Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,667
- 25,698
Leo tena najaribu kuleta mtazamo wa mchezo wa timu hizi kukiwa kumesalia dakika kama arobaini hivi mchezo kuanza.
Samir ni mzuri kwenye kutumia mbinu , mwendo na muono na vitu hivi vinamfanya awe tishio lakini Ashley Cole ana nguvu na ni mwepesi na anao uwezo wa kwenda mbele na kurudi nyuma kwa kasi na mipira yake mingi ya cross huwa inamfikia Didier Drogba.
Sagna ni beki mzuri sana kwa sasa na hupenda kwenda mbele na cross zake mara nyingi huzaa matunda. Malouda ni mshambuliaji wa pembeni ambae hupenda kuwachanganya mabeki kabla ya kutoa pasi kwa washambuliaji ili wafunge na wakti mwingine hufynga magoli yeye mwenyewe.
Frank Lampard leo anarudi kwenye nafasi yake ya kiungo baada ya kukaa benchi kutokana na kuwa majeruhi. Lampard ana nguvu na ni mzuri kwa mashuti ya mbali na ni mpigaji mzuri wa mpira ya adhabu. Lampard ana uwezo wa kufungua ngome ya ulinzi na kufunga magoli huvyo kufanya kuwa mchezaji hatari sana.
Mtoto Wilshere nae amekuwa mchezaji mhimu kwa Arsenal msimu huu akisaidia pale ambapo Cesc Fabregas anapokuwa hayupo. Wilshere akikomaa alipokwenda kuchezea timu ya Bolton kwa mkopo ambapo alipigwa sana kiatu na kumfanya kuzoea mikiki ya ligi kuu.
Wilshere humsaidia Alex Song kwa kumiliki mipira na kuigawa mbele kwa Nasri na Arshavin na ana muono mzuri na utoaji wake wa pasi ni "superb"