazi vyote vimechanganyika!mumcant tell kama upo town au bush!
Sawa umenena wakumlaumu ni nani kwenye miundo mbinu serikali au mwananchi?Mikoa kama arusha shinyanga mwanza ilitakiwa ipangwe mapema na kuendelezwa na kua na barabara nzuri kutokana na kuchangia uchumi wa nchi kwa miaka hiyo kuanzia utalii,madini,kilimo,uvuvi na biashara na ufugaji.Je viongozi waliona umuhimu wa kuendeleza hii miji,wakati mwingine atuwezi walaumu wananchi tunapaswa tuwalaumu walioshindwa kupendezesha mini yetu.Na nafikiri mikioa upinzani inashinda wananchi wake walitambua maendeleo ya kweli nijitihada za mtu mwenyewe na siyo chama na T-shirt na kanga.Pia mikoa ya nyanda za juu kusini mnazalisha chakula sana msibweteke mikoa ya kaskazini na hata Dodoma walishaongoza kwa uzalishaji wa chakula kipindi cha nyuma hivyo trend na majira ya uzalishaji yanabadilika.
 
Yaani kumbe kulia kotee ni ukubwa wa bei? Haahaaaaa! baki huko huko ambako matumbo yenu mmeyageuza makontaina ya kubebea unga, Arusha hela ipo ukiitafuta na uzuri wa Arusha sio dampo la bidhaa feki kama Dar ndio maana vitu origional na bei ni ya ukweli, Arusha hakkuna kukaa kijiweni asubuhi na jioni urudi na hela kwako, lazima ufanye kazi kuitafuta pesa, na ukishaipata unaitumia vyema tu kwa kununua hizo bidhaa safi. Unataka bidhaa mbovu kama zile za kariakoo ambazo matumizi yake ni wiki mbili? Bakini huko huku tunakula vitu origional ndani ya hewa safi viwanja vya kijanja na kila week end vinajaa, hapo ndio ujiulize kama pesa ngumu kumbi za starehee mbona zipo full?! Acheni uvivu njoo mpige kazi mpate hela sio kuomba omba mapedeshee wawabebe, kwanza Arusha hakuna pedeshee hata mmoja, kuna mabilionea umri hauzidi 50 na wanapesa mbaya sasa kama hakuna pesa hawa wanamiliki nini? Sekta binafsi Arusha ndio zimeajiri watu wengi kuliko serikali, ukiachana na walimu, bado hamuoni tu? Kizuri chajiuza, mtachoka sana na sasa chini ya UKAWA speed kubwa ya maendeleo.
Naona unadhihirisha mtoa mada yuko sahihi.
 
Sijui mtoa thred analinganisha arusha na mkoa upi...Ukweli nikwamba Arusha haijajengeka kama Dar, ila ukitaja Majiji maarufu na mizuri Arusha ni ya pili...nafikiri mtoa mada hujatembelea mikoa mingi..ndugu zangu niwaambie tu kuna mikoa hapa Tz utadhani kijiji kimoja alichotaja mtoa mada kama Ngaramtoni au kwa morombo...nimetembea mikoa karibia zote za Tz....hamna cha Mwanza wala sijui mbea....Arusha bado iko juu zaidi...Kitu kimoja tu ambacho Arusha inayo watu wa mikoa mingine na hasa Dar hawatezakumudu... Nikwamba maisha yako juu sana..vitu vinauzwa ghali tofauti na mikoà mingine. Na hii inasababishwa na utalii. Na kwasiojua arusha kuitwa Geneva Of Africa ni kutokana na hali hewa na mandhari ya jiji lenyewe...
Kweli mtoa mada yuko sahihi....OVERRATED.
 
