Anne Semamba Makinda's Profile!

William;

Mkuu kwanza habari za siku? Tumepoteana sana humu jamvini na nashukuru leo nimekutia machoni.

Most intresting ni facts zako. Kwanza unatumia ID yako ya kweli na picha yako, so Anna Makinda na Wadau wanakusoma na wanajua ni nani na utakuwa judged kwa hilo.

Nasshukuru kwamba umetupatia first hand information ambazo hazijachakachuliwa.

Wakati mengi uliyotuleza ni mazuri na hakika ni ya uhakika, je kuna mapungufu yoyote ya Kiuongozi aliyonayo ambayo wewe binafsi unayajua? Utakuwa umetusaidia sana kama utatuambia maana najua Anne is not an Angel.

Usipotee sana Mkuu.
 
William;

Mkuu kwanza habari za siku? Tumepoteana sana humu jamvini na nashukuru leo nimekutia machoni.

Most intresting ni facts zako. Kwanza unatumia ID yako ya kweli na picha yako, so Anna Makinda na Wadau wanakusoma na wanajua ni nani na utakuwa judged kwa hilo.

Nasshukuru kwamba umetupatia first hand information ambazo hazijachakachuliwa.

Wakati mengi uliyotuleza ni mazuri na hakika ni ya uhakika, je kuna mapungufu yoyote ya Kiuongozi aliyonayo ambayo wewe binafsi unayajua? Utakuwa umetusaidia sana kama utatuambia maana najua Anne is not an Angel.

Usipotee sana Mkuu.


- Ahsante sana mkuu ni kwamba Jamiiforums ni chombo kikubwa sana sasa katika jamiii ya taifa la Tanzania, nimeshirki kwa majina ya bandia kwa muda mrefu sana toka tukiwa kule BCS, Jambo Forums, TEF mpaka kufikia JF, I mean tumetoka mbali sana na hii mitandao, sasa ilifika mahali baadhi yetu hapa JF kama kina Dr. Kitila, tukaamua kwamba tunataka kwenda open kwa majina yetu kamili na picha, ili pamoja na mengine kuipa JF integrity zaidi kwamba hata ukijitokeza wazi hakuna tatizo, ninakumbuka siku ya kwanza nimemfahamisha Mkuu Invisible kuhusu uamuzi wangu kwanza he was very hesitant lakini kwa vile tunaheshimiana sana akanikubalia na kunitakia baraka zote, I am praying kwamba ndugu yangu sana Mkulu Mwanakijiji siku moja naye atajiunga na huu uamuzi.

- Otherwise, Mama Makinda as a human being ni mtu asiyependa mchezo au masihara kwenye kazi za masilahi ya taifa, hivyo hukasirishwa sana na wanaopenda mchezo mbele ya kazi ya wananchi yaani taifa. Mkuu ninakushukuru sana na huu mjadala, well she is my friend na nilidhani ni muhimu nikamjadili as I know her.


William.
 
Jana nilipost thread yangu titled: Tunapojadili jinsia ya ana makinda na kusahau mustakabali wa taifa letu, leo asubui naona haipo. Hii si mara ya kwanza, niliwahi tena kubandika hapa kuhusu, ahadi za kikwete wakati wa kampeni kufikia trilioni tisini, baada ya masaa mawili nayo ikayeyuka, bahati mbaya nikaiona kwenye gazeti la mtanzania daima

sasaa, kama ni hivyoo sioni tena umuhimu wa kubandika chochote hapa, sitendewi haki
Mbona umebandika hii au hii haina umuhimu.
 
