mchome jr
JF-Expert Member
- Apr 9, 2015
- 599
- 748
Hana hoja ya msingi...!Wewe kweli ni mchochezi
Hana hoja ya msingi...!Wewe kweli ni mchochezi
Nafikiri wale wanaosema Dar maisha magumu inabidi waache sasa kubana pua. Hio ripoti inaonesha Dar ndio kuna kiwango kidogo cha umaskini asilimia 5.2. Wa pili klm asilimia 14.3 kuna tofauti karibia asilimia 10 nzima.Dk Mpango aliitaja mikoa mitano yenye ahueni ya umaskini wa kipato kuwa ni Dar es Salaam (5.2), Kilimanjaro (14.3), Arusha (14.7), Pwani (14.7) na Manyara (18.3).
Teh teh ha ha ha hakapiga porojo wee mwisho wa siku akatoa point haswaa iliyomsukuma kuanzisha uzi huu kwamba "kitu cha elfu 5 utauziwa 30" sasa umasikini wake unamfanya awe na hasira zinazoambatana na chuki kali
umasikini mbaya sana!
ndo hivyo masta....Teh teh ha ha ha ha
Umenichekesha sana
Kumbe jijini shule haha ha ha ha ha
Wanabodi habari zenu
Nilikuwa sijawahi kufika Arusha, tangu nikiwa sekondari mpaka chuo nimesoma na machalii mbalimbali toka mkoa huo wa Arusha, wamekuwa wanapasifia sana kama si mno.
Hata wadau mbalimbali waliowahi kufika wamekuwa wanapasifia sana ni pazuri na pamejengeka vizuri hata kufikia hadhi ya kuitwa " Geneva of Africa ". Pia uwepo wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, uwepo wa machimbo ya madini na sekta ya utalii imechangia sifa za Jiji hilo la Arusha kuzagaa mikoa mingine hali inayofanya kila mtu atamani kufika Arusha akiamini ni pazuri kama alivyohadithiwa.
Mungu si Athumani, nikapata safari ya kwenda Arusha wiki iliyopita, MAMA YANGU!! Sikuamini macho yangu, ni sehemu moja ya kawaida sana tena sana. Kwanza hapo wanapopaita Mjini ni pa kishamba sana, Stand ya mabasi ni kawaida yaani hata stand ya daladala ya Mbezi ni nzuri.
Majengo yenyewe ni ya kuhesabu hapo katikati ya mji.
Nikaingia sasa maeneo kama Sakina, Moshono, Njiro pakawaida sana, nikaamini mkoa ni mkoa tu!! Jiji kama lile kuna hiace zile fupi ndio zimejaa mpaka kero, huko Ngaramtoni kuna vumbi ambalo sijawahi kuliona kabisa. Bei ya vitu ndio usiseme yaani kitu cha kuuzwa elfu 5 utaambiwa elfu 30. Hata viwanja vya kijanja vya kujirusha Arusha ni vya kuhesabu na ushamba mwingi sana.
Kitu pekee cha kujipongeza na kujisifu kwa watu wa Arusha ni uwepo wa mbuzi choma kwa Mrombo, baasi hiko ndio nimeona tu!! Kwa maneno mengine Arusha ni overrated region.
Tunauwezo wa kununua ndo mana tunakamatwa.siku nyingine uje na hela za kutosha,mana inaonekana ungenunua hizo raba ungeomba lift kurudi kwenuArusha hela ngumu kupatikana halafu bidhaa zipo juu mno nakumbuka mwaka jana nilienda kwenye msiba nilipofika nikaona kutembea tembea mtaani na raba muda wote sijazoe ikabidi nimwambie mwenyeji anipeleke sehemu nikanunue sandals akinipeleka kwenye soko flan hivi local aisee kuuliza bei naambiwa 45k wakati quality ileile hapa mjini dar unaipata kwa 15k hahaha hela nilikuwa nayo lakini ikabidi nighairishe zoezi moyoni nikasema kwa hizo bei mtawakamata haohao wa arusha
Mkuu acha porojo zako za ngarenaroTatizo wewe umeishia stand ..kuna satellite cities Arusha ...ambazo DAR hakuna......inategemea mwenyeji wako
Mkuu umemaliza kila kitu kilichobaki ni ubishi kwa wazawa wa huko.Alichokiandika mleta mada ni kitu cha ukweli kabisa....isipokuwa tu ni ubishani wa mtu kwao.....
Kabla ya hujafika Arusha unajenga picha kubwa sana ya jijj la Arusha lakini ukifika huko unarudi na picha ndogo sana ya mkoa wa Arusha.....
Wanging'ombe?? Hahahaaa kuna mtu anafananisha Arusha na Iringa na Mbeya kweli mmetoboka.Hayo ni mapenzi yako hakuna anaekuzuia, kwa Tz Arusha na moshi ni mikoa isiyonivutia kabisa kuishi, labda mikoa ya Iringa mbeya na Dar tu
Asante bosi!Au nayo unaoverrate!
DuuhSi Mwanza tu ambayo ni bora kwa Arusha, hata Mbeya ni bora zaidi ya Arusha.
Mkuu shikamoo"Daladala" za Arusha wao wanaita Hiece, zinazoingia mjini kati ni mabovu na hayastahili kabisa kuwa kwenye Jiji. Ni magari ambayo yangepaswa kuanzia huko Kisongo au Ngaramtoni kuelekea vijijini.
Asante!!Nimezaliwa arusha, nimetembea majiji yote ya afrika mashariki, kiuhalisia majiji haswa ni nairob na dar, haya mengine yoote, mombasa, mwanza, ars, kisumu, hamna tofaut kabisa, kampala naweza ilinganisha na mombasa , arush inaongelewa sana kwa sababu za kitalii, diplomacy, tanzanite na vingine na ndio kinachoifanya watu kudhan ni pa kipekee na tofauti sana but ni sawa na miji mingine inayokuwa, hamna cha mwanza wala nini kote hamna jiji!
We call it " Povu "Hahaa, ulitakaje kwani?!
Huku ni mkoani tuachie jiji letu wenyeji ndio twajua uzuri na utamu wake!!
Bakia huko unakokuona pamekucha maana huo ndio mtazamo wako! Hata hapo unapopaona pamekucha ni pa kishamba tu kwa wengine!!
Wachagga katika ubora wenuNa walioukuza zitakuwa haziwatoshi nadhani!
Clinton Bill ndio aliyetoa nickname ya Arusha kuwa ni Geneva of Africa!! Tafakari...!
Kwa Tanzania ni Arusha na Moshi tu ndio mikoa inayonivutia kuishi au kuweka makazi!!