Wee kima sana..!! Mijitu mingine.. utakuta kwenu hata pikipiki hamna.. unaongelea ARUSHA..!! Maskini wa akili ni maskini wa maisha yake yote kwa kila kitu.. ww maskini wa akili.. so maskini wee..!!
Unatukana bure mkuu! Kweli Arusha inapaishwa zaidi kuliko uhalisia. Huenda ni kutokana na Tanzanites, mbuga na Mount Meru...ndo maana unapewa air time.

Kuna mikoa mingine hali ya hewa safi, na kuna vivutio vingi tu vya utalii sema tu bado hazijapata coverage.

Mfano, mkoa wa Rukwa wakiamua kuutengeneza...unaweza kuipita mbali Arusha...basi tu umeachwa nyuma. Tena kuna vivutio vya utalii vingi tu!
 
Nakubaliana na INATEGEMEA NA MWENYEJI WAKE AKAWA HAJUI MAENEO PRIME, lakini sikubaliani na Sattelite Cities Kali ambazo Dar Hakuna-Hapo nakataa.
Hauhitaji kuwa na mwenyeji ili kuuona uzuri wa mji. Kama mji ni mzuri sana utauona tu...ukiona mpaka upate mwenyeji ndo uuone uzuri ujue hilo tayari ni doa!
 
Wanabodi habari zenu
Nilikuwa sijawahi kufika Arusha, tangu nikiwa sekondari mpaka chuo nimesoma na machalii mbalimbali toka mkoa huo wa Arusha, wamekuwa wanapasifia sana kama si mno.

Hata wadau mbalimbali waliowahi kufika wamekuwa wanapasifia sana ni pazuri na pamejengeka vizuri hata kufikia hadhi ya kuitwa " Geneva of Africa ". Pia uwepo wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, uwepo wa machimbo ya madini na sekta ya utalii imechangia sifa za Jiji hilo la Arusha kuzagaa mikoa mingine hali inayofanya kila mtu atamani kufika Arusha akiamini ni pazuri kama alivyohadithiwa.

Mungu si Athumani, nikapata safari ya kwenda Arusha wiki iliyopita, MAMA YANGU!! Sikuamini macho yangu, ni sehemu moja ya kawaida sana tena sana. Kwanza hapo wanapopaita Mjini ni pa kishamba sana, Stand ya mabasi ni kawaida yaani hata stand ya daladala ya Mbezi ni nzuri.
Majengo yenyewe ni ya kuhesabu hapo katikati ya mji.

Nikaingia sasa maeneo kama Sakina, Moshono, Njiro pakawaida sana, nikaamini mkoa ni mkoa tu!! Jiji kama lile kuna hiace zile fupi ndio zimejaa mpaka kero, huko Ngaramtoni kuna vumbi ambalo sijawahi kuliona kabisa. Bei ya vitu ndio usiseme yaani kitu cha kuuzwa elfu 5 utaambiwa elfu 30. Hata viwanja vya kijanja vya kujirusha Arusha ni vya kuhesabu na ushamba mwingi sana.

Kitu pekee cha kujipongeza na kujisifu kwa watu wa Arusha ni uwepo wa mbuzi choma kwa Mrombo, baasi hiko ndio nimeona tu!! Kwa maneno mengine Arusha ni overrated region.
Mkuu uko sahihi kabisa..
 
Arusha kuna sehemu zinaitwa Kijenge Juu, Unga Limited, na Sanawari karibu na Tangi la Maji hayo maeneo ukifika utastaajabu kama kweli uko Arusha. Kuna jamaa wametulia wanagonga pombe inaitwa DADII na nywele zimebadilika rangi. Anayoongea mtoa mada ni kweli kabisa kama iwapo Arusha ingepangiliwa vizuri ingelikuwa ni tishio kwa miji ya Afrika lakini kwa jinsi ilivyo mji hauvutii.
Hiyo mitaa huwa nikipita ni vituko tupu kwakeli huto amini!
 