Jana nilipost thread yangu titled: Tunapojadili jinsia ya ana makinda na kusahau mustakabali wa taifa letu, leo asubui naona haipo. Hii si mara ya kwanza, niliwahi tena kubandika hapa kuhusu, ahadi za kikwete wakati wa kampeni kufikia trilioni tisini, baada ya masaa mawili nayo ikayeyuka, bahati mbaya nikaiona kwenye gazeti la mtanzania daima <br />
<br />
sasaa, kama ni hivyoo sioni tena umuhimu wa kubandika chochote hapa, sitendewi haki
<br />
<br />

JF ina mkono wa TISS hukulijua hilo? Haiko that freeeee
 
Jana nilipost thread yangu titled: Tunapojadili jinsia ya ana makinda na kusahau mustakabali wa taifa letu, leo asubui naona haipo. Hii si mara ya kwanza, niliwahi tena kubandika hapa kuhusu, ahadi za kikwete wakati wa kampeni kufikia trilioni tisini, baada ya masaa mawili nayo ikayeyuka, bahati mbaya nikaiona kwenye gazeti la mtanzania daima

sasaa, kama ni hivyoo sioni tena umuhimu wa kubandika chochote hapa, sitendewi haki


Unamfahamu malaria sugu? Geniusbrain?
 
Jana nilipost thread yangu titled: Tunapojadili jinsia ya ana makinda na kusahau mustakabali wa taifa letu, leo asubui naona haipo. Hii si mara ya kwanza, niliwahi tena kubandika hapa kuhusu, ahadi za kikwete wakati wa kampeni kufikia trilioni tisini, baada ya masaa mawili nayo ikayeyuka, bahati mbaya nikaiona kwenye gazeti la mtanzania daima

sasaa, kama ni hivyoo sioni tena umuhimu wa kubandika chochote hapa, sitendewi haki

yaani wamefuta article yako, alafu ukaiona kweny gazeti la mtanzania..?!! kuna MOD alipewa kitu kidogo nini..? neways lbda zitakuwa zimeamishwa majukwaa mengine! jaribu kufuatilia
 
Ukweli kwamba uteuzi wake ulikuwa na mkono wa mafisadi ndani ya chama chake haupingiki kwa vile sababu alizojaribu kutoa Makamba ni vague na ni za kuihalifu Katiba ya nchi na hata ile ya chama chao CCM. Inawezekana kabisa mwenyewe hakuwa aware kupigiwa upatu na mafisadi, ingawa kitendo cha kuchukua fomu kupambana na aliyekuwa bosi wake pia kinazalisha swali la kulikoni? CCM waliwatega watanzania kwa siasa za gender balance, ukweli ni kwamba walikuwa na sababu za kimaslahi zaidi kuliko walivyotueleza.
La muhimu Mama huyu atumie busara zake kutekeleza majukumu yake na "abadilike" Yaani aachane na ushabiki wa chama chake kama ilivyojidhihirisha hapo nyuma kwa maana kama kuna Spika watanzania wote wanamfuatilia kwa karibu ni huyu wa sasa ambaye watanzania watajaribu kujiridhisha kama hakuwekwa na CCM kwa malengo ya kuwakingia kifua na kuwasafisha mafisadi. Itakuwa salama zaidi kwake kujipambanua dhidi yao (Mafisadi) na kuendeleza mijadala yenye afya kama mwenzake Sitta ili kulinda heshima yake, ya wanawake na chama chake dhidi ya hasira za umma zinazoweza kujidhihirisha 2015.
Juu ya ufuatiliaji wa maisha yake binafsi sioni sababu zaidi ya kumnyanyasa tu. Mbona hakuna aliyefuatilia mambo hayohayo kwa waliomtangulia yaani Sitta na hata Msekwa. Kama ni muhimu kufuatilia undani wa wanaotuongoza tusianzie na huyu mama, bali wote, kuanzia Rais, mawaziri, wakuu wa mikoa n.k.
Mimi naamini nguvu ya umma itamsukuma huyu mama kufanya kazi kwa umakini na uadilifu na pengine anaweza kuonekana "kichomi" kwa CCM zaidi hata ya Sitta kwa maana hata huyo walimlaumu tu bila ya kuelewa kwamba ilimbidi kufanya alivyokuwa akifanya kuitikia matakwa ya umma.
 
