Arusha imekuzwa kuliko ilivyo!! ( Overrated )

Arusha imekuzwa kuliko ilivyo!! ( Overrated )

5526cbdb8238820514918848d3b3af73.jpg
Hii ndio sakina sasa
 
kwa kifupi kwa mtu alietokea dar arusha ya kawaida sana labda kwa watu waliotokea maeneo mengine ndio wataisujudu.
 
Hii ndio sakina sasa
...acha upambe mtoto wa kiume utaolewa!, yani umepiga picha jioni ukiwa shimoni tena maeneo ya kawaida makusudi ili tu ulete umbeya huku!.... hiyo sakina ya wapi uliyopiga picha wewe!, magorofa, supermarket, restaurants hujaziona Sakina?!
 
...acha upambe mtoto wa kiume utaolewa!, yani umepiga picha jioni ukiwa shimoni tena maeneo ya kawaida makusudi ili tu ulete umbeya huku!.... hiyo sakina ya wapi uliyopiga picha wewe!, magorofa, supermarket, restaurants hujaziona Sakina?!
Anajitekenya alafu anacheka mwenyewe kweli kazi ipo...!camera yenyewe mbovu picha hata haieleweki
 
Nimezaliwa arusha, nimetembea majiji yote ya afrika mashariki, kiuhalisia majiji haswa ni nairob na dar, haya mengine yoote, mombasa, mwanza, ars, kisumu, hamna tofaut kabisa, kampala naweza ilinganisha na mombasa , arush inaongelewa sana kwa sababu za kitalii, diplomacy, tanzanite na vingine na ndio kinachoifanya watu kudhan ni pa kipekee na tofauti sana but ni sawa na miji mingine inayokuwa, hamna cha mwanza wala nini kote hamna jiji!
 
Sijui mtoa thred analinganisha arusha na mkoa upi...Ukweli nikwamba Arusha haijajengeka kama Dar, ila ukitaja Majiji maarufu na mizuri Arusha ni ya pili...nafikiri mtoa mada hujatembelea mikoa mingi..ndugu zangu niwaambie tu kuna mikoa hapa Tz utadhani kijiji kimoja alichotaja mtoa mada kama Ngaramtoni au kwa morombo...nimetembea mikoa karibia zote za Tz....hamna cha Mwanza wala sijui mbea....Arusha bado iko juu zaidi...Kitu kimoja tu ambacho Arusha inayo watu wa mikoa mingine na hasa Dar hawatezakumudu... Nikwamba maisha yako juu sana..vitu vinauzwa ghali tofauti na mikoà mingine. Na hii inasababishwa na utalii. Na kwasiojua arusha kuitwa Geneva Of Africa ni kutokana na hali hewa na mandhari ya jiji lenyewe...
 
4d597e0f66d4c512bf5763ce6137f65a.jpg

Mtoa mada hayo hapo nyuma sio maghorofa au hapo Dar Es Salaam??? Arusha nilikaa miezi kadhaa kikazi aiseee ni patamu kinyamaaa...hali ya hewa muruuuuua kama marekani vile...viwanja vya ukweli sema ulienda kimasikini sana ukategemea kununua vitu vya buku buku...hahahaa next time jipange na mkwanja wa maana hakika utaipenda Arusha
 
Arusha all day every day. Nashangaa sana people toka Dar au place nyingine Tz wanakuja A town wanatembea maeneo ya kawaida wanasema wanaijua A town. Njoo na dough ya kutosha hautotaka uondoke Arusha. Hapa hali ya maisha ni juu na kuna mambo mengi ya kufanya, sahau huko mnako tembelea, I doubt wewe bado hustling hujui. Arusha all day everyday
Hakiri matope we, unasifia ugum wa maisha, et arusha maisha ghali kumbe we mjusi kwel
 
Wanabodi habari zenu
Nilikuwa sijawahi kufika Arusha, tangu nikiwa sekondari mpaka chuo nimesoma na machalii mbalimbali toka mkoa huo wa Arusha, wamekuwa wanapasifia sana kama si mno.

