Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Status
Not open for further replies.
Kweli Dowans itawang'oa CCM, khaaaaaah yaani ukisoma labda uwe na kilema cha akili lakini kila kitu kipo wazi.
 
ccm kwishney, tunachotakjiwa ni kujiandaa tu kuchukua nchi taratibu....tena kwa raha zetu
the house which is devided itself can not with stand.
 
Natabiri: Anguko la CCM ni DOWANS!!! Kila nikipiga taswira yangu naona ni hivyo tu. CCM haifiki 2015, itafia mikononi mwa JK ambaye anashindwa kuithibiti kwa sababu mafisadi wameishika, na pia wamemshika barabara -- hafurukuti.

Baraza la mawaziri patawaka moto -- na Sitta hatakuwa peke yake, hiyo ninayo hakika. Anaonyesha ujasiri mkubwa kwa yeye waziri kusema malipo ya Dowans ni wizi tuuu. Nasikia mawaziri wengi tu wana msimamo kama huo. Hakika ni wizi.

Hebu fikiria alivyosema Ngeleja kwa mfano: Eti hatimaye wamegundua kutoka Brela kuwa wamiliki wa Dowans ni fulani na fulani na fulani... That's nonsense!

Yaani serikali iliingia mkataba na Dowans, na msururu wa yote yaliyotokea pamoja na kesi hii, siku zote haikuwa inajua wamiliki wa Dowans -- hadi juzi tu baada ya hukumu ya ICC kutolewa? Jamani, mawaziri wa JK mbona ni vichekesho sana?

Watz wote siyo mabwege kama wanavyofikiria, na nina hakika kuna wakubwa katika serikali hawaipendi hii kitu.

Anguko la CCM ni Dowans... you have to believe me.




Kweli?
sio kwamba ndo wana make more money ili waweze kulipa hata viongozi wao ambao kuwalipa imekuwa taabu kwa sasa?
Huoni kuwa pesa hizo zita wasaidia kujijenga kuelekea 2015?
 
dowans.jpg
 
Kwastaiki hii tuombe Mungu atuepushietu hili balaa maana huku tuendako!!!!!!!! Sipati picha.
 
Mke wa jamaa yangu amejifungua jana mtoto wa kiume amemeamua kumuita mtoto wake DOWANS kama kumbukumbu ya kihistoria
 
t Hata mimi muuza kahawa naona longolongo iliyo uchi!; najiuliza hivi hawa dowans hiyo kazi ya kufua umeme;
1- waliiomba au waliombwa waifanye?
2-kama ndivyo hao dowans waliomba hiyo zabuni walimuomba nani na kwa nani walipeleka maombi yao!
3-kama waliombwa nani aliwaomba hawa dowans kazi ya kufua umeme!
4-na ni nani aliridhia huo mkataba!
Haya ni maswali ya muuza kahawa jameni!

t
 
Wenyewee 30 Octoba mliichagua CCM irudi madarakani sasa inatukaba koo kulipa gharama za uchaguzi through Dowans...
 
mkulowaziri.jpg
Finance and Economic Affairs minister Mustafa Mkulo.

By Sylivester Ernest
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Treasury does not have funds to pay the Sh91 billion compensation that Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) owes controversial private power firm Dowans, Finance and Economic Affairs minister Mustafa Mkulo said yesterday.

Mr Mkulo told The Citizen in a telephone interview from his Kilosa constituency that the matter was being handled by the Energy and Minerals ministry.
Mr Mkulo said the Finance ministry had no plans to include the compensation in the national budget.

“I can’t say more as I’m on leave…however, that is their (Energy and Minerals) burden and they should find the means from their ministerial budget,” he said.

The Citizen had sought to know whether the money would be set aside in the 2011/12 Budget to be tabled in Parliament in June or if Treasury has extra funds to settle such debts.

Meanwhile, former National Assembly Speaker Samuel Sitta, who now is the East African Cooperation minister, said the decision to pay Dowans had not gone through the Cabinet.

Mr Sitta said he would seek an explanation over the matter when the Cabinet convenes, adding that there were some unanswered questions.

