Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,930
Sikutegemea huyu mama kusema maneno haya kwa wakati huu, hasa akiwa amechaguliwa kama speaker wa bunge. Hili linanipa shaka katika ufanisi wake wa kazi, kwani ameanza vibaya kwa kutumia siasa za maji taka.Kwa kweli kuchaguliwa kwa huyu mama ni maafa kwa taifa. Anakana kuwekwa na mafisadi wakati huohuo anasema yeye hajui kama kuna mafisadi kwani kwa ufahamu wake fisadi ni mwanaume anayeiba mke wa mtu (nukuu ya gazeti la Mwananchi la leo). Tanzania ya leo tunahitaji Spika mwenye ufahamu wa kiwango cha chini kiasi hicho?
Wote tunajua kuwa suala la kuongelea kuhusu 'wizi wa mke wa mtu' ni nini na linamlenga nani. Ni maji taka hayohayo ambayo yalitumiwa na viongozi wa ccm dhidi ya Dr. Slaa wakati wa kampeni za uchaguzi. Kwa hili tunaweza kusema kwel kama atafanya kazi yake vizuri? Leo hii hakuna haja ya kutafuta maana ya neno 'fisadi'. Kila mtu anajua hata mtoto wa darasa la 3 anajua.
Kwa kutamka hivyo hadharani, ameuhakikishia umma wa Kitanzania kuwa amewekwa pale kuetetea hoja za mafisadi, hakuna mjadala zaidi. Kama yeye alikuwa halijui hilo, basi imeliwa kwake!