Barabara nyingine ni inayotoka Silent Sakina kama unapandisha kwenye Kiranyi. Nyingine ni barabara inayotokea maeneo ya Esso kupandisha Sakina kupitia Matejoo. Kimsingi zipo kibao.
Nakubaliana na mtoa mada Arusha ni overrated sana.
Mkuu ahsante sana, tuko pamoja
 
"Daladala" za Arusha wao wanaita Hiece, zinazoingia mjini kati ni mabovu na hayastahili kabisa kuwa kwenye Jiji. Ni magari ambayo yangepaswa kuanzia huko Kisongo au Ngaramtoni kuelekea vijijini.
 
"
Safety lastSenior Member
Mikoa ya Kagera Mwanza,Geita,Kigoma na Singida imetajwa jana Bungeni kama mikoa ambayo wananchi wake ni maskini wa kipato kiasi wanashindwa hata mlo wa siku.

============

Dodoma. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amewasilisha bungeni Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa Fedha wa 2016/17, huku akitaja mikoa mitano inayoongoza kwa umaskini nchini.

Dk Mpango alisema mikoa hiyo imebainika katika Tathimini ya Hali ya Umaskini kimaeneo iliyofanyika kwa kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 na utafiti wa Hali ya Kipato na Matumizi katika kaya ya mwaka 2012.

Aliitaja mikoa hiyo na asilimia ya umaskini kwenye mabano Kigoma (48.9), Geita (43.7), Kagera (39.3), Singida (38.2) na Mwanza (35.3).

Kwa upande wa wilaya umaskini mkubwa upo katika Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma na Biharamulo mkoani Kagera na takribani asilimia 60 ya watu wapo chini ya mstari wa umaskini wa mahitaji ya kimsingi.

“Hii ina maana kuwa maeneo ya vijijini hususan pembezoni bado Watanzania wengi wanaishi kwenye umaskini na uwezo wao wa kupata mahitaji ya msingi mdogo,” alisema.

Dk Mpango aliitaja mikoa mitano yenye ahueni ya umaskini wa kipato kuwa ni Dar es Salaam (5.2), Kilimanjaro (14.3), Arusha (14.7), Pwani (14.7) na Manyara (18.3).

Pia, Dk Mpango alisema utafiti wa Hali ya Afya ya Mama na Mtoto, uliofanyika mwaka 2015 unaonyesha idadi ya wasichana waliopata watoto katika umri wa miaka 15 hadi 19 imeongezeka na kufikia asilimia 27 mwaka 2015 kutoka asilimia 23 mwaka 2010.

“Kuongezeka kwa wasichana wanaopata watoto wakiwa na umri mdogo, yaani miaka 15 hadi 19 siyo dalili nzuri kwani inaashiria kuongezeka kwa utegemezi na kudumaza jitihada za kuondoa umaskini katika jamii,” alisema.

Kuhusu wastani wa pato la kila mtu, Dk Mpango alisema pato la wastani la mtu limepungua kutoka Dola 1,047 za Marekani kwa mwaka 2014 hadi Dola 966.5 mwaka 2015.

Alisema hali hiyo imetokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania. “Hivyo ni dhahiri kuwa bado kunahitajika msukumo zaidi wa kuongeza ukuaji wa Pato la Taifa ili kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya kufikia Dola 3,000 za Marekani kwa pato la kila mtu na kuwa nchi ya uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025,” alisema.

Kuhusu urahisi wa kibiashara, Dk Mipango alisema taarifa ya urahisi wa kufanya biashara ya Benki ya Dunia (WB) ya mwaka 2015 , Tanzania ilipanda kwa nafasi moja katika vigezo vya urahisi wa kufanya biashara kwa kushika nafasi ya 139 kati ya nchi 189 duniani ikilinganishwa na nafasi ya 140 mwaka 2014. Alisema mwaka wa fedha 2016/17, Serikali imetenga Sh11.8 trilioni sawa na asilimia 40 ya bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo."
 
Back
Top Bottom