Anne Semamba Makinda's Profile!

Anne Semamba Makinda's Profile!

…Wadau wamchorea ramani Makinda


Source: Mwananchi; Saturday, 13 November 2010 00:26



cccspika%20wastaafu.jpg



Maspika wastaafu wa Bunge la Tanzania Pius Msekwa na Samwel Sitta wakipeana mikono nje ya Bunge baada yaa kumaliza jukumu la kumchagua spika mpya mjini Dodoma




UTEUZI wa Anna Makinda kuwa spika wa Bunge la kumi umepokewa kwa hisia tofuati huku wabunge, wananchi na taasisi kadhaa zimemtaka kutokubali kutumiwa na kikundi cha watu kwa maslahi binafsi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema Makinda anatakiwa kuwa imara na makini katika utendaji wake, kwani atakumbana na changamoto nyingi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe(Chadema) alisema Makinda ana uwezo mkubwa kuliongoza bunge, lakini anatakiwa kuendeleza mazuri ya bunge lililopita na kuweka ushabiki wa vyama pembeni ili aweze kuwatendea haki wabunge wote.

Mbowe ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni alitaja moja ya changamoto za Bunge hilo kuwa ni mwendelezo wa vita ya mafisadi kutoka kwa wapinzani.

Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda alisema hana shaka na uwezo, utendaji wa Makinda isipokuwa anatakiwa kufuata nyayo za mtangulizi wake, Samuel Sitta.

"Huyu mama ni mzuri sana, lakini najua asipokuwa makini lazima CCM wataingilia utendaji wake. Jambo hilo litaharibu kabisa na kuondoa mwelekeo wa sura ya bunge, hivyo ninamtaka asimame imara katika hilo kama alivyokuwa mtangulizi wake," alisema Shibuda.

Mbunge wa Mkanyageni kwa tiketi ya CUF, Habibu Mnyaa alimtaka Spika huyo kufanya kazi kwa nguvu zote ili aweze kufuta minong'ong'o kuwa alichaguliwa kwa hila na shinikizo la wakubwa wa CCM.

"Namshauri aendeleze mema na mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake kwani kuna ming'ong'ono kutoka kwa baadhi ya watu wanaodai kuwa ameingia kwa kazi maalumu hivyo afanye kazi ili aweze kuziba mapengo hayo," alisema Manyaa.

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Mafulila (NCCR-Mageuzi) alimtahadharisha spika huyo kuwa lazima atakutana na changamoto za vijana ambao kwa sehemu kubwa wanahitaji mageuzi.

Kafulila alimtaka Spika kuondoa u-CCM ndani ya vikao vya bunge ili aweze kutenda haki kwa watu wote na akamtaka afuate nyayo za mtangulizi wake ambaye alijenga heshima kubwa ndani ya bunge na nchi kwa ujumla.

Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema hataki kuamini kwamba Makinda anaweza kutumiwa na chama chake kuminya uhuru wa wabunge na kukiuka maslahi ya umma na kwamba, ikiwa hivyo wananchi hawataruhusu.

"Naamini CCM haiwezi kumburuza Makinda na kama ikifikia hali hiyo, Watanzania tuko macho hatudanganyiki tena hivi sasa. Lakini haiwezekani kuburuzwa kwa sababu anaongozwa na kanuni za bunge na sio za CCM," alisema Dk Bana.

Alisema hana wasiwasi na Makinda na kwamba, Watanzania wamepata Spika mzuri kwa sababu ana uzoefu, busara na hekima katika utendaji wake na kwamba ni mtu wa kanuni.

"Hofu yangu ni kwamba, sina uhakika kama Makinda ana uwezo wa kutosha kuhimili mikiki ya Bunge la vyama vingi, lakini kiuzoefu, busara na hekima tumepata Spika," alisema Dk Bana.

Alisema tatizo lililomwangusha Sitta ni kwamba, alijitambulisha wazi kuwa yumo katika kambi ya wabunge wa CCM, wanaoendesha mapambano dhidi ya wabunge wenzao wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali.

Alisema ingawa hilo haliko wazi lakini kila Spika anakuwa mtiifu na makini kwa chama na serikali ya chama chake, jambo ambalo Spika Sitta alionekana kulikiuka.

