Hakuna mmiliki mwenye akili timamu unaamua kumuacha beast striker kama Aubameyang aondoke unabaki na mfuga ndevu mpumbavu kama lakazete,hii timu ikipata mmiliki mwenye kuelewa maana ya uwekezaji kwenye soka kwa, wote pale hakuna anayestahili kubaki,wanapaswa wafurumushwe isibaki hata chupi kwenye kabati!.
Kuna muda ukiwaangalia wachezaji namna wanavyocheza unaweza kusema hawajala mwaka mzima au hawajalipwa misimu 6 mfululizo.
Bunley,Astonvilla,Brighton,watford n.k unakuta wanacheza kwa spirit ya hali ya juu japo huwa wanapoteza lakini kuna muda unaona kabisa wamepiga mpira,ukija kwa Arsenal unakuta wachezaji ni kuruka ruka tu uwanjani utadhani wanamizigo ya mabusha kwenye bukta zao,yaani wachezaji hawana uchu na uchungu wa kupigania matokeo.
Serikali ya Uingereza isipofanya fitna kama ambazo tunaziona kwa chelsea sasa hivi kuhusu mmiliki wake,basi Arsenal bado tunasafari ndefu sana ya mafanikio.
Miaka 2 ijayo Arsenal itabaki kuwa historia tu kama Nottingham forest.
Huu ndiyo Ukweli.
BILA STAN KROÈNKE NA MAPUMBAVU WENZIE KUIACHA TIMU KWA HIARI YAO WANAPASWA WASHINIKIZWE