TANGU ASUBUI LEO, VITUO VYOTE VYA REDIO NA TELEVISHENI HAPA VINASHINDANISHA WATAZAMAJI WAKE, NA WASIKILIZAJI KUHUSU SPIKA MPYA MWANAMKE WA AFRIKA MASHARIKI , KATI NA JANGWA KUSINI MWA SAHARA! hakuna tena kujadili kuhusu mustakabali wa taifa letu, lililotekwa na mafisadi wachache wasiozidi kumi. watu wanazungumzia kuhhusu jinsia ya spika mpya makinda, wamesahau kuwa jinsia ya anna makinda siyo muarobaini ya matatizo ya nchi yetu. wakati tupo kwenye kiza hiki kinene kuzungumzia jinsia ya anna makinda , akina rostam azizi na wengine wako bize kule bahi na namtumbo wakichimba urenium na tutakapozinduka madini haya adimu yaktakuwa yamekwisha.

watanznia wenzangu, hakuna atakaye pinga hata mama makindaakishika kiti cha kikwete provided hatutakuwa na mafisadi humu nchini.

tuache kushangilia mongela kuwa rais wa beijing, makinda kuwa spika, migiro kuwa katibu wa un. dada zetu hawa wawe mbele kupigana dhidi ya mafisadi, hawa ni da da zetu, mama zetu, bibi zetu, wanastahili kupewa hivi vyeo, wana nwake msibweteke, vita ni kubwa mbele yenu. msikubali kuhungwa mnastahili.

was on the same line of thinking, tumetekwa! hoja za msingi zimepindishwa, everyone is talking about GENDER instead of corrupted election and how we as nation has to move on, CCM wakali!
 
Kwa kweli kuchaguliwa kwa huyu mama ni maafa kwa taifa. Anakana kuwekwa na mafisadi wakati huohuo anasema yeye hajui kama kuna mafisadi kwani kwa ufahamu wake fisadi ni mwanaume anayeiba mke wa mtu (nukuu ya gazeti la Mwananchi la leo). Tanzania ya leo tunahitaji Spika mwenye ufahamu wa kiwango cha chini kiasi hicho?
 
Dhamira yake kwenye kupambana na ufisadi ndio bado inanipa mashaka..,otherwise time will tell.
 
Mtoto wa Anna atakuwa mkubwa kuliko huyo Neema. Neema atakuwa ni mtoto wa mke ambaye Prof alimuoa baada ya kuzaa na Anna. Watoto wa Prof kwa mke huyo wamesomea South Africa. I remain to be corrected .

mwenzako alisema anaitwa neema makinda na anafanana na Anna nakinda....

lets go...
 
Jana nimehudhuria press conference ya kwanza, Huyu mama yuko fit kila idara, waandishi walimrushia makombora ya kila aina na aliyapangua yote with confidence na bila emotions. That was a good start.
 
Ukiangalia jinsi alivyokuwa anawahandle wapinzani alipokuwa anaendesha vikao wakati wa bunge lililopita utatambua kuwa she is short-fused!! Unless anabadilika kazi hii ya kuendesha bunge itamuwia vigumu sana hata akapata ugonjwa wa shinikizo la damu kama hanaompaka sasa!! She has to learn to be calm!!

In deed Bulesi! Calmness is the character of the greatest. We learn it hard way sometimes. The truth of the matter is all the voices in parliament must be heard including of those that CCM would label, dissidents.
 