"Hili lilimwondolea sifa ya mamlaka ya kimaadili l Sitta kuwa Spika, kwa sababu hakuwa tena spika wa wabunge wote bali alikuwa wa kundi la wabunge wapambanaji," alisema Dk Bana.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (Saut) Dar es Salaam Profesa Mwesiga Baregu alisema: "Hofu yangu na Watanzania wengi ni uwezo wake wa kiutendaji na kukabiliana na shinikizo la CCM la kuzima mijadala ambayo wananchi watakaohoji maswali mazito kuhusu uwajibikaji wa serikali".

Hata hivyo, Profesa Baregu alielezea masikitiko yake kwa kitendo cha mchakato wa uteuzi wa mgombea wa Uspika uliofanywa na CCM ambao ulimtupa nje Spika aliyemaliza muda wake Samuel Sitta.

"Spika Sitta alichangamsha bunge na kuwaruhusu Watanzania kujenga ujasiri wa kuhoji masuala mazito kuhusu uwajibikaji na uadilifu wa serikali," alisema Profesa Baregu na kuongeza:

"Kitendo chake cha kuruhusu mijadala bungeni kilisaidia sana kuongeza na kunyanyua sauti ya upinzani bungeni, hadi leo hii tunashuhudia idadi kubwa ya wabunge kutoka vyama vya upinzani."

Kwa upande wake, Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimempongeza spika huyo mpya na wanawake wengine waliochaguliwa kuwa wabunge na kuwaasa kuwa wawe wabunifu, waadilifu na jasiri katika kulitumikia Taifa.

Makinda alichaguliwa jana na bunge kushika nafasi ya Spika wakati ambapo bunge la wakati huu limeongeza nafasi za wabunge wa viti maalumu kutoka 75 hadi 104.

Hii ni mara ya kwanza mwanamke kuchaguliwa kuongoza bunge ambalo ni moja ya mihimili mitatu ya dola. Mihimili mingine ni Serikali na Mahakama.

Mkurugenzi mtendaji wa Tamwa, Ananilea Nkya alisema jana katika taarifa yake kuwa viongozi wanawake waliochaguliwa, wanatakiwa kujiwekea malengo ya kuwatumika kwa bidii wananachi wote.

Nkya alisema, Makinda ni mwanamke mwenye busara, msimamo thabiti, hekima na ujasiri na kuwa atatoa uongozi mpya wenye mtazamo wa kijinsia unaojali zaidi maslahi ya Taifa na wanachi kwa ujumla.

"Tuna imani kuwa bunge hili jipya chini ya uongozi wa mwanamke litaonyesha mfano kwa vitendo kwamba katika mfumo wa vyama vyingi vya siasa inawezekana kuweka mbele maslahi ya wananchi na taifa kuliko maslahi ya vyama vya siasa au viongozi," alisema Nkya na kuongeza:

"Spika huyo atajenga mazingira mazuri yatakayoliwezesha bunge hilo kufanikisha taifa na kupata katiba mpya ambayo pamoja na mambo mengine, itachochea uwajibikaji wa viongozi katika ngazi mbalimbali."

Habari hii imeandaliwa na habel Chidawali, Dodoma, Salim Said na Minael Msuya, Dar

 
Hivi naombeni niwaulize utendaji wa kazi na historia ya familia yakekuna uhusiano wowote?
 
Makinda:Mimi si fisadi, dikteta

Source: Habari Leo, Tarehe: 12th November 2010

attachment.php


Spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, akiapa bungeni jana mjini Dodoma kuanza rasmi kazi hiyo baada ya kuchaguliwa kwa kura nyingi na wabunge wa Bunge hilo.



SPIKA mpya wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda (61) amesema, yeye si fisadi, hakuna mtu au kikundi cha watu kilichomuweka kwenye nafasi hiyo na hakuna anayeweza kumtumia.

Makinda amesema, katika ratiba ya maisha yake alipanga kuwa Spika wa Bunge la Tanzania, hivyo hayupo hapo kwa bahati mbaya.

