Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Anguko kuu la Kikwete na CCM, dalili zimeanza

Status
Not open for further replies.
Mods kuna threads nyingine kama hii,naomba hizi threads ziunganishwe ,First Come First Saved
 
Kamati teule ya bunge iliyoundwa 13/nov/2007 ilithibitisha kuwa RICHMOND ni kampuni hewa.kimsingi utakuta hata umiliki uliohamishiwa RICHMOND kwenda DOWANS pia haupo ama si halali. baada ya kubainika hapo , serikali hii hii unashangaa KWA NINI HAIKUTAIFISHA MALI ZA RICHMOND, wakati huo baada ya kubainika hilo.sasa kama DOWANS haikurith kihalali mali za RICHMOND, serikali ituambie kabla ya kuwalipa wapi ulipo uhalali wa madai ya kampuni isiyokuwa halali..........?
 
Kutokulipwa au Kulipwa kwa Dowans, hakutasaidia kitu, Sababu wezi bado wapo na wataendelea kuchota (what happened to pesa za EPA?).

The bigger and more important problem is to find who are responsible na kuhakikisha hawa watu wanawajibishwa na wanakuwa mfano kwa todays vibaka who will be tommorrows FISADIS

Hivi kweli hatuwajui wamiliki wa DOWANS, hivi hata kama hatuna concrete proofs hatuwezi kuwaweka hatiani hawa watu kwa kosa la kuhujumu uchumi?

SITTA et al wamekuwa wakiwataja hawa watu bila kuchukua any actions... huu umekuwa kama wimbo daily and nothing is done..... tukumbuke kuwa "An Ounce of Action is Worth a Ton of Theory"

Jamani the SYSTEM has got CANCER and to cure this CANCER we need to cut some of the organs.... and not paying Dowans haitamaliza hiyo CANCER na itaendelea kuumaliza mwili wetu ambao ni TANZANIA.... Thank God we know about Dowans ila kuna magapi hatujui.....?
 
In TZ government, is there anyone so wise as to learn by the experience of others?

 
In TZ government, is there anyone so wise as to learn by the experience of others?


Ninawalaumu viongozi ambao kila siku wanalalamika kuhusu hawa watu lakini hakuna action wanayochukua..... am sure if the Late Sokoine angekuwepo asingehitaji proof.... "Tupa wote ndani kwa kuhujumu Uchumi"
 
Dowans wakubuhu wizi


picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa 05 January 2011

dowans_123.jpg



VIGOGO ndani ya serikali wanatuhumiwa kupanga njama za kutaka kuilipa kinyemela mabilioni ya shilingi kampuni ya Dowans, kabla taratibu muhimu kuhitimishwa.

MwanaHALISI lina taarifa kuwa Dowans Tanzania Ltd., imewasilisha ankara zake Hazina, tayari kwa malipo kabla maamuzi kusajiliwa mahakama kuu.

Wakati taarifa hizo zikivuja, umetokea utata wa kampuni ipi hasa ya Dowans ilipwe, kwani kuna makampuni mawili yaliyojitokeza.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) ndiyo ilikuwa na mkataba na Tanesco kupitia kurithi mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Bali uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya Biashara (ICC) wa 15 Novemba 2010, unaagiza Tanesco kulipa Sh.185 bilioni kwa makampuni yote mawili.
Makampuni hayo ni Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Dowans Tanzania Limited.

Utata huo unaongezeka kwa vile wakati wote wa mgogoro wa Richmond na Dowans, hakukuwa na Dowans Tanzania Limited ambayo sasa imetinga katika maamuzi ya ICC.

Nayo kampuni ya Dowans Holdings SA (Costa Rica), hata hivyo iliwahi kutajwa na msajili wa makampuni nchini Costa Rica kuwa haijawahi kusajiliwa nchini humo.

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja wiki mbili baada ya gazeti hili kuripoti kuwa Dowans ni mradi wa vigogo watatu wakubwa ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka ndani ya serikali zinasema, mpango wa kulipa makampuni hayo unasukwa kwa ustadi mkubwa na watumishi wawili –mmoja kutoka wizara ya nishati na madini na mwingine ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali (AG).

Alipoulizwa Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo kuhusu njama za kutaka kulipa Dowans kinyemela alisema, "Hapa ninapozungumza na wewe niko Kilosa. Sina taarifa za karibuni za ofisini." Mkullo alikana pia kujua iwapo Dowans wamewasilisha ankara kwa ajili ya malipo.