Hata wadau mbalimbali waliowahi kufika wamekuwa wanapasifia sana ni pazuri na pamejengeka vizuri hata kufikia hadhi ya kuitwa " Geneva of Africa ". Pia uwepo wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, uwepo wa machimbo ya madini na sekta ya utalii imechangia sifa za Jiji hilo la Arusha kuzagaa mikoa mingine hali inayofanya kila mtu atamani kufika Arusha akiamini ni pazuri kama alivyohadithiwa.

Mungu si Athumani, nikapata safari ya kwenda Arusha wiki iliyopita, MAMA YANGU!! Sikuamini macho yangu, ni sehemu moja ya kawaida sana tena sana. Kwanza hapo wanapopaita Mjini ni pa kishamba sana, Stand ya mabasi ni kawaida yaani hata stand ya daladala ya Mbezi ni nzuri.
Majengo yenyewe ni ya kuhesabu hapo katikati ya mji.

Nikaingia sasa maeneo kama Sakina, Moshono, Njiro pakawaida sana, nikaamini mkoa ni mkoa tu!! Jiji kama lile kuna hiace zile fupi ndio zimejaa mpaka kero, huko Ngaramtoni kuna vumbi ambalo sijawahi kuliona kabisa. Bei ya vitu ndio usiseme yaani kitu cha kuuzwa elfu 5 utaambiwa elfu 30. Hata viwanja vya kijanja vya kujirusha Arusha ni vya kuhesabu na ushamba mwingi sana.

Kitu pekee cha kujipongeza na kujisifu kwa watu wa Arusha ni uwepo wa mbuzi choma kwa Mrombo, baasi hiko ndio nimeona tu!! Kwa maneno mengine Arusha ni overrated region.

Hahaa, ulitakaje kwani?!
Huku ni mkoani tuachie jiji letu wenyeji ndio twajua uzuri na utamu wake!!
Bakia huko unakokuona pamekucha maana huo ndio mtazamo wako! Hata hapo unapopaona pamekucha ni pa kishamba tu kwa wengine!!
 
Siku zote huwa nasema hapa, arusha ina Jina kubwa kuzidi mji wenyewe, arusha hakuna lolote mji wa kawaida mno umekuzwa tu kwenye vyombo vya habari

Na walioukuza zitakuwa haziwatoshi nadhani!

Clinton Bill ndio aliyetoa nickname ya Arusha kuwa ni Geneva of Africa!! Tafakari...!

Kwa Tanzania ni Arusha na Moshi tu ndio mikoa inayonivutia kuishi au kuweka makazi!!
 
Na walioukuza zitakuwa haziwatoshi nadhani!

Clinton Bill ndio aliyetoa nickname ya Arusha kuwa ni Geneva of Africa!! Tafakari...!

Kwa Tanzania ni Arusha na Moshi tu ndio mikoa inayonivutia kuishi au kuweka makazi!!
Hayo ni mapenzi yako hakuna anaekuzuia, kwa Tz Arusha na moshi ni mikoa isiyonivutia kabisa kuishi, labda mikoa ya Iringa mbeya na Dar tu
 
kwa kifupi kwa mtu alietokea dar arusha ya kawaida sana labda kwa watu waliotokea maeneo mengine ndio wataisujudu.

Uzuri ni subjective!
Nimezaliwa na kukulia Dar, ila maisha ya Dar kwa sasa ni full stress japo wengi watakuambia ni jiji la kishua (wengi wao wametokea bush)!
Pengine swali la kujiuliza... je mtoa mada analinganisha Arusha na mkoa gani mwingine?
 
Hayo ni mapenzi yako hakuna anaekuzuia, kwa Tz Arusha na moshi ni mikoa isiyonivutia kabisa kuishi, labda mikoa ya Iringa mbeya na Dar tu

Ni mtazamo wako tu vile vile!
Ila kusema A town inapewa sifa isizostahili sio sahihi. ., lazima itambulikane kuwa kuna vigezo vinavyozingatiwa kabla ya mji fulani kupewa hadhi iliyonayo!! Watu huwa hawakurupuki!

Jiulize Clinton ni jiji gani Marekani au Ulaya asilolijua hadi akurupuke kusema Arusha ni Geneva of Africa?!

Tuachieni jiji letu jamani UZURI na UTAMU wake twaujua sie wakaazi!
 
Back
Top Bottom