Amesema, alitaka kuwa Spika, ni sehemu ya ratiba ya maisha yake na kama angetumiwa asingetaka kuwa kwenye nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa Makinda, mwaka kuna watu walimshawishi agombee uspika wa Bunge mwaka 2005, ilikuwa lazima agombee wakati huu lakini kama Samuel Sitta angegombea yeye (Makinda) angejitoa.

Amesema hatagombea ubunge mwaka 2015, hajawahi kutumia hata senti katika kampeni, wanaomfanyia hivyo huwa wanafanya kwa mapenzi yao.

Makinda amepuuza madai kuwa, kuna mafisadi wamemuweka kwenye nafasi hiyo, na wanamlipia mkopo wa nyumba.

Amekiri kuwa anadaiwa benki, deni lake litakwisha mwaka 2019, analipa kila baada ya miezi mitatu, na amehoji kwamba, kama kuna mafisadi wamemuweka kwenye nafasi hiyo kwa nini hawamlipii deni hilo.

Makinda amewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, katika maisha yake hajawahi kutawaliwa, anaishi kadri anavyoamua yeye na hakuna anayeweza kulibadili hilo.

Amepuuza pia maneno kwamba, watu wanaotaka kugombea mwaka 2015 watalitumia Bunge kujisafishia njia, na amebainisha kwamba, wanaweza kufanya hivyo kwenye vyama vyao na si bungeni.

Makinda amesema, kitaaluma yeye ni mkaguzi wa hesabu, aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1975 na alitumia miezi sita kujifunza masuala ya Bunge.

"I have been in the Parliament for all may life" amesema Makinda akimaanisha kwamba, amekuwa bungeni maisha yake yote na kwamba, kitu kikubwa alichokifurahia katika maisha yake ni kuwa Mbunge

Mwanasiasa huyo pia amesema, yeye si dikteta na hakuna namna ambayo Spika wa Bunge anaweza kuwa hivyo.

Amesema, kinachozingatiwa bungeni ni Kanuni za Bunge na zisipotumika kutakuwa na fujo hivyo wabunge wajenge hoja na hakutakuwa na kukomoana.

"Wabunge lazima wajifunze networking na wanapofika humu lazima wawe realistic (wawe na uhakika) toka huko" amesema na kuwataka wabunge wawe makini.

Makinda amesema, wabunge wanapaswa kuwa na uwezo wa kuibua vitu na wawe na ushahidi na kwamba hilo ni jukumu lao.

"Siasa yeyote sio kuzua maneno na mnapozua mnasababisha vurugu ndani ya Bunge"amesema mwanasiasa huyo aliyejiwekea historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuwa Spika wa Bunge la Tanzania.

Amesema, anasikitika kwamba, kulikuwa na kashfa moja tu katika Bunge lililopita iliyohusu mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati ya Serikali na kampuni hewa ya Richmond.

"Pale zilitakiwa Richmond zaidi ya 10' alisema Makinda katika moja ya kumbi za mikutano katika Ofisi ya Bunge mjini Dodoma na akabainisha kwamba, wakati mwingine wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani huungana kwenye suala kama hilo.

 

Attachments

  • Makinda.jpg
    Makinda.jpg
    49.6 KB · Views: 175
Mie nilimwona mara moja tu huyu makinda nikiwa mtoto, alikuja kanisa la catholiki jirani na home kwetu ambapo alikuwa kwenye benzi nyeusi. zamani sana.
hilo ndo nilijualo kwa sasa. ila nimefurahi kumsoma kwa undani zaidi maana nimekuwa nafuatilia sessions za bunge kwa sana tu na ninamwona kama mtu ambaye kisaikolojia hayuko sawa na hii ni hatari sana. inawezekana hii ya kukosa mwenzi ni sababu mojawapo
 
Mie nilimwona mara moja tu huyu makinda nikiwa mtoto, alikuja kanisa la catholiki jirani na home kwetu ambapo alikuwa kwenye benzi nyeusi. zamani sana.

hilo ndo nilijualo kwa sasa. ila nimefurahi kumsoma kwa undani zaidi maana nimekuwa nafuatilia sessions za bunge kwa sana tu na ninamwona kama mtu ambaye kisaikolojia hayuko sawa na hii ni hatari sana. inawezekana hii ya kukosa mwenzi ni sababu mojawapo

Msanii; kwa sasa ni vigumu kujua kwani alikuwa Naibu. Sasa hivi ni mtu Mkubwa na anashikilia moja ya Mhimili. anaweza kuwa Kaimu rais ikibidi. Na kama hoja nzito ikija ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani Rais anatakiwa aisimamie.