<font size="3"><font color="blue"><br />
- Ahsante sana mkuu ni kwamba Jamiiforums ni chombo kikubwa sana sasa ka
tika jamiii ya taifa la Tanzania, nimeshirki kwa majina ya bandia kwa muda mrefu sana toka tukiwa kule BCS, Jambo Forums, TEF mpaka kufikia JF, I mean tumetoka mbali sana na hii mitandao, sasa ilifika mahali baadhi yetu hapa JF kama kina Dr. Kitila, tukaamua kwamba tunataka kwenda open kwa majina yetu kamili na picha, ili pamoja na mengine kuipa JF integrity zaidi kwamba hata ukijitokeza wazi hakuna tatizo, ninakumbuka siku ya kwanza nimemfahamisha Mkuu Invisible kuhusu uamuzi wangu kwanza he was very hesitant lakini kwa vile tunaheshimiana sana akanikubalia na kunitakia baraka zote, I am praying kwamba ndugu yangu sana Mkulu Mwanakijiji siku moja naye atajiunga na huu uamuzi.
<font size="4"><font color="red">William.</font></font>
Nakupongeza kwa kuja rasmi na true identity. Nawapongeza na wote wenye majina halisi wanaifanya JF iwe more real with real people hata posti wanaposti wenye real names ni tofauti na enzi zile za pen names hivyo kuipa JF more credibility.
 
nchii bana

kuna kipindi wakati mkapa anataka kumaliza mda wake watu walikuja juu wakasema si-aendelee maana kafanya makubwa---jamaa akasema mi nasepa.

baadae akaja jk ndani ya mwezi mmoja mkapa alifunikwa mbaya mpaka wakenya wakatoa katuni ya ajabu juu ya waandishi wa habari wa tz....

tumeendaa weeee....ikafika mahali kikwete akanza kutia kichefuchefu....kama kawaida watanzania wakamkumbnuka mkapa....ohh walau mkapa uchumi uliimarika nchi ikapata heshima---jk kasimama juu ya mabega ya mkapa hakuna analofanya anatafuna pesa zilizoachwa---

sasa imeingia issue ya uspika--- jamani sita alikuwa anafaa---huyu mama katumwa----mara ohhh sita chuma cha pua----

NA NDIO MAANA HATUENDI MBELEKAMA TAIFA MDA MWINGI NI KIPIGA POROJO TUUUU----SUBIRI AFANYE KAZI NDO TUJIE KAMA KWELI HUYU MAMA NI SHUPAVU KAMA WILLIAM ANAVYOSEMA-- hata mimi nikekwa karibu sana na jk lakini mbona kila kukicha ananiaibisha...... !!!! na mpaka sasa simtambui kama raisi na hili analijua...
 
anamakindampya.jpg


Spika mpya wa Bunge, Anna Makinda akiongozwa na Askari wa bunge kuingia bungeni mjini Dodoma jana baada ya kuchaguliwa na wabunge wengi kushika wadhifa huo


Sitta ampa changamoto Makinda

Source: Mwananchi; Saturday, 13 November 2010 00:30

BAADA ya wabunge kumchagua kwa kishindo Anna Makinda kuwa Spika wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyekuwa Spika wa Bunge la tisa, Samuel Sitta amemtaka kuwa makini kwa kuhakikisha kwamba, chombo hicho cha kutunga sheria hakipotezi mwelekeo kutoka mahali kilipofikia kidemokrasia.

Makinda ambaye ni mbunge wa Njombe Kusini, alichaguliwa jana kwa kura 265 ambazo ni sawa na asilimia 74.2 ya kura zote zilizopigwa (327), huku mpinzani wake Mabere Marando akiambuliwa 53 (asilimia 16.2) na kura tisa ziliharibika.

Baada ya matokeo hayo, Spika Makinda aliwashukuru wabunge kwa kumchagua kwa kura nyingi ambazo alisema anaamini zimeonyesha kuwa wabunge wengi wamemkubali. Aliahidi kuwa atafanya kazi ya uspika kwa kuzingatia misingi na kanuni za bunge.

"Nitajitahidi kuzielewa kanuni za bunge pamoja na ninyi waheshimiwa wabunge, hivyo naomba mzisome na kuzielewa vema sheria za Bunge letu tukufu ili kusiwe na mgongano wa kimaslahi," alisema Makinda.

Spika huyo alisema atajitahidi kulifanya bunge liwe moja, bora, imara na liwe la watu wote kwa kuanzisha utaratibu wa vipindi katika vyombo vya habari ikiwemo radio ambavyo vitawawezesha wananchi kuzielewa kanuni za Bunge.

