Mkuu wangu sana Kweli.....Nimekusoma vizuri sana....
Timu yetu(kwa kiwango walichoonesha juzi wakati wa game na Newcastle) bado ni mbovu mkuu...Hatuna kiungo cha kuaminika,hatuna beki 4 mzuri wa kusaidiana na kitasa TV5, hatuna beki 3 mzuri(Gibbs akiumia sijui nani atacheza,Traore?),hatuna mshambuliaji mfungaji mzuri wa kusaidiana na RVP pale mbele.....Pia Sagna akiumia sijui itakuwaje....
Mpira wa sasa ni pesa mkuu,ni pesa ndizo zimeifanya Chelsea ikawa tishio kwani iliweza kusajili wachezaji wa maana kiasi cha kutupoka ile nafasi yetu ya kuwa wapinzani na washindani wakubwa wa Man Utd kwenye title race ya EPL.....Ni pesa ndizo zinaifanya Man City kutuondoa kwenye Big 3 ya EPL....Na ni pesa ndizo zitatufanya tusiwepo hata kwenye Big 4 ya EPL.....Tatizo Arsenal si pesa,tatizo ni sera mbovu za AW na Directors wake.....Wanaweka pesa mbele kuliko maslahi ya timu.....
Haiwezekani Arsenal iliyokuwa tishio kubwa katika EPL,ambayo ilikuwa ikipokezana ubingwa na Man Utd leo hii ikawa nyuma ya Man City na Chelsea.....Haiwezekani hata kidogo.....AW na bodi yake wanatakiwa wafanye maamuzi magumu,wazitumie pesa watakazozipata kwa kuwauza Fabregas na Nasri kuwanunua wachezaji wa maana....Nashangaa sana kusikia eti AW anabargain kumnunua beki mahiri kama Chris Samba kwa paundi mil 12,eti anataka kununua chini ya hapo....Huu ni upuuzi.....Pia juzi kasema hana mpango wa kuwanunua Jadson wala Mata,hii ina maana hana mpango wa kununua kiungo atakayeziba pengo la Nasri wala nafasi ya Fabregas?.....Hiki kitakuwa ni kichekesho,maana huyo Ramsey ambaye anategemea ndiyo ataziba pengo la Nasri/Fabregas sijaona lolote alilolifanya juzi zaidi ya kukimbiakimbia uwanjani na kupoteza mipira....Hata Frimpong bado sana kumtegemea......
AW anapaswa kusajili wachezaji wa maana(bila kuangalia bei zao),tumechoka kwa kweli kweli kuwa wasindikizaji kwa misimu zaidi ya mitano.....Tusiitumie timu ya wakubwa kuwaandaa/kuwatengeneza wachezaji,wachezaji waandaliwe kwenye academy na kwenye timu ya reserves lakini si kwenye timu ya wakubwa,hii ni bahati nasibu na ni utaratibu ambao tayari umeonesha kufeli(kwa miaka mitano iliyopita)......Nina uhakika Liverpool,Newcastle na Spurs wakiendelea kusajili na kukaa sawa na sisi tusiposajili msimu huu tutakuwa nyuma yao......Kwangu mimi kuwa nyuma ya timu hizi hakuna tofauti na kuwa nafasi ya 10 kama sio ya 15....
Arsenal haikupaswa kuwa nyuma ya Chelsea wala Man City,Arsenal size yake ilikuwa ni Man Utd basi.......Arsenal siyo timu ya kukosa hata kombe la Carling kwa kufungwa na vibonde walioshuka daraja Birmingham....
Nawakumbuka sana The Invincibles