Huenda ni wasiwasi tu wa Wadau kwa kuwa Kihisoria anakuwa mwanamke wa kwanza kufikia level hii ya juu sana Tanzania ukiacha Migiro ambaye yuko UN na mama Mongela ambaye alikua AU.
 
Sitta amwosia Anne Makinda

Source: Habari Leo

KWA kawaida katika familia mzee anapoondoka huacha wosia kwa wanaobaki hata kama kuondoka kwake kunaweza kuwa si kwa kumfurahisha, ndivyo alivyofanya jana Spika wa zamani.

Samuel Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki, baada ya jana kupokea ushindi wa Spika Anne Makinda (61) kwa moyo mkunjufu, hakuwa mnyimi wa ushauri na hivyo akamtaka ajiandae kwa changamoto kubwa mbele yake.

“Namfahamu vizuri Makinda, ni mchapakazi, lakini cha msingi avae viatu vyangu katika kazi hiyo, kwa sababu Bunge hili lina changamoto nyingi kutokana na kuwa na watu wa aina mbalimbali wenye fani mbalimbali.”

Wosia huo ulitolewa pia na wabunge mbalimbali wakimpongeza na kumhadharisha awe jasiri na asikubali kufanya kazi kwa kushinikizwa na watu kwa maslahi binafsi na kuegemea CCM.

Sambamba nao, mshindani wake, mwanasheria Mabere Marando, aliyepata kura 53 kati ya 318 halali, alisema Makinda ameshinda kutokana na kura za wabunge wa chama chake, ambao walilazimishwa kumpigia kura. Makinda alipata kura 265.

Marando alisema “nampa hongera Makinda, lakini nimetambua kuwa amepata kura za chama, CCM wemejipigia wenyewe, kwani walidhibitiwa na chama chao wampe yeye (Makinda) kura, kazi iliyobaki sasa ni kuijenga Chadema ifike mbali na isiyakute yaliyoikuta NCCR-Mageuzi, ili uchaguzi ujao CCM iwe upinzani.”

Hamad Rashid Mohamed wa CUF, alisema kuna uwezakano mkubwa Makinda akaegemea chama chake wakati wa kufanya kazi ya uspika na hata kama hatataka, atalazimishwa kuegemea chama chake na kusisitiza “yeye lazima ahakikishe anaonekana ana uamuzi wake na atende haki.

“Spika ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM lazima ataegemea chama chake, tunatakiwa sasa kubadilika na kufuata Kenya ambako mbunge akishakuwa Spika anatoka kwenye mkondo wa chama,” alisema.

Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda wa Chadema, alimtaka Spika kutofanya kazi yake kwa matakwa na utashi wa watu binafsi bali afanye kwa manufaa ya Taifa na kumhadharisha kutoweka urafiki katika utendaji wa kazi yake.

“Rafiki anayempenda Makinda amwache atimize kazi yake bila kumwingilia … CCM ina deni la kuhakikisha Spika wa chama chao hatasongwa na watu waliopo kwa maslahi yao binafsi, Bunge likileta U-CCM wajue uspika ndiyo mtaji wao wa kisiasa, hivyo wamwache afanye kazi kwa uhuru, kanuni na taratibu za Bunge,” alihadharisha.

Katika hatua nyingine, Hamad alisema CUF inaendelea na mazungumzo na Chadema kuhusu kuundwa kambi ya upinzani na imetoa masharti kwa Chadema kuwa itashirikiana nayo iwapo itaviingiza vyama vyote kwenye kambi hiyo.

Alipoulizwa itawezekanaje wakati Chadema imeshaunda kambi ya upinzani na kuteua viongozi wake, alisema “jana (juzi) niliongea na Mbowe (Freeman) na anaweza kubadilisha kambi yake, nasi CUF tumetoa masharti ya kuungana nao ni kambi kuwa na vyama vyote na si CUF na Chadema pekee,” alisema Hamad ambaye ni Mbunge wa Wawi, Pemba.
 
