Kwa kumsajili Gustavo, Wenger anathibitisha kwamba amenuia kuunda upya timu ya Arsenal.
Ni miaka nane imepita tangu Arsenal wanyakue kombe la ubingwa wa Uingereza mwaka 2004 baada ya kwenda msimu mzima bila kupoteza mechi hata moja.
Lakini mwaka ule uliona timu ya Arsenal iliyoundwa na kipa Jens Lehmann, Lauren, Kolo Toure, Ashley Cole na Sol Campbell, katikati kulikuwa na Gilberto Silva, Patrick Vieira, Ray Parlour na Robert Pires na mbele kulikuwa na Denis Bergkamp na Thiery Henry, na hii ndio ilikuwa first XI ya Arsenal.
Arsenal ilianza na ushindi katika mechi nne za kwanza na kwenye mechi ya nane dhidi ya Manchester United kidogo Ruud Van Nistelrooy atufunge kama angekwamisha mpira kimiani baada ya Man Utd kupewa penalty na badala yake akapaisha juu ya mwamba.
Baada ya hapo Arsenal ikawa inatoa vichapo nyumbani na ugenini na timu hii ilikuwa ni timu ngumu kuikabili na ilikuwa na mtindo wa kuvutia wa uchezaji hususan kwa akina Bergkamp na Henry.
Meneja Arsene Wenger alikuwa ameunda timu imara kwenye ulinzi wa Ashley Cole, Lauren Koro Toure na Sol Campbell na hawa wote walikuwa wakilindwa na Gilberto Silva katikati ambae alikuwa kigawa mipira kwa ama Patrick Vieira au Robert Pires ambao ama waliamua kwenda mbele kufunga au waliwapa Bergkamp na Thiery Henry wamalizie kazi, ailikuwa ni burudani wakati huo.
Msimu ujao wa 2013-2014 unaanza Jumamosi ijayo na Arsenal wanaanza ligi kwa kucheza nyumbani Emirates na wanawakaribisha Aston Villa timu ya kutoka sehemu ijulikanayo kama "The Midlands" ambayo inajumuisha mikoa mbalimbali ikiwemo Derby, Coventry na Birmignham.
Zikiwa zimebakia siku 20 kwa dirisha la usajili kufungwa Arsenal mpaka sasa imemsajili mchezaji Yaya Sanogo kutoka Auxere ya France na ambae hakulipiwa gharama yoyote le kwani mkataba wake na timu hiyo uliisha wenyewe.
Mpaka kufikia leo ni habari kwamba Luiz Gustavo anazungumza na Arsenal na huenda akacheza siku ya Jumamposi ikiwa masuala yote ya mkataba na makubaliano mengine yatakamilika kufikia kesho jioni.
Luiz Suarez bado suala lake lina mgogoro ikizingatiwa kwamba Liverpool hawataki kumuuza kwa Arsenal eti kwasababu wao ni mahasimu wetu katika msimu wa 2013 na wanataka kufuzu kucheza ligi ya mabingwa wa Ulaya mwakani kwa kushika moja ya nafasi nne za juu kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Lakini napenda kuzungumzia ujio wa Luiz Gustavo na nafasi ya Mikael Arteta kwenye timu ya Arsenal mwaka huu.
Arteta ana umri wa miaka 31 na sasa inafikiriwa ni kwa jinsi gani uongozi wake kwenye sehemu ya kiungo utarithiwa na Aaron Ramsey na Jack Wilshere.
Arteta na Ramsey wameonyesha uimara kwa kiasi kikubwa hasa katika mechi 10 za mwisho katika mismu wa 2012-2013 na wamefanya hivyo huku wakiwa wanapanda kwenda kushambulia mbele. Lakini kupatikana kwa DM wa aina ya Luiz Gustavo kunaweza kumfanya Arteta apunguziwe majukumu yake na Wenger kuamua kuwacheza Gustavo na Ramsey kwenye sehemu ya kiungo na kumuachia Jack Wilshere awe anapanda kwenda kushambulia.
Mara nyingi Ramsey, Arteta na Wilshere wamekuwa wakienda mbele kushambulia na kuacha nafasi kati ya mabeki na kiungo au kukaa nyuma sana na kuweka nafasi kati yao na washambuliaji na kusababisha wachezaji wa timu pinzani kutawala sehemu hiyo.
Hii ilionekana kwenye mechi na Tottenham ambapo Gareth Bale alitawala nchezo na kutufunga na baadae kumpatia pande Aaron Lennon ambae alifunga goli la pili kirahisi. Lakini tokea mechi ile na mechi thidi ya Bayern Munich, wachezaji hawa wamegundua makosa yao mengi tu na wameelewa na nini kinahitajika kufanyika.
Suala hili limekuwa likisumbua katika kutafuta suluhisho la kwamba Wilshere awe anaruhusiwa kwenda mbele huku Arteta na Ramsey wakiwa wanashughulika na ulinzi wa mabeki wao huku nao wakijaribu kusaidia mashambulizi.
Lakini kuja kwa Luiz Gustavo kama kunavyotarajiwa kutaondoa majukumu mengi ya Arteta na Ramsey na hivyo kuweka mfumo mmoja wa 4-3-3 ambao kiuchezaji unageuka kuwa wa 4-1-2-2-1 ambapo Gustavo anakuwa mbele ya mabeki wanne, Ramsey na Wilshere wakiangalia sehemu ya kiungo na huku Santiago Cazorla Theo Walcott walishughulika na kutafuta vyumba na magoli.
Lakini katika wazo hili hakuna nia mbaya ya kumpuzisha kabisa Mikael Arteta kwani amekuwa kiongozi na msimazi mzuri wa Aaron ramsey ambae sasa anajua kuzuia mipira mingi ya pasi ndefu (interceptions) kutoa pasi na kukabili wachezaji wa timu pinzani (tackles).
Lakini Le Proffesor Wenger anafahamu namna atakavyopanga timu yake bila kuathiri nafasi ya Mikael Arteta ambae amekuwa mchezaji muhimu sana kwetu.
COYG!!!!!