Mr Sitta, who was the Speaker when a parliamentary committee investigated Dowans’ predecessor, Richmond Development Company, over the $172 million emergency power supply scandal, said it was “painful” to pay the amount.

The minister said he believed Mr Ngeleja and Attorney General Frederick Werema would have something to tell the Cabinet since all the announcements they were making had not been discussed by ministers.
“They will have to tell us…t is very serious. We have not discussed the matter collectively and made a decision to pay up,” he said, adding that he was commenting as a responsible citizen, knowing the issue was outside his docket.

Yesterday Mr Ngeleja could not be reached for reaction even as anti-corruption activists and other political leaders said they were surprised at the manner in which the Dowans saga was being handled within government.

In a swift reaction, Civic United Front (CUF) national chairman Prof Ibrahim Lipumba called on all involved government officials, irrespective of where they sit, to resign, saying they have insulted the intelligence of Tanzanians.

“As far as I am concerned, the buck stops with the President…it is a pity that he is just sitting and watching this happen. Our beautiful country is now going like a rudderless ship,” said Prof Lipumba.The renowned economist said the country had no such money to waste and that it would be a pity to pay it while it could have been spent on other developmental activities.

The executive director of Concern for Development Initiatives in Africa (FORDIA), Mr Bubelwa Kaiza, said the government would not escape blame despite releasing the names of Dowans owners.

“The way this thing has been going leaves no doubt that some government officials are owners….why were they quiet for that long? Why are they taking this matter so lightly?” he queried. He said poor taxpayers would be overburdened with the debt.

The executive secretary of the non-governmental organization Agenda Participation 2000, Mr Moses Kulaba, said the naming of the owners of the company was pity and could not mean there were no shareholders of the company in the Tanzanian government.

Mr Ngeleja on Thursday announced that the government would pay the compensation as ordered by the international trade tribunal following a contractual dispute between Dowans whose contract was ended by Tanesco in 2008.
 
Japo sisomei sheria naona sinema ya dowans imefika patamu'maswali magumu ni kwann jk yuko kimya up to now'kwanini ngeleja anatumia force lazima tuilipe kampuni hewa mnakumbuka siku anayotaja majina alikuwa acheka alimaanisha nn kwenye kitu muhimu kama kile'kwa pinda kwanini hakufata mapendekezo ya kamati maalumu ya bunge'ngoja tuendelee kusubiri lakini ni wakati mzuri wa wanasheria kuchanga karata lazima watu watolewe ili tanganyika isonge
 
Pinda M, atakipata kilicho mpata Lowassa E, according to the doctrine of VICARIOUS LIABILITY.
Ukiwashwa vizuri moto huu wa Dowans Bungeni, Pinda itatakiwa kuwajibika kwa kujihuzuru wadhifa wake. Kwanini yeye anatetea malipo ya Dowans? Kwa waziri wa wizara ya nishati na madini anatetea ulipwaji kinyemela kwa Dowans? Hapa kuna kitu!
 
Pinda M, atakipata kilicho mpata Lowassa E, according to the doctrine of VICARIOUS LIABILITY.
Ukiwashwa vizuri moto huu wa Dowans Bungeni, Pinda itatakiwa kuwajibika kwa kujihuzuru wadhifa wake. Kwanini yeye anatetea malipo ya Dowans? Kwa waziri wa wizara ya nishati na madini anatetea ulipwaji kinyemela kwa Dowans? Hapa kuna kitu!

nashukuru kwa mchango wako
 
Kwa nchi iliyomakini, siku moja tu baada ya Ngeleja kuitisha ile conference tayari angeshajiuzulu, lakini kwa hapa kwetu swala la kujiuzulu sahauni.
Yale yaliyomkuta Lowasa na mawaziri wake ilikua ni accident tu hakukua na jinsi lakini walikuwa tayari kwa gharama zozote zile waendelee kukalia viti vyao.
 