Aliwaonya wabunge kwamba hatakiwi kupeleka ndani ya bungeni hoja zenye maslahi binafsi au kwa kutumiwa na mtu au vikundi vya watu na kusisitiza kuwa wapeleke bungeni hoja zinazotoka katika majimboni yao.

"Kitakachozingatiwa humu bungeni ni sheria, kanuni na taratibu hatuwezi kuingiza bungeni mambo yanayobeba maslahi ya watu fulani au vikundi, hivyo msome na mzielewe kanuni za Bunge," alisisistiza.

Akitoa mchango wake kuhusiana na kuchaguliwa kwa Makinda, Sitta ambaye alijizolea umaarufu kwa kuliongoza Bunge lililopata umaarufu kutokana na kuruhusu mijadala ya wazi, alimtaka spika huyo kutoyumbishwa katika kipindi chote cha uongozi wake.

Alibainisha kuwa hivi sasa wananchi wameelevu zaidi kwani wanafuatilia kwa umakini masuala ya Bunge, hivyo wanahitaji kuona vitu vizuri na haki ikitendeka ndani ya chombo hichi. Alishauri kuwa viwango na msimamo waliokuwa wameufikia katika Bunge la Tisa unafaa kuendelezwa.

Sitta alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari nje ya Viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Alisema hana shaka na uwezo wa Makinda, lakini alibainisha kuwa Bunge la Kumi lina changamoto kubwa kuliko mabunge yote yaliyotangulia katika historia ya Tanzania.

"Mimi nadhani ataweza kumudu vema kazi hiyo, ila ninamtahadharisha kuwa asiwe na msimamo wa kuyumbishwa na wala asiwe na upendeleo na ikibidi, afuate nyayo zangu naamini kuwa bunge litakuwa na heshima kubwa," alisema Sitta.

Mbunge huyo wa Urambo Mashariki alisema Bunge la Kumi lina wasomi wengi ambao wengi wao ni vijana na hivyo ni bunge bora kuliko yaliyotangulia.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo litakuwa na mijadala mizito yenye changamoto nyingi linalomlazimu Makinda kuwa makini zaidi katika majukumu yake.

Akizungnza kwenye ukumbi wa Spika baada ya kuanza rasmi kazi hiyo, Makinda alisema hatatumia nafasi hiyo kumsafisha mtu yeyote anayetaka kugombea urais kama watu wanavyodai.

Pia alisema kuwa hajawekwa kwenye uspika na mafisadi, ila alisimama mwenyewe kwa kuwa aliamua kugombea nafasi hiyo.

"Kuwa spika ni ratiba ya maisha yangu, ni kitu ambacho nilikuwa nakifikiria na mimi ni mtu wa kufuata taratibu. Kwanza sijui kama kuna mafisadi kwa kuwa fisadi ni mwanaume anayeiba mke wa mtu," alisema Makinda.

Kuhusu uendeshaji wake wa bunge alisema kuwa hatakubaliana na hoja za kukomoana bali atahitaji hoja zilizofanyiwa utafiti ili maamuzi yanapotolewa yaweze kuleta tija.

Alisema siasa si za kuzua maneno tu lazima hoja ziwe za kitafiti na ni lazima wabunge wawe na uwezo wa kuibua mambo ili kazi iwe nzito.

"Nasikitika kuwa bunge lililopita lilikuwa na hoja nzito moja tu ya Richmond, zilitakiwa ziwe zaidi ya kumi kama hizo ili bunge liwe na nguvu zaidi,"alisema Spika huyo ambaye katika bunge lililopita alikuwa Naibu Spika akimsaidia Sitta.

Makinda alisema katika bunge hili atatoa kipaumbele kwa huduma za wabunge na wafanyakazi wa bunge kuwa bora zaidi na kutoa elimu kwa wabunge iliwaweze kuzielewa kanuni vizuri.
 
Back
Top Bottom