Walianza Albion na sasa Magpies, hizi timu zote ndio zimepanda tena daraja msimu huu zinatunyanyasa nyumbani?
Na nikikumbuka misimu ya nyuma akina Hull City nao walikuja Emirates na kuondoka na ushindi, hakuna heshima tena , sio intimidated ground kama ilivokuwa Highbury, Westham nao chupuchupu wajiondokee na pointi!!
Wenger na arudie formula ile ya zamani ambayo ilitupatia mafanikio,na turudie kusajili Wanaume, hivi vitoto havitoshinda kombe (labda Carling) tunahitaji wapiganaji kama walivokuwa The Invincible,akina Gilberto, Pires, Vieira, Ljunberg, Campbell, Parlour,Keown wote ni wapiganaji ambao kama ni urembo wanaweza na ukitaka vita poa vilevile, nakumbuka ile mechi Old Trafford Van Nistelrooy v Keown, Vieira v Keane, aah masikini timu yetu, eti akina Andy Caroll, Tiote na Ameobi wanakuja Emirates na kuweka authority?