Ufaransa kujaza watu weusi kwenye timu ya taifa ni kuendeleza utumwa

Sella turcica

Senior Member
Oct 13, 2020
104
193
Kwanza kabisa nimefurahi Messi kuchukua kombe la dunia. Isingekuwa haki kama huyu mwamba angestaafu bila kuchukua hii ndoo. Poleni timu Ronaldo, mimi nafurahi nikiona mnaumia.

Niende kwenye mada husika. Timu ya Ufaransa imejaa wachezaji wa Africa. Nimeona waafrica wengi wakiishabikia Ufaransa kwa sababu imejaza watu weusi. Mimi naona huo ni utumwa. Hawa jamaa weusi wanaochezea Ufaransa na mataifa mengine ya Ulaya hawana haki sawa na wazungu. Wana uraia sawa but they are second class citizens. Watawatumia tu kuwaburudisha lakini hawatakaa washike positions muhimu kwenye nchi kama mambo ya kibenki, mahakama, wala kumiliki nyenzo za kiuchumi. Kule jamaa wanadharauliwa. Kuna likizo moja Pogba alitembelea nchi moja ya Africa, siikumbuki jina, watu walikuwa wanamshangilia yani akajihisi kama ambavyo Messi anajihisi akiwa Argentina. Wazungu hawana shobo na watu weusi, juzi watu wamevamia nyumba ya Sterling. Aubameyang naye alivamiwa kule Barcelona.

Mahitaji ya binadamu sio pesa tu, kuna kuthaminiwa utu pamoja na heshima. Africa ingefika mbali kisoka kama wachezaji weusi wangechezea timu zao za asili. Wangepata mafanikio na kuimbwa kama mashujaa wa mataifa yao. Eti Bukayo Saka ni mwingereza😀😀😀.

Africa tuache rushwa na ukiritimba. Waafrica wengi wanakimbia matatizo huku kwao na kuzamia ulaya walau wapate ugali. Kule wanahangaika na kutupiwa mfupa wa kuchezea timu za taifa za wazungu. Ukoloni unaendelea sema kwa sura nyingine. Babu zetu walitumikishwa mashambani, viwandani na majumbani, wajukuu zao wanatumikishwa uwanjani.
Waafrika tusiposolve matatizo yetu wenyewe na kupafanya pawe mahali pazuri basi tutaendelea kutawaliwa na hao jamaa hadi tunaingia kaburini.
 
Pumba.

Unaongea bila kijisikiliza. Wewe unaeshabikia Argentina ndio mbwanyenye?

Kama historia ulikariri ishia hapohapo.

Mataifa yaliyotawaliwa na Ufaransa mnalingana nayo kiuchumi au hata kiutamaduni.

Walau Kongo hapo, wabongo mmejaa mnatafuta ugali, shukuru wakongomani wanawapenda wabongo
Tuachanenna Hilo.

Wachezaji wakiafrika unaozungumzia wako utumwani wanafanyakaz na hiyo ndiyo ajira yao. Wanapata pesa hilo ndio Lengo lao.
 
Wanacheza Bure?

Akili ya mwafrika ni shida,
Waache wachezaji wa Ufaransa kulalamika sio shida zao
 
Naona mnanishambulia badala ya kupinga hoja kwa hoja. Sikatai kwenda kucheza ulaya kutafuta pesa, ila kuchezea timu za mataifa ya ulaya huku wao wakiwa na asili ya Africa ni form nyingine ya utumwa. Waisrael hata wakae miaka mingapi kwenye nchi nyingine, bado watabaki kuwa wayahudi. Pingeni kwa hoja na sio matusi.
 
Hao wa-argentina unaowashabikia unajua walichowafanya watu weusi huko Argentina?!

"Tusichokijua"
 
Unajua maana ya utumwa? Utumwa emz za ukolon unafananisha na utumwa wa sasa?
Leo mbape, pogba,mane, salah n.k wanagombaniwa kwa dau kubwa na wazungu, bado unaita utumwa, wale watumwa wa kipindi kile waligombaniwa kwa hii expensive?
Wale wanatafuta kula yao tena ina thaman kuliko huku kwetu, tuwaheshim ni nafasi chache kama zile kutokea
 
Sikatai kuchezea clubs za ulaya, nazungumzia kuchezea timu za mataifa ya Ulaya.
 
Naona mnanishambulia badala ya kupinga hoja kwa hoja. Sikatai kwenda kucheza ulaya kutafuta pesa, ila kuchezea timu za mataifa ya ulaya huku wao wakiwa na asili ya Africa ni form nyingine ya utumwa. Waisrael hata wakae miaka mingapi kwenye nchi nyingine, bado watabaki kuwa wayahudi. Pingeni kwa hoja na sio matusi.
Kwa hiyo wewe shughuri zako zote za kimaendeleo unafanya katika eneo lilipo chimbuko la ukoo au kabila lako. Think bigger man.
 
Back
Top Bottom