hili jimbo ni tajiri sana ila huyu mama kashindwa kuwainua watu wake chadema msilaze damu
Kusema ukweli wilaya ya Same ina utajiri mkubwa sana, na watu wake ni wachapakazi sana. Miaka ya nyuma walikuwa wanaitwa wachina wa Tanzania. Ukitaka kuuelewa utajiri wa wilaya hii usiangalie chini (bondeni) kama mji wa Same ambao mara nyingi unasumbuliwa na ukame. Hata mji wa Same ukame wake unatokana na kuharibika kwa pump za visima vilivyokuwepo tangu miaka ya 60-70. Maji yapo mengi chini ya ardhi, visima vya kutosheleza upatikanaji wa maji safi na salama vipo, pump zimeharibika na hakuna mwenye mpango wa kuzitengeneza au kufunga pump zingine!
Utajiri wa wilaya ya Same uko milimani, maeneo yote ya juu milimani yana mvua nyingi na rutuba inayoweza kulima au kuotesha mazao mengi kama mahindi, ndizi, mihogo, iliki, tangawizi, kahawa n.k. Wapare walijenga barabara zao kupanda milimani kwa nguvu zao wenyewe, walipasua miamba kwa kuwasha moto kwenye miamba na baadaye kumwagia maji ya baridi. Maji huko milimani ni mengi yanamwagika na kilimo cha umwagiliaji kilikuwa kimeendelea sana miaka ya nyuma. Kuna tabia moja ya wapare nilikuwa ninaipenda na niliona ingefaa kuwa mfano wa kuigwa, ni ile ya kufanya kazi kwa pamoja, wenyewe wanaiita 'msaragambo'. Siku hizi sidhani kama inaendelea. Siku ya 'msaragambo' taarifa ilikuwa inapitishwa vijiji vyote, na kila mtu mwenye nguvu (sio mgonjwa au mzee) alipaswa kushiriki. Ilikuwa ni kujenga shule, kutengeneza barabara, kufyeka misitu n.k.
TATIZO:
Wapare tofauti na watani wao wachagga, ni watu wanoogopa sana mamlaka (authority). Kwa mantiki hiyo, kukiwa na kiongozi mbovu au asiyeweza kuwapa maelekezo yanayofaa, ile ari ya kujituma kufanya kazi inakosa msimamizi. Na hili ndilo lililotokea huko Same, na si Mashariki peke yake, bali hata Same Magharibi kwa mbunge David Mathayo. Shida za maji, ubovu wa barabara, uharibifu wa mazingira, ukame na uhaba wa vyakula vyote sasa vimekuwa hali ya kawaida sana.
Ninaamini majimbo hayo yako wazi kabisa na tayari kwa mabadiliko. CDM amkeni sasa mjizatiti mtaichukua Same yote!
Acheni Mama Kilango aendelee kuota ndoto za Alinacha!