- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Baada ya Afrika, bara la Amerika Kusini ndilo lenye watu weusi wengi zaidi wakikadiriwa kuwa zaidi ya milioni 170 huku Brazil ikiongoza ikiwa na watu weusi takriban milioni 120.
Nchi ya Argentina inatajwa kuwa mpaka sasa watu weusi ni chini ya laki mbili wakiwa takriban asilimia 0.5% kutoka asilimia 48% miaka ya 1800.
Inadaiwa watu weusi baada ya kuisaidia Argentina kupigana vita na maadui zake, watu weusi waliosalia waliwekwa kwenye maeneo maalumu ambayo kwa kipindi hicho kulikuwa na ugonjwa wa hatari unaosababishwa na bacteria “Plague” ambapo serikali iliwanyimwa huduma muhimu hivyo upelekea vifo vyao.
Zitto kupitia ukurasa wake wa Twiiter aliwahi kumhoji jamaa kuhusu kuishabikia Argentina, nanukuu 'Una support argentina ambayo iliua Watu weusi wote Lakini unapinga Morocco kwa kiwango cha SGR! Spain colonised Sahrawi and irresponsibly left. Morocco did a good job defeating them.'
Pia, wadau wengine wamehoji inakuwaje timu ya Taifa ya Mpira wa miguu iliyochukua kombe la dunia 2022 ikakosa mchezaji hata mmoja mweusi? Hii ikahitimisha kuwa Argentina kweli waliua na kupoteza kizazi cha watu weusi ili kulinda kizazi chao.
Pia nasikia waafrika pekee waliothaminiwa ni waafrika weupe lakini kwa kupewa masharti mazito ya kuendeleza vizazi vyao na waargentina asilia weupe. Kwa case hii tunaweza kumtazama mchezaji aliyepata kukipiga Vilabu vya Manchester United, Inter Milan na timu ya taifa Argentina anayejulikana kama Juan Sebastian Veron ambaye hakuwa mzungu asilimia 100.
Kikosi cha Timu ya Taifa Argentina kilichotwaa kombe la Dunia 2022
Nchi ya Argentina inatajwa kuwa mpaka sasa watu weusi ni chini ya laki mbili wakiwa takriban asilimia 0.5% kutoka asilimia 48% miaka ya 1800.
Inadaiwa watu weusi baada ya kuisaidia Argentina kupigana vita na maadui zake, watu weusi waliosalia waliwekwa kwenye maeneo maalumu ambayo kwa kipindi hicho kulikuwa na ugonjwa wa hatari unaosababishwa na bacteria “Plague” ambapo serikali iliwanyimwa huduma muhimu hivyo upelekea vifo vyao.
Zitto kupitia ukurasa wake wa Twiiter aliwahi kumhoji jamaa kuhusu kuishabikia Argentina, nanukuu 'Una support argentina ambayo iliua Watu weusi wote Lakini unapinga Morocco kwa kiwango cha SGR! Spain colonised Sahrawi and irresponsibly left. Morocco did a good job defeating them.'
Pia, wadau wengine wamehoji inakuwaje timu ya Taifa ya Mpira wa miguu iliyochukua kombe la dunia 2022 ikakosa mchezaji hata mmoja mweusi? Hii ikahitimisha kuwa Argentina kweli waliua na kupoteza kizazi cha watu weusi ili kulinda kizazi chao.
Pia nasikia waafrika pekee waliothaminiwa ni waafrika weupe lakini kwa kupewa masharti mazito ya kuendeleza vizazi vyao na waargentina asilia weupe. Kwa case hii tunaweza kumtazama mchezaji aliyepata kukipiga Vilabu vya Manchester United, Inter Milan na timu ya taifa Argentina anayejulikana kama Juan Sebastian Veron ambaye hakuwa mzungu asilimia 100.
Kikosi cha Timu ya Taifa Argentina kilichotwaa kombe la Dunia 2022
- Tunachokijua
- Argentina ni miongoni mwa mataifa makubwa na mashuhuri Barani Amerika ya Kusini. Licha ya kuwa na historia na mambo mengi Taifa la Argentina linajulikana zaidi duniani kisoka kutokana na kutoa wanamichezo mashuhuri na maarufu kama Diego Maradona na Lionel Messi.
Pamoja na upande huu mzuri wa Argentia kumekuwapo na hoja na maswali ya watu mbalimbali duniani kuhusu uwapo wa watu weusi katika taifa hilo. Hoja hii imekuwapo miaka mingi iliyopita lakini Barani Afrika hoja hii imeanza kushika kasi mwaka 2022 baada ya taifa hilo kufikia fainali ya kumbe la dunia na kuwa na wafuasi wengi tokea Afrika.