Kwa mujibu wa sheria za usuluhishi nchini na zile za kimataifa, uamuzi wa ICC sharti usajiliwe katika mahakama kuu ya Tanzania.
Aidha, kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo katika mkataba kati ya Dowans Holdings SA (Costa Rica) na Tanesco, yote yaliyokubaliwa ndani ya mkataba yatafuata sheria za Tanzania.

Hata hivyo, taarifa zinasema, msukumo wa kutaka malipo hayo kufanywa kinyemela, umefuatia kutajwa katika mwenendo wa kesi, mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

"Hapa kuna kitu kinafichwa. Rostam hataki kesi hii isajiliwe hapa, maana jina lake limetajwa ndani ya kesi hii zaidi ya mara tatu. Hivyo anajua kuwa iwapo itasajiliwa ataumbuka," ameeleza ofisa mmoja wa serikali.
Naye mjumbe mmoja wa Bodi ya Tanesco aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini amethibitisha kuwa ankara za madai ya Dowans tayari zimewasilishwa serikalini kwa hatua zaidi.

"Bodi ya Tanesco iliarifiwa jambo hili katika kikao chake kilichofanyika 21 Desemba 2010, na kila mmoja alishtuka," ameeleza mtoa taarifa.
Alisema, "…wanaleta ankara za madai hata kabla mahakama kuu haijasajili kesi yao? Hapana! Tukasema, sisi bodi hatuwezi kuidhinisha malipo haya…"

Kutajwa kwa Rostam katika shauri la Dowans kulifuatia kubanwa na majaji wa mahakama hiyo, mfanyakazi wake mmoja kutoka kampuni ya Caspian.

Mfanyakazi huyo aliyekuwa anahudhuria bila kukosa vikao vyote vya mahakama vilivyokuwa vikifanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, alieleza mahakama, "…niko hapa kufuatilia maslahi ya bosi wangu."

Mtoa taarifa anasema, "Yule bwana aliulizwa na wale majaji, mbona kila siku anaingia mahakamani na hatoki mpaka muda wa kesi unamalizika."
Anasema, "Ndipo yule kijana akajibu, ‘nimetumwa na bosi wangukumwakilisha.'" Mahakama ikataka kujua huyo bosi ni nani? Ndipo akamtaja Rostam," anaeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.
Anasema mara baada ya kutaja jina la Rostam, majaji waliokuwa wanasikiliza shauri lile, haraka wakauliza, ‘Kwani Rostam ni nani katika Dowans?' Yule bwana akajibu, ‘Ni mwanahisa…'"

Kuna taarifa za kuaminika kuwa mmoja wa watu wawili waliosaini makubaliano ya kuhamisha mkataba kutoka Richmond kwenda Dowans, ni Henry Surtees, Mwingereza anayedaiwa kuwa mtumishi wa kampuni ya Rostam ya Caspian.

Wiki iliyopita, gazeti la kila siku la Mwananchi lilimnukuu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema akisema, Dowans ilisajiliwa nchini Costa Rica na Rostam ndiye aliyepewa nguvu ya kisheria kusimamia malipo hayo.

Werema hakuzungumzia kwa undani hatua ya wanaojiita wamiliki wa Dowans kumpa Rostam nguvu hizo za kisheria.
Tarehe 7 Februari 2008, Rostam alikana kumiliki aina yoyote ya hisa kwenye kampuni mbili – Dowans na Richmond.

Mmoja wa wanaotajwa kuwa wamiliki wa Dowans katika nyaraka za sasa zilizopo ofisi ya usajili wa makampuni (BRELA), Brigedia Jenerali Sulaiman Mohamed Yahya Al Adawi amekana mara kadhaa kuifahamu kampuni hiyo.

Naye raia wa Canada, Andrew James Tice anayeonekana katika nyaraka za sasa za BRELA, aliwahi kuwa meneja uzalishaji katika kampuni ya Songas na baadaye kushika nafasi hiyo katika kampuni ya Richmond.
Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali ambazo gazeti linazo, Tanesco na Dowans wamekubaliana kuwa maamuzi yoyote ya suala hilo, ni lazima yafuate sheria za Tanzania.

Ibara ya 14 ya mkataba wao inasema pamoja na suala hilo kufikishwa ICC, pale ambapo kutatokea mgogoro, bado sheria za ndani ya Tanzania zitatumika wakati wa kufikia utatuzi.

Ibara ya 17 ya sheria ya usuluhishi inasema, mara baada ya maamuzi husika kutolewa, yatasajiliwa na mahakama kuu na baada ya hapo itachukuliwa kuwa ni amri halali ya mahakama ya nchi.

Nchini Costa Rica, ambako Dowans inadaiwa kusajiliwa, hakuna rekodi zozote inazoonyesha kuwapo kwa kampuni hiyo. "Dowans si kampuni halali ndani ya Costa Rica," inasema barua kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali nchini Costa Rica.