JK ampongeza Makinda, aahidi atampa ushirikiano



Source: Nipashe​


mremamakinda.jpg



Mbunge wa Vunjo kwa tiketi ya TLP, Augustine Mrema, akisalimiana na Mbunge wa Njombe Kusini,Anne Makinda, baada ya kuonana nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma jana.


Rais Jakaya Kikwete (pichani) amemtumia salamu za pongezi, Spika wa Bunge, Anne Makinda kwa kuchaguliwa kwake na kuahidi kushirikiana naye katika kulitumikia taifa.


Taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana, ilieleza kwamba Rais Kikwete alisema Spika Makinda amechaguliwa kwa sababu ya uwezo wake, uzoefu na umakini wake.
"Ninakuahidi ushirikiano wangu katika shughuli zako za bunge na za kujenga nchi yetu kwa ujumla," Rais alikaririwa katika taarifa hiyo na kuongeza kuwa kuchaguliwa kwa Makinda ni heshima kwa Chama Cha Mapinduzi.​

"Ni heshima kwa Chama Cha Mapinduzi, umejenga imani kubwa kwa wanawake na umewatia moyo na shauku ya kufanya kazi kwa ufanisi na ueledi katika jitihada zao za kushika nyadhifa mbalimbali za maamuzi," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo ikimkariri Rais Kikwete.​


Tamwa yawapa changamoto viongozi wapya wanawake

Kwa upande wake, Chama Cha Wanahabari Wanawake nchini (Tamwa), kimewapongeza wanawake waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi kufuatia uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hata hivyo, Tamwa imewaasa wawanake kujiwekea malengo ya kuwatumikia wananchi wote kwa bidii, ubunifu, uadilifu na ujasiri mkubwa.​

Taarifa ya Tamwa iliyosainiwa na Mkurugenzi wake, Ananilea Nkya, na kusambazwa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana iliwataja wanawake hao kuwa ni pamoja na Anne Makinda, aliyechaguliwa kuwa Spika wa Bunge, wabunge na madiwani kupitia majimboni na viti maalum.​

"Tunamwamini Anne Makinda kuwa ni mwanamke mwenye busara, msimamo thabiti, hekima na ujasiri na kwamba atatoa uongozi mpya wenye mtazamo wa kijinsia unaojali zaidi maslahi ya taifa na wananchi wengi wakiwemo wanawake, wanaume na watoto wanaotaabika kutokana na ufukara," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.​

"Ni matarajio yetu makubwa pia kwamba Spika Makinda atajenga mazingira mazuri yatakayoliwezesha Bunge lijalo kufanikisha taifa letu kupata katiba mpya ambayo pamoja na mambo mengine, katiba hiyo itachochea uwajibikaji wa viongozi katika ngazi mbalimbali na kujituma kwa wananchi kufanya kazi kwa bidii ili kujenga taifa jipya lenye kujitegemea," ilisema.​

Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (Shivyawata), kwa kushirikiana na asasi zinazotoa huduma kwa watu wenye ulemavu nchini, wamemtumia salamu za pongezi Spika Makinda.
"Kuchaguliwa kwake kumefungua milango mipya kwa wanawake kuweza kushika uongozi mkubwa kati ya moja ya mihimili ya dola…tunampongeza sana mheshimiwa Anne Makinda," ilisema sehemu ya taarifa ya shirikisho hilo iliyotumwa kwa vyombo vya habari.​


 
tumpe muda jamani!
nadhani ni muda muafaka wa kuziweka tofauti zetu ki-siasa pembeni na kuiangalia nchi yetu!

GENERAL SPEAKING,naona anafaa tu

SHUKRANI ZA DHATI KWA FMES
 
Jana nilipost thread yangu titled: Tunapojadili jinsia ya ana makinda na kusahau mustakabali wa taifa letu, leo asubui naona haipo. Hii si mara ya kwanza, niliwahi tena kubandika hapa kuhusu, ahadi za kikwete wakati wa kampeni kufikia trilioni tisini, baada ya masaa mawili nayo ikayeyuka, bahati mbaya nikaiona kwenye gazeti la mtanzania daima

sasaa, kama ni hivyoo sioni tena umuhimu wa kubandika chochote hapa, sitendewi haki
Shida watu wengine nyie ni wa ajabu sana. Hujatafuta post yako kwenye forums au threads nyingine zote unalalamika.

