Nitajibu maswali mawili hapa.
Nimefanya kazi na Anna Wilson Makinda miaka ya 1980s, namjua kidogo. Nimewahi kufika kwao wakati baba yake alikuwa hai, na pia mara moja baada ya baba yake kufariki miaka ya 1990s. Baba yake aliwahi kuwa mkuu wa mikoa kadhaa, nakumbuka Tabora, Ruvuma, Tanga, wakati wa Mwalimu JKN.
Anna hajawahi kuolewa, na wala hana mume sasa. Ana mtoto mmoja wa kike, alizaa na Bwana mmoja (nadhani jina ni Ndunguru) ambaye alikuja kuwa Prof pale SUA. Nadhani ni mtu wa Songea au Ruvuma.
Last time kuonana naye, aliniambia binti yake yuko Marekani na kaolewa na mtu wa huko (siyo m-Tanzania), ila hakusema kama ni mzungu au mweusi. Na mimi sikuuliza.
Anna hana CPA lakini ni trained Auditor na ni mzuri sana katika hiyo kazi.
Ni dada mmoja mwenye heshima sana, uelevu na si msahalifu, hiyo ni ki-binafsi.
Ki-siasa ana mtazamo na msimamo mwingine ambao wakati mwingine unaweza kukuacha unakuna kichwa.
Namtakia mafanikio mema, na nina imani hii kazi ataiweza vizuri tu.