Barua hiyo ilisainiwa na Marianela Jimenez, Jumamosi ya 3 Agosti 2008 na kutumwa ofisi ya katibu wa Bunge la Jamhuri, saa 11:09 jioni ya siku hiyo.

Mmoja wa wanasheria nchini ameliambia gazeti hili kuwa serikali haistahili kulipa hata shilingi kwa Dowans kwa kuwa kampuni hiyo ilinunua mkataba kutoka kwa kampuni feki – Richmond.

Amesema, "Hata hatua ya Dowans Holding kuingiza kampuni ya Dowans Tanzania Limited katika madai yao, wakati wakijua fika kwamba kampuni hiyo siyo iliyosaini hati ya kuhamisha mkataba, ni kinyume cha taratibu na sheria za makampuni."

Kampuni ya Dowans ilirithi mkataba kutoka kampuni nyingine yenye utata ya Richmond ambayo ilipewa kazi ya kufua umeme kuanzia Januari 2007 hadi Juni 2008.
 
Dowans ni chuma ulete wa ikulu?


4416b987ae0e48879f6e6e4c8aec6895

Na Joster Mwangulumbi - Imechapwa 05 January 2011

Wazo Mbadala


HERI ya Mwaka Mpya wapenzi wasomaji wa safu hii ya Wazo Mbadala inatolewa wakati bei mpya ya umeme imeanza.
Katika salamu zake za Mwaka Mpya, Rais Jakaya Kikwete, alikomalia wananchi wakubali maumivu ya bei mpya zilizopitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kufuatia maombi ya Tanesco.
Rais anasema bei hiyo mpya ni kwa maslahi ya kibiashara au kiuchumi. Hapa rais ameficha ukweli.
Ukweli ni kwamba serikali yake ilipandisha bei ya umeme ilipotengeneza nyoka mfano wa ‘chuma ulete’ aitwaye Richmond ili kufyonza fedha za Watanzania masikini.
Hivi sasa ‘serikali ya Kikwete’ inachungulia namna ya kupokea Sh. 185 bilioni kama fidia ya ‘chuma ulete’ Dowans eti imeshinda kesi ilipozuiwa kufyonza fedha kupitia mkataba feki wa Richmond ambao iliruhusiwa kuurithi.
Rais anathubutuje kuzungumzia bei mpya bila ya kugusia athari za fidia hii? Je, huu si ushahidi wa kimazingira kwamba anahusika?
Mazingira ni haya: nyoka akiingia ndani ya nyumba, kimbilio la watoto na mama huwa kwa baba yao; kama hayuko mbali basi watatimua mbio kumfuata au kumtwangia simu arudi haraka kupambana na nyoka.
Watoto wanajua kwamba baba yao ana uwezo, mbinu na mikakati ya kumtoa nyoka bila kusababisha madhara kwa familia.
Lakini kama baba ataingia ndani ya nyumba na kupiga usingizi huku nyoka akionekana kuranda vyumbani na watoto wakiwa nje, familia yake itakuwa na jibu moja tu – kumbe baba ndiye mmiliki wa nyoka huyo.
Au kama baba ataonekana kukwepa kujadili tatizo au ugonjwa unaoathiri familia yake au anakataa kumpeleka mgonjwa hospitali au kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kumpatia tiba, basi baba moja kwa moja ndiye mhusika wa ugonjwa huo.
Baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Mwanasheria Mkuu Frederick Werema na Waziri wa Afrika Mashariki Samuel Sitta kutoa maoni yanayotofautiana kuhusu uhalali wa fidia kwa chuma ulete Dowans, masikio ya Watanzania yalibaki kwa ‘baba yao,’ Rais.
Sasa akakwepa. Hakuelezea. Badala yake, akakomalia watu walipe bei mpya. Jamii inamtilia shaka baba kwamba ameridhia chuma ulete Richmond/Dowans.
Haiwezekani katika mazingira haya, wananchi wajadili kwa miaka minne, kwa hisia kali, halafu Rais anakwepa na anaingia Ikulu kupiga usingizi!
Anathubutuje kulala kwa raha zake, wakati Richmond/ Dowans imeitikisa nchi na kusababisha anguko la kisiasa kwa msaidizi wake mkuu na rafiki yake mkubwa, Edward Lowassa? Kikwete anaamini Lowassa ameridhika?
Au zilikuwa mbinu za kifisadi kwamba mradi huo wa kifisadi ukijulikana “mmoja ajiuzulu na tuseme hiyo ni ajali ya kisiasa?”
Kamati Teule ya Bunge iliyokuwa chini ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe ilitumia mabilioni ya shilingi kwa safari ya Marekani kuchunguza nyaraka muhimu na kuhoji watendaji wakuu.
Kamati hiyo ikawasilisha ripoti yake, lakini haikumtaja mmiliki isipokuwa ilisema ni kampuni feki na kwamba serikali iliingia mkataba wa kufua umeme na kampuni feki.
Mjadala ulipopamba moto na kamati hiyo kurushiwa tuhuma kuwa ililenga kuchafua watu, Dk. Mwakyembe alisema wako radhi kueleza hata mambo waliyoyaacha ambayo yangeikomoa serikali.
Je, nani aliokolewa? Hii ndiyo sababu Dk. Mwakyembe kazibwa mdomo kwa kupewa uwaziri? Ndiyo sababu aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta naye kapewa uwaziri ili asiruhusu mijadala mikali bungeni?
Je, Kikwete atapuuza kwa kusema “…kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala usingizi” au atajifariji kwa kusema “mtapambana lakini hamtashinda?”
Gazeti toleo na. 223
 