Na mimi naanza kuona kwa nini ni lazima hata kama mimi ni Mod nitafuta posts zako. Huweki Posts zako kwenye majukwaa yanayostahili. Kwa mfano haya malalamiko yana Forum yake wewe umeweka hapa kwenye forum ya uchaguzi, huoni kuwa umekosea? Post articles zako kwenye majukwaa husika please.

Moderators wanapokuta thread imewekwa jukwaa lisilohusika wanaihamishia jukwaa linalohusika au kama ina relate na Thread nyingine iliyokwisha kuanzishwa wanaziunganisha. Usibwabwaje tu hapa! Kama wamefuta ni haki yao.
 
Wakati wanazaa naye Prof. tayari alikuwa ameoa au bado? Hii itasaidia kujua background yake in Moral Values.

Kwenye moral value hazina uhusiano katika kuchapa kazi kama mtu ni commited kwenye kazi na yuko fair. Kuna watu wangapi ambao kwenye moral value unweza kuwapa 99.9% lakini kwenye kazi hovyooooo na wale ambao maral value unaweza kuwa 30% lakini kwenye kazi ana-score 99.9% kama vile Rais wa Marekani wa zamani Bill Clinton.

Mimi nafikiri kiongozi yeyote tum-evaluate kwa utendaji kazi na si kwa ametemmbea na wangapi au na nani kimapenzi
 
Kwenye moral value hazina uhusiano katika kuchapa kazi kama mtu ni commited kwenye kazi na yuko fair. Kuna watu wangapi ambao kwenye moral value unweza kuwapa 99.9% lakini kwenye kazi hovyooooo na wale ambao maral value unaweza kuwa 30% lakini kwenye kazi ana-score 99.9% kama vile Rais wa Marekani wa zamani Bill Clinton.

Mimi nafikiri kiongozi yeyote tum-evaluate kwa utendaji kazi na si kwa ametemmbea na wangapi au na nani kimapenzi

Kamanda ulisikiliza Hotuba ya Mwalimu Nyerere pale Kilimanjaro?

Uadilifu ni nini?
 
Ukweli kwamba uteuzi wake ulikuwa na mkono wa mafisadi ndani ya chama chake haupingiki kwa vile sababu alizojaribu kutoa Makamba ni vague na ni za kuihalifu Katiba ya nchi na hata ile ya chama chao CCM. Inawezekana kabisa mwenyewe hakuwa aware kupigiwa upatu na mafisadi, ingawa kitendo cha kuchukua fomu kupambana na aliyekuwa bosi wake pia kinazalisha swali la kulikoni? CCM waliwatega watanzania kwa siasa za gender balance, ukweli ni kwamba walikuwa na sababu za kimaslahi zaidi kuliko walivyotueleza.


- Mkuu ninaomba kutofautiana na wewe respectively kwamba mafisadi will never let this woman to be a Speaker maana wametumia mbinu chafu sana kujaribu kumzuia asirudi bungeni, unless tukiulizana mafisadi ni nani! Mimi ninaamini sana kwamba huu ulikuwa ni uamuzi wa Ikulu kitu ambacho kinaninfanya niamini kwamba kuna mabadiliko makubwa sana yanakuja na term ijayo, mkuu ninaomba nikuhakikishie kwa Miungu yangu yote ni kwamba mafisadi ninaowajua wametumia kila njia kuhakikisha huyu mama harudi bungeni na jana wameumia sana kuona anakuwa Spika.

- Chaguo lao mafisadi lilikuwa Mh. Anna Abdallah, na Mh. Kate Kamba siku zote ni chaguo la Wazee Butiku na Warioba.


William.
 
kitu ambacho kinaninfanya niamini kwamba kuna mabadiliko makubwa sana yanakuja na term ijayo

William.