Waziri Mwakyembe amesema kidogo kuhusu DOWANs na anaungana na Mheshiwa Sita katika sakata la serikali kuilipa DOWAN

Kwa maana hiyo inaonyesha mawaziri wa JK hawana mawasiliano kila mmoja ana lake na serikali kuu inapuuza maswala muhimu yanayohusu taifa letu maana wametoa tamko la kuilipa dowan bila hata ya kuwashirikisha baraza la mawaziri

sasa waJF tutafika kama kila waziri anafanya kazi kifyake na serikali kuu nikimaanisha JK & PM wanaamua tu na wizara husika mambo yanaenda?

Kuna tatizo hapa kwa mawaziri kutofautiana na hii inamdhalilisha rais aliyewateua
 
Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amevunja ukimya kuhusu sakata la kutaka kulipwa fidia ya mabilioni ya Shilingi kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans Tanzania Limited, kwa kueleza kwamba itakuwa jambo la ajabu kama serikali itakubali kulipa fedha hizo, kwani kampuni hiyo awali ilibainika kuwa ya kitapeli, lakini sasa inaonekana kuwa ni halali.

“Tulishasema kuwa Richmond ni kampuni hewa ambapo Dowans wamerithi mkataba hewa, hivyo inakuwaje walipwe tena mabilioni ya fedha, tunasubiri kuona msingi uliotumika tapeli kulipwa fidia kwa kazi ya utapeli, nitaangalia amelipwa kwa sheria ipi,” alisema Dk. Mwakyembe jijini Dar es Salaam jana.

Dk. Mwakyembe ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza mchakato wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond Development LLC, alitoa tamko hilo katika mahojiano maalum na NIPASHE ofisini kwake, baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu tangu itolewe hukumu hiyo ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi (ICC) na kulitaka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuamuriwa kuilipa Dowans Sh. bilioni 94..
Alisema suala la kutaka kuilipa Dowans lina sura mbili, sura ya kisiasa na sura ya kitaalamu.

Alisema katika sura ya kitaalamu yeye kama mwanasheria ambaye amekuwa katika fani hiyo kwa zaidi ya miaka 20, anasubiri kwanza hukumu hiyo isajiliwe na itatoa fursa kila Mtanzania kuyasoma na kuyaelewa yaliyomo ndani.

Dk. Mwakyembe alisema kama mwanasheria, anatilia mashaka na kuzua maswali mengi hukumu hiyo kwa sababu haiwezekani kampuni iliyoonekana mwanzo kuwa ni ya kitapeli leo inaonekana halali.

“Mimi ni mwalimu wa sheria wa siku nyingi na nimekuwa kwenye fani hii kwa zaidi ya miaka 20, kwa hiyo nasubiri kwa hamu usajili wa hukumu hiyo ya ICC ili nione ni sheria ipi iliyotumiwa na wanasheria, tapeli kulipwa fidia kwa kazi yake ya utapeli,” alisema Waziri Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alisema baada ya kusajiliwa kwa hukumu hiyo, pia ana dukuduku la kutaka kujua ni vipi Tanzania imepoteza kesi rahisi kama hiyo ambayo hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Shahada ya Sheria angeweza kuiendesha na kushinda.

“Nina dukuduku kutaka kujua ni vipi tumepoteza kesi rahisi kama hii ambayo hata mwanafunzi wangu wa mwaka wa kwanza wa digrii ya sheria nina uhakika angeshinda kwa sababu Bunge lilishatafuna kila kitu,” alisema.

Alisema kama serikali itaingia mkenge kulipa mabilioni hayo ya fedha, ipo katika hatari ya kuingizwa katika kesi iliyofunguliwa Marekani ambayo Dowans wameshitakiana na Richmond kutokana na kung’ang’ania mtambo mmojawapo wa kuzalisha umeme.

Alisema kesi hiyo kati ya Dowans na Richmond ipo katika Mahakama ya Wilaya ya Kusini (The United State District Court for the Southern District of Texas Houstorn Division) ambapo zipo tetesi kuwa Tanzania itakapolipa fedha hizo itajumuishwa kwenye kesi hiyo ya kugombaniana mitambo.

