App/Software ya kuonyesha matokeo Bongo (NECTA)

Samedi Amba

JF-Expert Member
Nov 13, 2018
227
178
Habari wanajamvi,

Natumaini tunaendelea vizuri.

Kila mwaka sisi hutarajia matokeo ya mitihani. Hata kama sio ya kwako, mtoto/ shangazi/ mpwa/ mke/ mme nk wanahusika.

Naomba kujua kama kuna apps au systems au SMS shortcodes nk ambazo zimerahisisha hili, kiasi kwamba sina haja ya kwenda kwenye site ya NECTA kutafuta.

Vijijini wanateseka sana. Huwa wanatupigia kuomba tutafute. Ndo uende weee link baada ya nyingine.

Nafikiria kutengeneza kitu, ila nahofia inaweza kuwa tayari ipo sokoni.
 
Unaweza tengeneza app ama hata web wrapper ya hayo matokeo, ila sidhani kama itasaidia ikiwa servers ni zile zile za Necta.

Sijui sheria zinasemaje ila kinachohitajika ni backup server ama 3rd party server ambayo itapunguza load, hapa ukiwa na uhakika na server hata app si tatizo.
 
Hizo ni takwimu mjomba, mwenye mamlaka wa kuzitoa na kuzisambaza ni NECTA, sheria ya takwimu itakubana. Labda ukaongee nao muingie ubia ila huwa hawatoi ushirikiano.

Kiufupi utasumbuka sana, ila penye nia labda kuna njia ila njia iliyojaa miiba na vizuizi vingi sana.
 
Asante kwa kuwa muwazi. Since huwa wanapublish content, ntajua cha kufanya...

Back
Top Bottom