Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Nawatakia wadau wote wa soka Christmas njema na mwaka 2011 wenye mafanikio.

Wazee wote wa darajani Stamford, Rev Masa, EL NINO, Rev Kishoka, Sanda Matuta, Ab-Titchaz, AljuniorTz na Invisible, bila kusahau wakongwe wa Old Trafford, Manda, Belo, Eqlypz, Idimi na Ngongo, pia washika bunduki wa Emirates, Arsene Wenger, Mbu, Kweli, Wacha1, Balantanda, Baba Mkubwa, Genekai, Questt, Bubu Ataka Kusema na Ng'wanza Madaso,....mzee Shedafa wa WHL na Acid wa Anfield na wengine wote ambao sikuweza kuwakumbuka kwenye post hii, I wish you and your loved ones a Merry Christmas and Happy New Year.
stock-photo--apos-merry-christmas-apos-santa-claus-rings-christmas-bells-in-the-village-a-circa-2128030.jpg

Asante sana jirani......Nami niungane nawe kuwatakia Heri ya Krismas na Mwaka Mpya wadau wote wa jukwaa hili Pendwa hapa jamvini,Kila la heri na mafanikio kwa vilabu vyenu kwa mwaka 2011
 
Merry Christmas & Happy New Year kwa wadau wote wa Emirates...
 
Asante sana jirani......Nami niungane nawe kuwatakia Heri ya Krismas na Mwaka Mpya wadau wote wa jukwaa hili Pendwa hapa jamvini,Kila la heri na mafanikio kwa vilabu vyenu kwa mwaka 2011

Ahsante sana mkuu!
 
Merry Christmas wakuu wote na familia zenu,Mungu awalinde wakati huu wakusheherekea sikukuu zote.
Merry Xmas and Happy New Year 2011 wapenzi na mashabiki wote wa Arsenal😛arty:. Inshaaalah mwaka 2011,uwe wa mafanikio kwetu sote! Walau tunyakue kikombe hata kimoja.
Merry Christmas & Happy New Year kwa wadau wote wa Emirates...

54xpbars.jpg

...Thanks very much wadau wote, kila la heri kwenu nyote na familia!
Pamoja, kama kawaida!
 
54xpbars.jpg

...Thanks very much wadau wote, kila la heri kwenu nyote na familia!
Pamoja, kama kawaida!

Merry Xmas Mkuu na wadau wote wa kijiwe chetu hichi mwanana. Kwa maoni yangu mechi na Chelsea ina umuhimu mkubwa sana kama tunataka kuendelea kuwa nafasi ya kulitwaa taji la EPL. Ili kuongeza uwezekano wa kushinda mechi hiyo inabidi Fabregas, Persie na Walcott wote waanze ili kuipa pressure kubwa ngome ya Chelsea ambayo siku za karibuni imekuwa ni kichochoro. Vinginevyo yatakuwa yale yale ya Drogba & Co wawafanya vibaya Arsenal.

Msikose kijiweni kufuatilia kwa karibu kitakachojiri katika mechi hiyo.

After man Utd, Man City and T'ham's wins, May be Arsene Wenger will come with both planz A & B for the win 2mrw....Hope we will...God Bless Goonerz...God Bless my H'ness......C u 2mrw...
 
Arsenal leo ni lazima ishinde.

Ili kuweka matarajio yetu hai leo ikiwa tupo nyuma kwa 5 points na Man United wana kiporo cha mechi moja na Blackpool, Arsenal haina budi kushinda mechi hii muhimu kwani ndio utakuwa mwanzo wa msimu wa Arsenal baada ya kungojea kombe hilo kwa miaka inaenda sita sasa.

Meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti leo ataiagiza timu yake icheze mchezo wa kujilinda na kuziba maeneo yote ya uzalishaji mashambulizi kutoka kwa Andrei Arshavin, Samir Nasri na Cesc Fabregas huku wakifanya mashambulizi ya kushtukiza kwa Arsenal wakimwacha Didier Drogba peke yake mbele. Ni mbinu nzuri ambayo Chelsea walitumia kwenye mechi yake ya kwanza na Arsenal pale uwanja wa Stamford Bridge na ilifanya kazi na Arsenal wakalazwa 3-0.

Mbinu hii ya kucheza kwa kujilinda huku mchezaji mmoja akiachwa peke yake mbele pia ilitumiwa na Jose Mourinho na timu yake ya Inter Milan dhidi ya Barcelona kwenye nusu fainali ya Champions League mapema mwaka huu na Inter ikashinda na kwenda kunyakua kombe hilo la Uefa Champions League. Inter walimwacha mbele Samuel E'to na Diego Milito akimsaidia na katikati nahodha wa Inter Javier Zanetti alikuwa akihakikisha back four yake haisumbuliwi.

