Arusha imekuzwa kuliko ilivyo!! ( Overrated )

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,772
7,272
Wanabodi habari zenu
Nilikuwa sijawahi kufika Arusha, tangu nikiwa sekondari mpaka chuo nimesoma na machalii mbalimbali toka mkoa huo wa Arusha, wamekuwa wanapasifia sana kama si mno.

Hata wadau mbalimbali waliowahi kufika wamekuwa wanapasifia sana ni pazuri na pamejengeka vizuri hata kufikia hadhi ya kuitwa " Geneva of Africa ". Pia uwepo wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, uwepo wa machimbo ya madini na sekta ya utalii imechangia sifa za Jiji hilo la Arusha kuzagaa mikoa mingine hali inayofanya kila mtu atamani kufika Arusha akiamini ni pazuri kama alivyohadithiwa.

Mungu si Athumani, nikapata safari ya kwenda Arusha wiki iliyopita, MAMA YANGU!! Sikuamini macho yangu, ni sehemu moja ya kawaida sana tena sana. Kwanza hapo wanapopaita Mjini ni pa kishamba sana, Stand ya mabasi ni kawaida yaani hata stand ya daladala ya Mbezi ni nzuri.
Majengo yenyewe ni ya kuhesabu hapo katikati ya mji.

Nikaingia sasa maeneo kama Sakina, Moshono, Njiro pakawaida sana, nikaamini mkoa ni mkoa tu!! Jiji kama lile kuna hiace zile fupi ndio zimejaa mpaka kero, huko Ngaramtoni kuna vumbi ambalo sijawahi kuliona kabisa. Bei ya vitu ndio usiseme yaani kitu cha kuuzwa elfu 5 utaambiwa elfu 30. Hata viwanja vya kijanja vya kujirusha Arusha ni vya kuhesabu na ushamba mwingi sana.

Kitu pekee cha kujipongeza na kujisifu kwa watu wa Arusha ni uwepo wa mbuzi choma kwa Mrombo, baasi hiko ndio nimeona tu!! Kwa maneno mengine Arusha ni overrated region.
 
Back
Top Bottom