Watu wengi ikiwamo Mwanachama wa JamiiForums kama Black Movement waliibuka kuhoji Waafrika wanaoshabikia timu hiyo ikiwa imewahi kuwatendea mabaya watu weusi. Hoja hii pia imewahi kutolewa na Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter huku yeye akiona ni bora zaidi Waafrika kuiunga mkoni timu ya taifa Morocco kuliko Argentina kutokana na kuwahi kuwaangamiza watu weusi.
Je, Argentina iliua kizazi cha watu weusi ili kulinda watu weupe?
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali vya kihistoria ili kujua nini kipo nyuma kati ya taifa la Argentina na watu weusi kama Ifuatavyo:
Mnamo mwaka 2002 Chuo Kikuu cha Grand Valley nchini Marekani kilichapisha jarida lililoitwa
The Disappearance of the Black Community in Buenos Aires, Argentina, 1850-1890 lililoeleza namna kizazi cha watu weusi kilivyopotea nchi Argentina. Jarida hili linaeleza kuwa Vita na Magonjwa zilikuwa ni miongoni mwa sababu kubwa zilizopelekea kizazi cha watu weusi kupungua katika nchi hiyo.
Zaidi ya hiyo Makala inadokeza Nadharia ya Kijamii ya Darwin inayoeleza kukosekana kwa uwiano baina ya Wanawake na wanaume weusi baada ya vita vya uhuru. Nadharia hii inaeleza kuwa wanaume wengi weusi walikufa wakati wa vita hivyo baada ya vita kulikuwa hakuna uwiano kati ya wanaume na wanawake weusi. Hivyo, wakashindwa kuzaliana na hatimaye kumezwa na watu weupe. Sehemu ya jarida hilo inaeleza:
Ukipita kwenye mitaa ya Argentina, mtu anaweza kushuku kwamba hakuna watu weusi kati ya wakaazi wa mji huo. Ingawa jamii ya watu weusi haipo sana katika Argentina ya leo, historia inasimulia hadithi tofauti. Kuanzia mwaka 1535 na kuendelea katika karne nne zilizofuata, watumwa waliletwa Buenos Aires. Wakati Argentina ilipopata uhuru wake mwaka 1810, watu weusi walichangia idadi kubwa ya watu katika Buenos Aires na walisaidia kuchangia densi yao inayojulikana kama candombe, dini, na fasihi katika utamaduni tajiri wa nchi hiyo. Hata hivyo, kuanzia miaka 1850 hadi 1890, idadi ya watu weusi ilipungua kwa kiasi kikubwa na jamii ya watu weusi ilipotea kabisa. Vita na magonjwa vilisababisha kupungua kwa idadi ya watu weusi, huku uhamiaji wa Ulaya, nadharia ya Darwin ya kijamii, na kuchanganyika kwa watu wa rangi tofauti vikisababisha kupotea kwa jamii ya watu weusi mpaka ikawa haipo tena Buenos Aires.
Naye Prof. Sylvain B. Poosson mtaalamu wa masuala ya tamaduni na historia ameandika makala inayoitwa The Expression of Blacks in 19th Century in Argentina mwaka 2004 ambayo anaelezea namna Argentina ilivyojaribu kuteketeza historia ya watu weusi licha ya mchango wao mkubwa katika kulijenga taifa lao katika karne ya 19. Katika makala hayo Prof. Sylvain B. Poosson anaeleza kuwa watu weusi nchini Argentina walipata wakati mgumu wakati wa utawala wa Rais Domingo Faustino Sermiento kuanzia mwaka 1864 mpaka 1874.
Inaelezwa kuwa Rais huyo alifaya jitihada za kuteketeza kizazi cha watu weusi nchini Argentina kwa kuhakikisha wanapata wakati mgumu ikiwamo kuwekwa seheu zenye maambukizi ya magonjwa hatari na kunyimwa huduma za afya.
Sehemu ya makala hayo Prof. Sylvain B. Poosson anaeleza:
Unapoitazama historia ya Taifa la Argentina katika Karne ya 19 inashangaza kwa sababu sio Kila aliyehusika kupigania kulijenga Taifa Hilo alipewa umuhimu. Domingo Faustino Sermiento Aliyekuwa Rais kuanzia mwaka 1864 mpaka 1874 aliyefanya jitihada nyingi kuwaangamiza watu weusi. Aidha, inadaiwa rais huyo amewahi kusema kama una mtu anawapenda watu hao basi aende kuwaona nchini Brazil. Hata hivyo Prof. Sylvain B. Poosson anakiri kuwa pamoja na jitihada zote kutekeleza watu kizazi cha watu weusi bado Argentina haijaweza kufuta mchango wa watu weusi katika kujenga taifa lao.
