Game dhidi ya man u.
Betting companies zinaamini tunalingana nguvu lakini wapiga kura wameipa ushindi man u. Hivyo tunaingia kwenye hii game na favorite wa kushinda mechi ni man u.
Na hawajakosea sana kulingana na recent time performance Arsenal hatuwezi kua favorite, man u kuanzia game na Newcastle au tangu ole atishiwe kibarua imekua ya moto mwanzo tulihesabia ushindi wao ni penati na VAR ila sasa hivi ushindi wao ni penati, VAR na juhudi za wachezaji.
Arsenal tunaenda huku tukiwa hatuna kiungo wa kusambaza mipira, picha za hivi karibuni zimeonyesha beki au kiungo wa Arsenal akiwa na mpira anakosa mtu wa kumpa mpira as kila mchezaji anaenda kwenye nafasi yake huku hakuna kiungo wa kuupokea huo mpira na kuwapelekea wenzie. Hivyo Arsenal imejikuta inategemea crosses ambazo nazo haziwezi kutumiwa vizuri.
Watu wanadai Auba karelax kisa mkataba. Pengine kwakua hakuna wa kumpa mipira na mabeki wamekua wakimkaba sana.
Luiz kaumia. Kumchezesha Saliba ni ishuas hana uzoefu na ligi, Holding na Chambers sidhani kama ni wazima so tunaweza kumrudia tena Mustafi. Kwa ubovu wa Mustafi katika spidi natarajia tusicheze 3 4 3.
Ushindi wetu utatarajia zaidi makosa ya Fridge na wan bisaka. Pia weledi wa refa, mike dean, refa wa leo anaongoza kuipa penati man u kuliko refa yeyote yule.
Game zinazofuatia huko uefa kwa man na europa kwa Arsenal siyo game ngumu sana naona timu zote zikikamia game hii mno kiasi Arteta anaweza kumpanga academy yeyote kati ya Willock au Nelson. Kwakua De Gea anajulikana natarajia outside the box shots ziwe nyingi.
Sisemi kama tutashinda ama la kwakua derby ni games ngumu kutabiri na wachezaji hujitoa zaidi ya 100% kwa games za hivi. Tulikua hovyo kuliko leo kipindi cha Emery yet man u alikufa na kusuluhu naye.
Natarajia a stunning performance.