Kuna Radar, Ndege, Richmond, EPA, na mengine mengi tu hata ya kudumaza opposition yamefanyika under the watch of Mwang'onda, na Mengine under the watch of RO.
Cha muhimu ni kuoverhaul TISS yote, iendenane na wakati, ifanye kazi ya usalama wa Taifa...isifanye kazi ya kukilinda chama au kuwalinda watu, au maslahi ya watu hili ndio la msingi kwa sasa. Kuna mengine mengi ambayo insiders wa TISS wanamwaga hapa yanaonesha kuwa TISS ina tatizo.
Hapo umenena. Reform ya hali ya juu inahitajika kwenye Security and Law Enforcement sector! kwenye dunia ya sasa ya utandawazi lingekuwa jambo jema kuigawanya TISS kwenye idara mbili tofauti.
1. Idara itakayo-deal na Security, espionage and intelligence gathering; hapa depts nyingi zilizoko TISS kwa sasa zihamie kwenye taasisi hii mpya,
2. Criminal Investigative Service, hii iwe independent isihusishwe na jeshi la polisi, na iwe chini ya wizara ya sheria, ifaye kazi bega kwa bega na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
3. Jeshi la Polisi livunjwe, nafasi ya Mkuu wa Polisi iondolewe.. badala yake baadhi ya idara zenye umuhimu zijumuishwe kwenye idara mpya iliyotajwa hapo juu (no 2), na kazi nyingine zote za polisi ziwe local. Maana kazi kubwa ya polisi ni kulinda maisha na mali za watu, ku-enforce Sheria,, Criminal investigations( especially domestic) , ku-regulate traffic, na public safety. ( Cha ajabu utakuta polisi hajui hata kuendesha gari).
Pia kuwepo na juridisction kati ya Idara mpya itakayoundwa na Regional Polices.
Idara ya Manumba inaweza kugawanywa btn regional Polices na idara mpya (no 2 hapo juu)
Muundo wa sasa wa Taasisi zetu za Ulinzi na Usalama umengeneza kundi la untouchables, kitu ambacho si kizuri kwa nchi ya Kidemokrasia.
Haya yote yanawezekana kwa sababu sisi raia ndio tunaotunga sheria kupitia wawakilishi wetu bungeni , maana kazi kubwa ya Bunge ni ku-
make Rules for the Government.Rais (Executive Branch) ni mtekelezaji na Mahakama (Judiciary) ni Mtafsiri wa Sheria hizo.
Idara zote zilizobakia zimebakiwa na kazi moja tu, ku-enforce sheria na taratibu tulizojiwekea
. So kama tunataka mabadiliko inabidi tuwakabe akina Zitto, wanapokuwa Bungeni waache U-CCM, u-CUF na u-Chadema instead at least waunde non-partisan gangs wa-introduce miswada yenye kuleta mabadiliko!
Hakuna kitu kinachoshindikana kama tukiamua kufanya mabadiliko!