Kiongozi, Hapa sikubaliani kabisa, Hakuna mabadiliko yeyote iwapo huyu huyu Mkwere alisimama kwenye majukwaa kuwanadi akina Lowassa, Rostam na hata Mzee Mramba akisema hao ni watu safi! Kila Mtanzania anajua hao ni mafisadi wa kutupwa. Leo unataka kuja na hadithi eti tutegemee mabadiliko, uko serious kweli mazee/

Mch Masa K
 
Kiongozi, Hapa sikubaliani kabisa, Hakuna mabadiliko yeyote iwapo huyu huyu Mkwere alisimama kwenye majukwaa kuwanadi akina Lowassa, Rostam na hata Mzee Mramba akisema hao ni watu safi! Kila Mtanzania anajua hao ni mafisadi wa kutupwa. Leo unataka kuja na hadithi eti tutegemee mabadiliko, uko serious kweli mazee/

Mch Masa K

- Mkuu matokeo ya uchaguzi yako very clear kwamba wananchi wengi sana wamemuadhibu Rais kwa hayo makosa ya kwenye kampeni, kuna mahali nimesema kwamba Rais anahitaji kuwafukuza kazi maramoja wale wote waliomshauri kwenda kwenye majimbo ya wagombea wanaotuhumiwa kuhusika na corruptions, kwamba haikuwa lazima aende kwenye hayo majimbo na pia haikuwa lazima wagombea hao wawepo kwenye kampeni za Rais, ninaamini matokeo yamemfahamisha Rais na CCM kwa ujumla kwamba hatuwezi kuwa-take wananchi for granted kama zamani.

- Again my point ni kwamba ninafahamua standing za Mama Makinda, kuanzia kwenye CC na ndani ya bunge, na kuchaguliwa kwake ni lazima kuwepo na mkono wa Ikulu, sasa why would Ikulu support her to be a Speaker kama hawana nia ya mabadiliko na hasa kuyasikiliza matokeo ya uchaguzi wa juzi na knowing huyu mama standing? Ndipo ninaposema kwamba ninaamini kwamba huenda kuna mabadiliko makubwa yanakuja ni imani yangu tu, looking at political facts at hand.


William
 

- Mkuu matokeo ya uchaguzi yako very clear kwamba wananchi wengi sana wamemuadhibu Rais kwa hayo makosa ya kwenye kampeni, kuna mahali nimesema kwamba Rais anahitaji kuwafukuza kazi maramoja wale wote waliomshauri kwenda kwenye majimbo ya wagombea wanaotuhumiwa kuhusika na corruptions, kwamba haikuwa lazima aende kwenye hayo majimbo na pia haikuwa lazima wagombea hao wawepo kwenye kampeni za Rais, ninaamini matokeo yamemfahamisha Rais na CCM kwa ujumla kwamba hatuwezi kuwa-take wananchi for granted kama zamani.



William

That was a political suicidal mazee! Kama wapinzani wangekuwa makini ile ilikuwa ni silaha za kuwamaliza CCM! Tafsiri ingekuwa CCM ni chama kinachobeba wala rushwa na mafisadi. Hakuna siri hata wewe wajua urafiki wa Lowassa na Rostam ilikuwa ni lazima Kikwete aende kwenye majimbo yao. Ningeamini kweli amedhamilia kumaliza rushwa kwenye chama chake kwa kutopitisha hata majina yao kuwa wagombea wa CCM. Bila shaka hili lingeweka imani kubwa sana kwa wananchi hata mimi Mpinzani ningejua kweli CCM wameamua kuwa chama kile kilichoasisiwa na Mwalimu. Kukampenia Lowassa, Chenge na Rostam haikuwa turufu kwa uimara wa CCM kwa miaka ijayo. Kutumia familia kama ni wanakampeni wa raisi na CCM inaiweka CCM mahali pabaya sana iwapo CCM wataweka mgombea dhaifu coming 2015.

Anna Makinda utendaji wake tutauona muda si mrefu kwenye uspika, kama nilivyosema jana! Mama atajijengea heshima sana iwapo ataacha UCCM kwenye masuala nyeti ya kitaifa. Aweke maslahi ya taifa mbele bila kujali ni hoja ya TLP, NCCR, CUF ama CHADEMA.

Mchungaji Masa K
 
Back
Top Bottom