Wananchi tumeelewa ila kwa mzee jk hakuna kitu. atasikia vp wakati kavaa earphone anakula bongo flava?
 
MMOJA wa mawakili mahiri wa kujitegemea nchini, Kennedy Fungamtama, ameiomba serikali na umma upuuze ushauri wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wa kutaka serikali kukataa kuilipa fidia ya sh bilioni 94 Kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, kwani ushauri huo unaweza kulidhohofisha taifa kwa kuliingiza katika matatizo makubwa.

Fungamtama aliyasema hayo juzi katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muda mfupi baada ya gazeti hili kupata taarifa kuwa wakili huyo ni miongoni mwa wanasheria walioisoma hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji (ICC).

Mwanasheria huyo ambaye alimuelezea Sitta kuwa mtu anayejaribu kucheza na akili za Watanzania, kwa sababu ya kutojua kwao undani wa hukumu ya ICC, alisema endapo serikali itakaidi kulipa fidia hiyo ni wazi taifa linaweza kukabiliwa na madhara makubwa mawili.
Alisema moja ya madhara hayo ni kwa wafadhili kuiweka nchi kwenye orodha ya kunyimwa misaada, kwa sababu ya kutoheshimu sheria na mikataba ya kimataifa ambayo imeridhia.
Wakili huyo alisema madhara mengini ni pamoja na wawekezaji kuingiwa na hofu ya kuja kuwekeza hapa nchini na kuongeza kuwa hilo likitokea taifa ndilo litakalopata hasara na si Waziri Sitta binafsi.

Fungamtama alisema amefikia uamuzi wa kuzungumzia jambo hilo baada ya kuisoma na kujiridhisha kwamba hukumu hiyo yenye kurasa 150 ya kesi namba 15947/VRO kati ya Kampuni ya Dowans na TANESCO ilipokewa na ICC Novemba 20, mwaka 2008 na ikatolewa hukumu Novemba 15 mwaka jana.

Alisema mkataba kati ya TANESCO na Dowans ulisainiwa Juni 23, mwaka 2006 na mkataba huo unajulikana kama ‘Power Off - Take Aggreement (POA)" chini ya kifungu cha 14 (e) cha POA, na kufafanua kwamba pande zote mbili katika mkataba huo zilikubaliana kwamba uamuzi wa Mahakama ya ICC ndio utakuwa wa mwisho na utazibana pande zote mbili na hautaweza kukatiwa rufaa.

Fungamtama alisema kifungu cha 14 (f) cha POA, kinasomeka: "The parties waive any right to challenge or contest the validity or enforceability of this arbitration agreement or any arbitration proceeding or award brought in conformity with this section."

Kwa tafsiri nyepesi, Fungamtama alisema kifungu hicho kinasema, TANESCO na Dowans katika mkataba wao walikubaliana kwa maandishi kuweka kando haki za kupinga au kuhoji mwenendo na tuzo zitakazotolewa na baraza la usuluhishi.

Alisema Waziri Sitta amenukuliwa na vyombo vya habari akitaka serikali itumie kifungu cha 16 cha Sheria ya Tanzania ya Usuluhishi Sura ya 15 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2002, kwamba serikali inaweza kutumia kifungu hicho kutengua hukumu ya mahakama ile ya kimataifa.
"Ni kweli Mahakama Kuu ya Tanzania imepewa mamlaka ya kutengua maamuzi yanayotolewa na mahakama za kimataifa endapo tu itadhihirika kuwapo kwa mambo mawili yafuatayo:
Moja; msuluhishi wakati akiendesha kesi alikuwa akiegemea na kupendelea upande mmoja (arbitrator has miss - conducted himself. Pili: Mazingira ya kufikia uamuzi ule yalitawaliwa na rushwa au shauri lilifikishwa mahakamani bila kufuata taratibu za kisheria (an arbitration or award has been improperly procured).