“Dowans na Richmond wameshitakiana Marekani kwa kung’ang’ania mtambo GE TM2005 S/N 481-364,7LM 2005-PE-MDW GE UNIT ID.W/O 601178, sasa zipo tetesi kwamba Tanzania inasubiliwa kuingizwa katika kesi hiyo itakapokubali kulipa fedha hizo,” alisema.

Alisema hatua ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, kueleza kwamba serikali imeamua kuilipa fedha Dowans, ameufanya haraka kwa sababu angesubiri kwanza hukumu hiyo isajiliwe.

Aliongeza kuwa kama serikali itakubali kulipa fidia hizo, kutakuwa kuna utata kwa sababu majina ya waliotajwa kuwa ni wamiliki wa Dowans Tanzania Limited, lakini wale wa Dowans Holding SA (Costa Rica) hawajulikani na wala hawana anuani ya posta wala simu nchini.

Alisema anayetajwa pekee kuwa mmiliki wa Dowans Holding SA ni Bernal Zamora Arase ambaye hata hivyo, ana makampuni 100 yanayoishia na SA.

“Huyu Bernal Zamora Arase anayetajwa kuwa mmiliki wa Dowans Holding SA hana simu, ofisi wala anuani ya posta, nyumba ya kuishi, gari wala pikipiki hapa nchini,” alisema Dk. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa Watanzania wengi bado wanafahamu kuwa chini ya makubaliano, mali zote za Richmond bado hazijahamishiwa Dowans na hivyo wanalipwa pesa kinyemela na wameshitakiana Marekani.

Naibu Waziri huyo akizungumzia katika sura ya kisiasa kuhusiana na sakata la Dowans, alisema wasemaji wakuu ni Spika wa Bunge, ambaye Bunge lake lilipitisha maazimio 23 mwaka 2008 ambapo kati ya maazimio hayo ambayo yalihukumu Richmond kuwa ni kampuni hewa.

Alisema Bunge hilo pia lilienda mbele zaidi kwa kuagiza kutaka ifutwe kwenye orodha ya makampuni halali Tanzania ambapo Oktoba 2008 Richmond ilifutwa kama kampuni isiyo halali.

“Kimsingi, mwenye mamlaka ya kuelezea hatma ya maazimio 23 yaliyotolewa na Bunge ni Spika wa Bunge la Tanzania, kwa sababu hukumu ya ICC imegusa baadhi ya maadhimisho,” alisema.

Dk. Mwakyembe alisema pia Waziri Mkuu ambaye kikatiba ni msimamizi mkuu wa shughuli za Bunge na serikali hivyo ana imani baada ya kupokea ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali atakuwa na kauli yake ya mwisho.
 
Matumizi matumizi ya colon ':' katika kichwa cha habari yametumika vibaya. ':' katika kichwa cha habari inatumika kuelezea kuwa maneno ya mwanzo kabla ya ':' yamesemwa na mtu/chombo/taasisi iliyowekwa baada ya ':'.Vile vile kuelezea maana zaidi ya neno,neno baada ya colon linaelezea maana ya neno kabla ya colon au neno baada ya colon ni subtitle ya neno kabla ya colon

Matumizi hayo ni kama ;
Dowans hawastahili kulipwa : Sitta

Hii inaonesha kuwa Mheshimiwa Sitta amekaririwa akiongea maneno hayo. Sentensi "Waziri Mwakyembe atikisa misuli Dowans" haijatamkwa na Nipashe wala haiendani na matumizi niliyoyaelezea hapo juu ya colon ,bali chanzo cha habari ni Nipashe kwa hiyo kichwa cha habari hakikutakiwa kiwe kama ulivyoandika bali kama nilivyoandika.

Unapotaka kukariri kuwa habari fulani inatoka katika chombo fulani cha habari basi andika habari kama ilivyo na halafu chini uandike mfano ,Chanzo : Nipashe au Source : Nipashe

Alamsiki
 
Kikwete ana kazi kwa kuwa mawaziri sasa wapingana wenyewe kwa wenyewe na kuna uwezekano hii serikali ikaangukia pua bungeni.Sisi tusubiri yetu macho.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom