Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Wapiga bunduki walio geuka warusha mishale!

Ndugu yangu rubaman na Wacha1 hamna haja ya kusononeka wala kutukimbia hapa!Ndiyo soka kaka

Nilikuwa nawajibika mchana kutwa, unajua mambo ya huku yalivyo. Sikuweza kuangalia mechi zaidi ya kufuatilia online. Matokeo mabaya sana haya. Arsenal tuna gundu fulani katika CL, hadi litakaposafishwa ndo tutaweza kufanya vizuri.
 
Kama leo tungekua tunacheza na Barca au Bayern, jamaa wangecheza mpira wa kueleweka. Ni wazi kuwa jamaa walibweteka baada tu ya kuona kuwa tunacheza na Monaco, kwenye vichwa vyao walikua wanajua piga ua lazima washinde! Inawezekana kusonga mbele japo itakua ngumu sana if am being honest and realistic, tusubiri tuone.
 
rubaman nilikuambia lakini

Nilisema watu waliokuwa wanafurahia kupangiwa na Monaco ni wale wasiojua kitu. Anyway, ndo mambo ya soka mkuu. CL mtoano timu yoyote inaweza kuiondoa timu yoyote. Ingawaje ni kibarua kigumu tulichonacho mechi ya marudiano bado tunaweza kushinda kama tulivyowapiga Inter kwao 5-1. Nafasi ni finyu sana.
 
Weee! Umenichekesha sana.
Hao wanaojua,wanaozungumza na kuelewa kiingereza walikisahau leo? :lol::lol:
Au walisahau kuwasiliana?
 
Nimeona tumepigwa na counter attacks. Tulikuwa exposed kama vs Antwerp. na vs Stoke. Tunatakiwa kurekebisha huu upuuzi. Hongera kwa wapenzi wa Manchester United, Liverpool kwa ushindi na kuweza kuangalia Champions League maana mnaimiss(hasa Man United) na mtaimiss msimu ujao. Viva Arsenal. We will bounce back. Remember that.
Cc Nzi, DonDonald, Malafyale
 
Mi naona kabisa tukienda na kupata matokeo. Ni babu akubali vitu vichache kuvibadili ktk mfumo.

Matokeo mazuri mna zungumzia CL ya mwakani?

Mwaka huu mmeisha tolewa bana acheni kujipa matumaini hewa
 
Kabisa Mkuu nasi tunaweza kabisa kuwafunga kwao ila ningependa kuona mstari wa mashambulizi Walcott anaanza badala ya Ozil ambaye mara nyingi hupunguza speed ya mashambulizi. Inawezekana kabisa kwenda mapumziko tukiwa juu 2-0 au hata 3-0. Let's keep our fingers crossed for a surprise results.

CC: everlenk


.......there's a way! Keep the faith bro.
Kama wao wameweza, sie kitatushinda nini?.....
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu
Labda katika ulimwengu wa maajabu, there's no way we gonna come back from 3-1 to beat them 3-0 in France...No way!

Kwa Arsenal hii wakienda Monaco hata sare hawapati

Hawa wameisha tolewa wajiandae tu na Europa League yao maana kikosi chao hiki hawawezi qualify CL mwakani
 
Reactions: Nzi

Arsenal hawana historia ya kubadili matokeo ya kiwango hicho. Ingekuwa chelsea tungesema tusubiri tuone. Lakini kwa Arsenal ndo imetoka hiyo! Waendelee tu kufukuzia malengo yao ya kila mwaka ya kubakia top 4.
 

Tatizo ni kuwa huwa mnaangalia ligi ya Uingereza tu hivyo hamjui current form ya timu kwenye ligi nyingine. Hawakubeza hata kidogo sema kiwango bado sana. Kiwango cha Arsenal kinaishia kugombea kubakia top 4 ya EPL.
 
The last team to advance to the QF after losing 2+ goals at home, was Ajax FC in 1969 😎😎😎

Duh mkuu umesahau hao Asernal kama sikosei ilikuwa 2004/2005 walipigwa 3 bila na Inter walivyoenda kule Inter akapigwa 5-1.
1969 Mbali sana.
 
Reactions: Mbu
Duh mkuu umesahau hao Asernal kama sikosei ilikuwa 2004/2005 walipigwa 3 bila na Inter walivyoenda kule Inter akapigwa 5-1.
1969 Mbali sana.


Mzee ni 2003-2004 Arsenal alifungwa e bila Highbury na Inter , walivyokwenda San Siro wakashinda 5 - 1. Lakini ilikua ni katika group stages na Arsenal ilikua lazima ishinde.
 
Reactions: Nzi
Makosa yetu wenyewe yametugarimu, ila uwezekano wakuwafunga 3-0 kwao upo, Monaco sio timu yakututoa sisi kwenye mashindano haya
 
Hii timu majanga...yaani mpira tucheze sisi na kumiliki sisi alafu tunafungwa sisi. Inasikitisha sana

Jana nilikwambia lkn pale mbele kuna tatizo, si jambo la kawaida kuwa na engine kama zile alafu unapoteza game nyepec kama ile.
 
Arsenal hawana historia ya kubadili matokeo ya kiwango hicho. Ingekuwa chelsea tungesema tusubiri tuone. Lakini kwa Arsenal ndo imetoka hiyo! Waendelee tu kufukuzia malengo yao ya kila mwaka ya kubakia top 4.

Bila kusahau kombe lao la FA
 
Tulifungwa kwa bahati mbaya,Arsenal hatuna bahati mwaka huu.
 

hahaha! na wanashika nafasi ya nne ili wacheze mechi za awali waingize fedha. usisahau kwamba wenga ni profesa wa uchumi na ni mmoja wa wakurugenzi wa aseno. money matters more than silvawares. hii ndio FALSAFA ya aseno tangu zamani. kila mwaka wanatengeneza FAIDA ya kumwaga.
 
Reactions: Nzi
Ningeshangaa kuona ngoma ya watoto inakesha leo!!!!! Acha wagongwe ili waelekeze nguvu zao kupigania top 4....,.....ha ha ha ha ha ha

exactly! huu ndio ukweli mkuu. bora warudi wakaitafute top 4 vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…