Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread


Kwenye msafara wa nguchiro hata
pimbi wapo. khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee


...safari hii jamaa wameanza visingizio na mapeeeema, hhha hhha hhha!...na bado
tunakuja na kelele mpya msimu huu...Halafu kuja na Id mbili mbili humu hatutaki,....
tunajuana wenyewe waarabu wa Pemba!

Roll Call na ianze sasa!
 

Belo is back ..... .... nasikia noisy neighbour anawakosesha usingizi, mtakoma mwaka huu. Vipi Chicha nasikia huko USA mambo hayakumwendea mswano .... ..... Chacha mlifikiri Obama angewakaribisha White House? Yule ni hammers au hamjui?


Kweli

Nasikia
peas of ant amekwenda kutafuta list ya Chelsick bado anabangaiza kampata padri bandia peke yake chacha anafikiria jinsi ya kurudi hapa na kuomba radhi.

Man City ni jirani zetu na lakini sio size yetu,Chicha kashawafunga Chelsea,Liverpool bado nyie tu msubirini
 
Mkuu hii division ulonipa ni muhimu sana kwani inahusiana na masuala yoote ya mbinu au "tactical purposes".

Nashukuru sana kwa wadhifa huo na ntakuwapo hapa mwezi ujao.

Arsenal huwa wanafanya mambo yao bila kutumia vyombo vya habari maana vyombo vyenyewe siku hizi vimekuwa kama vya kwetu tu Africa, yaani kuongea mambo bila kufanya upembuzi yakinifu.

Wachezaji waliosajiliwa mpaka sasa ni mmoja tu Gervinho ambae Mzee Wenger anataka acheze pembeni namba kumi akichukua nafasi ya Samir Nasri na Nasri atakuwa akicheza pale kati yaani namba nane. Nasri kwenye mechi zote za karibuni amekuwa akicheza namba nane akiwa amechukua nafasi ya Fabregas (hii ni mbinu pia ikiwa Fabregas atauzwa au atakuwa akikaa bench).

Gervinho_6.jpg

Gervinho (miaka 24) amesajiliwa na kwa gharama za paundi milioni 10.6 kutoka timu ya Lille ya France.

article-1311935584532-0D18427500000578-990670_636x300.jpg

Phil Jagielka mpaka sasa ni mchezaji wa Everton ya Uingereza.

article-1311257259116-048AA172000005DC-203985_636x300.jpg

Juan Mata mpaka sasa ni mchezaji wa Valencia ya Spain.


article-1311848913107-0D0A33A300000578-195121_636x300.jpg

Christopher Samba mpaka sasa ni mchezaji wa Blackburn.

Kuna kila uwezekano wa Arsenal kutoa kitita cha fedha kulipa gharama za usajili wa wachezaji muhimu watatu Juan Mata (Paundi Milioni 17.5) kutoka Valencia ya Spain, Phil Jagielka (Everton wanataka Paundi Milioni 18) na Chris Samba wa Blackburn ambao wanataka paundi milioni 12. Hizo ni jumla ya paundi milioni 44.5 na Arsenal ina akiba ya pesa benki mpaka sasa (ambayo haijaguswa ) paundi 110 milioni.

Ikiwa mambo yatakwenda sawa tactically Arsenal watakuwa na moja ya ngome ngumu kupitika ikijumuisha Kipa- Szczesny, Sagna, Vermaelen, Djourou na Jagielka ( kama deal likikubali) au Cocsielny.

Kiungo- Song, Wilshere, Nasri na Gervinho

Washambuliaji- Van Persie, na Carlos Vela

Wachezaji wa akiba- Juan Mata (kama deal litakubali) , Chris Samba(kama deal litakubali) , Arshavin, Aaron Ramsey na Thomas Rosicky.

Jumamosi tuna mechi ya kirafiki na Boca Juniors na Jumapili pale Emirates kutakuwa na Emirates Cup na timu yetu itaanza kucheza na Red Bull New York ambayo itakuwa na Thiery Henry miongoni mwa kokosi chake cha kwanza.


si kweli .. usajili wetu wa kwanza ni beki wa charton A. mbona mnamsahau! au coz le prof. alitumia vijisent vichache ...! umewasajili vijana wawili kutoka barca youth team ...

so total wapya emarates ni 4 !.. lakini usajili wa maana kwa maono yangu so far ni 1 tu! gervinho ... mbaye tulimuona kwe action! na yule aliyetoka charton A. amenza vibaya kwa kujifunga goli moja tamu saaana!

nasubiri kuwaona hawa madogo wawili toka barca youth ...
 
Naona kumekucha wakuu, safi sanaa mie niko busy namsaidia wajina ku-negotiate manake kuna watu wamechafua market kinoma.wao wakitajiwa bei tu wanakurupuka na kumwaga hela.Tuwe wavumilivu wakuu mambo yatakaa vizuri kila la kheri kwenye shughuli zenu za kila siku ,pamoja.
 
Naona kumekucha wakuu, safi sanaa mie niko busy namsaidia wajina ku-negotiate manake kuna watu wamechafua market kinoma.wao wakitajiwa bei tu wanakurupuka na kumwaga hela.Tuwe wavumilivu wakuu mambo yatakaa vizuri kila la kheri kwenye shughuli zenu za kila siku ,pamoja.
tupo pamoja katika kuitetea klabu yenye soka tamu duniani kote haijapata kutokea-Arsenal
 
Hii safu yetu ya ushambuliaji naona imekaa vizuri,
Ngoja tuone Leo vijana wetu watafanya nini!
 
Sidhani kama Arsenal inaweza kuchukua kombe ikiwa na wachezaji kama Almunia,Diaby,Eboue,Rosisky,Chamakh,hivi mmeshapata beki wa kushoto? au mnamtegemea Gibbs
 
List la leo watakaoanzaFabianski,traore,djouro,koscienly,jenkinson,wilshere,frimpong,nasri,gervinho,arshavin,van persie.
 
List la leo watakaoanzaFabianski,traore,djouro,koscienly,jenkinson,wilshere,frimpong,nasri,gervinho,arshavin,van persie.
Foward imekaa vizuri, but nipo worried na hiyo safu ya Ulinzi! Kwanini TV5 hajaanza?
 
Back
Top Bottom