Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

i hope next game tutamaliza shughuli.
Natumai itakuwa hivo, inakera sana kufungwa kizembe namna ile, wachezaji wetu walicheza kama vile ni mazoezi na zaidi Clichy imekuwa ni tabia yake kufanya uzembe, bahati mbaya Gibbs nae haishi majeruhi ila inafaa huyu Clichy apate challenge kwenye hii position.
Kutokuwepo Song ama Denilson pale kati kulifanya tukose defensive cover kwa Djourou na Squillaci kwani dogo Eastmond bado hajamudu mechi kubwa.
 
Haya Jumapili ni Newcastle, kila nikiona hii fixture namkumbuka Dennis Bergkamp The LEGEND!! hebu tujikumbushe, bao hili kwangu mimi ni Namba 1 kwa ubora katika magoli bora ya Arsenal, kutokana na 'technique and execution' sambamba na goli lile la Kanu dhidi ya Chelsea.
Si vibaya tukijikumbusha:


 
Last edited by a moderator:
Nadhani Wenger anaapaswa kujifunza kutokana na makosa anayoyarudia mara kwa mara katika kikosi chake!
 
Tuko pamoja wakuu kila la kheri.

list ni fabianski,sagna,squallaci,koscienly,clichy,wilshere,fabregas,song,nasri,walcott na chamakh.
 
Hii mechi ya leo tukiikosa basi imekula kwetu katika safari ya kusonga kwenye kilele, manake jamaa wanashinda kweli mechi zao!
 
Ingekuwa Bongo, hilo lango la Newcastle tungeenda kuchimba tucheki kama kuna mitishamba!
 
Back
Top Bottom