Camilo_Cienfuegos
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 11,378
- 15,384
Naiangalia tena hii mechi ss football plus
Striker na wakati hakuna nafasi zilizotengenezwa za kumuitaji uyo striker,Kuna mtu aliwahi kuzungumzia,walizungumzia na tunazungumzia.We need a STRIKER
Uko sahihi kabisa na Fabio Vieira leo ametoa pasi murua sana kwa Jesus kwenda kufunga, na hivyo ndivyo Zinchenko apaswa kuangalia analink vipi mchezo na mchezaji wake wa kiungo (Havertz).Haya masuala ya kumsubiri mtu ajifunze wakati ambao tunataka matokeo ndio jambo ambalo sisi mashabiki hatuwezi kulivumilia.
Kama kuna watu walioko tayari kama Fabio/ESR ni bora muda mwingi wapewe wao huku tukimpa muda kidogo kidogo Havertz wa kujifunza.. awe anaingia time kama zile anazoingia Fabio, dk ya 75 hivi muda huo tukiwa tunaongoza goli 2 na kuendelea au asubiri aanze mechi za Carabao na FA.
Yote sawa mkuu, Hakuna anayelazimisha aanze ,tatizo wadau wanaweka chuki SanaWadau humu hatupingi Kai kupata time. Everyone anahitaji kucheza.
Vieira alipata time akianzia nje. Na Kai iwe hivi.
Nili Note hiki kitu na mimi, baada ya kupika pasi ya hovyo iliyoenda kuzaa bao la Man U.Nilikua naona Martinelli hamuamini Kai, akipata mpira Kai akitokea Martinelli anatafuta njia kwingine.
Katika games nne za points 12 tumepata 10. Siyo mwanzo mbaya hata kidogo. Kilichopo benchi lione ni kivipi tunaweza secure points nyingi zaidi
Kwann asianze na jorginho na rice kipind hiki partey hayupo naona kam mchele utatupa faida san ukiwa juu kidogo sabb jamaa anatupa energy y kutosha kila angle y uwanjaHapo ndipo kazi ya umeneja inapokuwa muhimu sana kwa timu.
Player management ni kitu kizuri sana na Arteta safari hii akiweza kuwamanage wachezaji basi Arsenal itafika mbali kwenye mechi za PL na CL.
Partey kwa sasa ni kwa mechi chache akipona na kwa kuangaliwa sana ila nahisi Arsenal watatafuta DM mwingine ikifika January.
Muda wote alochezea Chelsea Havertz alitumika kama mashambuliaji na ndipo alipopata shida ya kutofunga magoli mengi.Nachokiona ni kwamba Kai siyo m bovu ila tu kwenye role ambayo anataka arteta acheze sana kuizoea kwa sababu yeye ni mshambuliaji . Xhaka ilikuwa rahisi kui master vizuri. Hata Fabio mwanzo alikuwa hivi hivi hasa lege lege Nashukuru sasa hivi Fabio anau wezo mzuri sana . Hata siku Ode akikosekana ntakuwa sina wasi wasi kutokana na uwepo wa Fabio. Ila leo naamin kama angeanza jorginho na rice game ilikuwa inaisha mapema sana
Me nataka Rice achukue Role ya Xhaka Anaiweza vizuri sana . Pale chini amuache Parteyna JorginhoRice taratibu anachukua Dimba la Kati
£105m
Harvertz kachukua Nafasi ya Xhaka ???? HowHavertz amechukua nafasi ya Xhaka na ataweza kuwa sawa.
Anatakiwa awe na maelewano mazuri ya Zinchenko upande wao wa kushoto.
Atakuwa sawa tu na atafunga magoli kama ilivyokuwa kwa Xhaka.
Mpira wa wenzetu ni mipango na mifumo na ili kuipatia kucheza yatakiwa uwe na ustahamilivu.
Meneja ana imani na Harvetz na atakuwa acheza kila mechi ili kufit in katika mfumo wa uchezaji wa Arsenal.
Ila huko mbele Jesus atarudi kuanza mechi na Nketia atarudi bench.
Pia hali ya hewa kulikuwa na joto kali hivyo kuathiri uchezaji kwa kuufanya uwe slow sana.
Jorginho ni mbadala wa Odegaard hivyo akiingia Jorginho na huku Odegaard yumo kutaleta hitilafu kwenye mfumo wa uchezaji.Kwann asianze na jorginho na rice kipind hiki partey hayupo naona kam mchele utatupa faida san ukiwa juu kidogo sabb jamaa anatupa energy y kutosha kila angle y uwanja
Alipokuwa akicheza Xhaka ndipo anapocheza Kai Harvetz na ndo maana Xhaka akaruhusiwa kuondoka.Harvertz kachukua Nafasi ya Xhaka ???? How
May be kabadilishiwa majukumu ila kusema amechukua nafasi ya Xhaka ni uongo
Nafasi ya Xhaka ilikua inatoa Assist na Magoli
Kwa sasa kitu icho hakipo mpaka sasa
Nguvu ya kuzuia wakati hatuna mpira now zinazibwa nafasi ambapo kwenye hilo Kai anasaidia
Mtu naemuona anauwezo wa kuchangia Goals & Assist kwenye LCM alipokua anacheza Xhaka ni Fabio na Trousard ila kwa Kai naona Awe ST tu basi wawe wanaachiana nafasi na Nketia,Jesus
Tumeshinda ila Kai anatuchelewesha sanawazee Kai kaanza
sijui itakuwaje leo??
Kumbe he is one of us?We rarely lose when Anthony Taylor is officiating
Iyo game inaitaji mafundi tupu hasa LT19Havertz wengi wadhani ni striker au "deep lying midfielder" jambo ambalo si sahihi.
Arteta ataka Havertz awe analink mchezo kati ya Zincheko na Ben White na awe anakuja mwisho kumalizia shambulizi kwa kufunga goli.
Ndo maana mechi zingine zilopita amecheza kama "false 9" au attacking midfielder nafasi ambayo leo amecheza Odegaard kwa ufanisi mkubwa ikiwemo kufunga goli la kusawazisha.
Hivyo Havertz ni "deep lying midfielder", Odegaard ni attacking midfielder na Declan Rice ni central Midfielder nafasi ambayo ilikuwa ni ya Thomas Partey.
Havertz atakiwa sasa akazanie kujifunza kutopoteza mipira sana na pia kutokuwa slow kwenye kulink mchezo.
Hivyo mechi ijayo na Everton utashangaa Arsenal ikiwa ni timu ingine kabisa kwa kutumia mfumo mwingine ili kumzuia Sean Dyche asicheze "10 men behind the ball" kisha kuvizia kufanya counter attack kama alivyokuwa akifanya Rashford leo.
Pressing na athleitism imeshuka sio utaniTimu yetu imepoteza nguvu ya utafutaji, tunacheza kawaida sana toka msimu huu uanze
Kabla meneja hajapanga timu huangalia timu pinzani na kisha huangalia ni wachezaji wepi wafaa kuanza mechi.Kwanini Trossard/Rowe/Vieira wasianze kwenye LCM kisha kama kocha ana mahaba na Kai amu-intergrate taratibu kwenye kikosi kwa kuingia sub? Mbona anafosi sana