Makala haya ya Prof. Sylvain B. Poosson yanasaidia kutupa mwanga kuona kuwa kuna jitihada zimeshawahi kufanyika katika taifa la Agentina katika kuteketeza kizazi cha watu weusi.
Aidha, Mnano mwaka Desemba 18, 2022 siku ya Fainali ya Kombe la Dunia kati ya Argentina na Ufaransa Mdau wa michezo Zakazakazi aliibuka na hoja kuwakosoa watu weusi wanaoiunga mkono timu ya taifa ya Argentina kwa kueleza historia ya namna taifa hilo lilivyowafanyia ubaya watu weusi. Katika andiko lake Zakazakazi anaeleza:
Argentina kama zilivyokuwa nchi zote za Amerika, Kusini na Kaskazini, yalikuwa mashamba ya mataifa makubwa ya Ulaya. Mashamba haya yalihitaji nguvu kazi ambayo haikuwepo huko, ndipo biashara ya utumwa iliposhamiri kwa kuchukuliwa watu kutoka Afrika na kupelekwa huko.Mataifa yote ya Amerika, Kusini na Kaskazini, yana idadi kubwa sana ya watu weusi walioenda kule kama watumwa na vizazi vyao kubaki huko baada ya utumwa kupigwa marufuku. Vizazi vyao viliendelea kubaki huko na kuwa sehemu ya jamii na kushiriki mambo yote ya kijamii ikiwemo michezo.Na hata kwenye timu zao taifa kuna wachezaji weusi. Ni nchi moja tu, Argentina, ambayo haikutaka kubaki na watu weusi. Baada ya utumwa kupigwa marufuku nchini humo mwaka 1813, harakati zilianza mara moja kuangamiza watu weusi wote.Harakati hizo zilienda mbali zaidi kwa serikali kuagiza watu weupe kutoka Ulaya, Hispania na Italia, ili wahamie nchini humo kuitakasa nchi hiyo iwe ya weupe watupu.Rais wa Argentina wa wakati huo, Domingo Faustino Sarmiento, aliapa kwamba anataka kuwamaliza watu weusi wote nchini humo baada ya miaka 20. Akasema, 'tukiwa na hamu ya kuwaona watu weusi basi tutaenda Brazil maana wao wanawapenda sana'.Kikawekwa kipengele kwenye katiba ya nchi hiyo kinachoitangaza Argentina kama taifa la watu weupe kutoka Ulaya waliokuja na meli. Watu weusi walitungiwa sheria ngumu za kuishi ikiwemo kukosa huduma zote za kijamii ikiwemo afya.Magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu na tauni yakawaandama na kuwaua kwa kiasi kikubwa sana. Ikatokea vita na serikali ikawachukua watu weusi ambao hawakuwa na mafunzo ya kiaskari na kuwaeeka mstari wa mbele kama chambo. Maelfu kwa maelfu walikufa vitani.Kutokana na sheria hizi ngumu, wengine wakakimbilia mataifa jirani kama Brazil ambayo angalau yaliwajali watu weusi. Hii ndiyo sababu hakuna wachezaji weusi kwenye timu ya taifa ya Argentina.Ufafanuzi huo wa Zakazakazi hautofautiani na ufafanuzi uliotolewa na Prof. Sylvain B. Poosson. Melezo yao yanatupa hitimisho taifa la Argentina lilifanya jitihada za makusudi kufuta historia ya watu weusi katika nchi yao.
Kimsingi, vyanzo vingi vinakubali kwamba mnamo karne ya 16 wakati wa biashara ya utumwa Argentina ilikuwa na watu weusi waliozidi asilimia 30 ya wakazi wote wa eneo hilo wakija kama Watumwa. Vyanzo hivyo pia havitofautiani sana kuona ilikuwapo jitihada kubwa za kuwaondoa watu weusi wakati wa utawala wa Rais Domingo Faustino Sermiento mwaka 1864 mpaka 1874.
Hivyo, kutokana na mapitio mbalimbali na ufafanuzi uliotolewa na wanahistoria na majarida ya vyuoni, inawezekna kuwa hoja ya Argentina kufanya jitihada kuwaondoa watu weusi katika taifa lao inaweza kuwa na ukweli.