Kama utakuwa na "well organised back four" hata timu nzuri kuliko zote haitaweza kuwafunga na Barcelona walifungwa na Inter Milan. Ni mbinu nzuri sana ambayo inatumiwa na timu zote zinazocheza na Arsenal na timu hizo huishia kuifunga Arsenal au kutoa sare. Tayari mwaka huu West Brom waliwafunga Arsenal tena kwao na baadae Newcastle na Man United mara mbili na Arsenal wakatoa sare na Sunderland na wote huwapa Arsenal uwezo wa kumiliki mipira kwa muda mrefu walingoja kupata nafasi walau moja au mbili na kutumia nafasi hizo kuwafunga Arsenal.

Leo baadae tunaelekea Emirates kushuhudia Arsenal ikicheza mchezo uleule na "free flowing" na hii inazifanya timu kama Chelsea zisiwe na wasiwasi sana. Mbinu ya "10 men behind the ball" inaisaidia Chelsea wanakuwa na mwelekeo mmoja wa mashambulizi huku wakiwachanganya mabeki, na pia wanakuwa wanapeleka mipira mingi ya juu kwa Didier Drogba na pembeni wanawatumia mabeki wanaokwenda mbele Ashley Cole na Branislav Ivanovic.

Kwahio matokeo yoyote yale yasio ushindi kwa Arsenal basi itakuwa ni mwisho wa ndoto ya kunyakuwa kombe la ubingwa baada ya miaka sita.
 
Tusikibiane kesho mkuu
 
Arsenal na "tactical point of view" ili iifunge Chelsea au iambulie sare leo.

Kwa kuwa Robin Van Persie bado hajaiva kwa kuwa na stamina ya kutosha baada ya kukosa kucheza mechi nyingi kutokana na kuwa majeruhi mzee Wenger anaweza akaanza na Marouane Chamakh ambae anaweza kuwa anawasumbua John Terry na Ivanovic kwa kujaribu kumiliki mipira mbele ya mabeki hao wawili huku akitafuta nafasi ili awaponyoke na kwenda kufunga. Kwa mabeki wengi mshambuliaji akiwa mbele yako kila mara inakuwa rahisi kumdhibiti kuliko akiwa kila wakti anakukimbia.

Pia hali hio itawapa nafasi Jack Wilshere na Cesc Fabregas kujaza nafasi ambazo Chamakh ataziacha kwa kuwa na Terry na Ivanovic na kuwapeleka maeneo mengine.

Lakini ikiwa Wenger ataamua kuanza na Van Persie basi mshambuliaji huyo pia ni mzuri kwa kumiliki mipira huku akiangalia wachezaji wenzie akina Anderi Arshavin na Samir Nasri ambao watakuwa wakijaza nafasi ambazo mabeki wa Chelsea wataziacha watakapokuwa walimchunga Robin Van Persie.

Kwa hali hii Samir Masri ambae aliwekwa kapuni na MAn United ataweza kuibuka na kufunga magoli na ni jambo lisilo na ubishi kwamba Nasri ni mfungaji mzuri pale apatapo nafasi.

Kwa ujumla Arsenal leo inahitaji kuchagua ni mshambuliaji yupi wa kati ya Van Persie na Chamakh aanze mchezo ni hio ndio uamuzi wa muhimu.
 
walete walete haoooo.wameokolewa na balafu kupata kichapo jumapili iliopita leo hakuna kuokolewa na balafu wala nini kipigo tu.
 
Tarehe 9 February kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya timu za taifa za Portugal na Argentina mechi itakayofanyika kwenye uwanja wa Emirates pale kaskazini mwa London.

Hii itakuwa mara ya pili kwa timu hizo kukutana baada ya Argentina kucheza na Brazil na kufungwa 3-0 mwezi September 2006 na baadae February 2007, Argentina ikacheza na Portugal kwenye uwanja huohuo na kufungwa 2-0.

Kwahio kwa mara ingine tena Lionel Messi na Christiano Ronaldo watakuwa wakiwaburudisha wapenzi wa mpira uwanjani Emirates uwanja ambao mpaka sasa umekuwa mwenyeji wa mechi tano za kimataifa tangu ufunguliwe ramsi mwezi July mwaka 2006.
 
Back
Top Bottom