"Hayo ndiyo mambo mawili peke yake yanayoweza kusababisha Mahakama Kuu ya hapa nchini kutengua hukumu zilizokwisha kutolewa na mahakama za kimataifa za usuluhishi na si kwa jambo jingine lolote.

"Sasa kama Sitta ana ushahidi, vigezo hivyo viwili vya kisheria katika lililokuwa shauri baina ya Dowans na TANESCO kwamba wasuluhishi wale ambao ni majaji waliipendelea Dawans, au walikura rushwa, ingekuwa ni vyema haraka apeleke ushahidi huo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kuwatuma wanasheria wake wakafungue kesi Mahakama Kuu ili iweze kutengua hukumu hiyo kupitia huo ushahidi wake kama anao na si kama anavyofanya hivi sasa kupayukapayuka kwenye vyombo vya habari," alisema wakili huyo.
Aidha, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha jedwali la 3 katika Sheria ya Usuluhishi ya Tanzania, Sura ya 15 ya mwaka 2002 kinasomeka hivi:
"Each contract state undertakes to ensure the execution by its authorities and in accordance with the provisions of its national laws of arbitrarily awards made in its own territory under the preceding articles".


"Kwa tafsiri rahisi, kifungu hicho utaona tayari nchi imejifunga mikono na utekelezaji wa hukumu zinazotolewa na mahakama za kimataifa kwa sababu ni nchi yetu yenyewe imeridhia sheria na mikataba ya kimataifa."
Alisema kwa hiyo maelezo ya Waziri Sitta ya kutaka Dowans isilipwe, ni kutaka kuishawishi serikali na umma kukaidi kutekeleza maamuzi halali chini ya sheria na mikataba ambayo serikali iliiridhia kuitii na kuitekeleza.

Aidha, alisema jambo jingine lililojitokeza wakati kesi hiyo ikiendelea baina ya Dowans na TANESCO ni TANESCO walitaka kujua wamiliki wa Dowans ni kina nani na Mahakama ya ICC iliona hoja hiyo ya TANESCO ya kutaka kumjua mmiliki haina umuhimu wowote katika mgogoro uliokuwa mbele yao na ikatupilia mbali, kwa sababu iliona hoja hiyo haina maana yoyote mbele yao.

"Kwa hiyo kwa kitendo cha Waziri Sitta kulianzisha suala hilo la kutaka kujua wamiliki wa Dowans wakati hoja hiyo tayari ilikwishatolewa uamuzi na ICC, kisheria hawezi kulianzisha tena jambo hilo la kutaka kujua wamiliki kwa njia anayoitumia ya vyombo vya habari.

"Kwa hiyo maelezo yote yanayoendelea kutolewa kuhusu hukumu hiyo ni kutaka kujinasua katika lawama wakati yeye na baadhi ya maswahiba zake enzi zile akiwa Spika wa Bunge ndio waliokuwa chanzo cha TANESCO kuvunja mkataba na Dowans, hivyo mwisho wa siku shirika hilo la umeme kujikuta likiburuzwa katika korti ya ICC.

"Na ifike mahala wananchi na vyombo vya habari na serikali itoke usingizini na ijiulize maswali yafuatayo kwamba Sitta hakuwepo kwenye usikilizwaji wa shauri hilo? Sitta hakuwa akijua kwamba TANESCO imefunguliwa kesi na Dowans katika Mahakama ya ICC?

"Kwa kuwa Sitta alikuwa mstari wa mbele kuzipiga vita Dowans na Richmond, ni wazi alikuwa akifahamu kwamba TANESCO imeburuzwa mahakamani na kama kweli Sitta ni mzalendo wa kweli na hana chuki binafsi katika hili ni kwanini hayo madai anayoyasema asingeiomba serikali imuweke kama shahidi wa upande wa TANESCO ili akatoe ushahidi anaousema kila kukicha kwenye vyombo vya habari?

"Amesubiri tayari shirika letu la umeme ambalo ndilo lilikuwa mdaiwa katika shauri hili limeshindwa kufurukuta kwenye kesi hiyo na tumetakiwa tulipe kiasi hicho kikubwa cha fidia ndiyo kila kukicha anazungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu hukumu hiyo, tena ukitazama maoni anayoyatoa utafikiri si mtu aliyesomea sheria kabisa….naomba sana hasa serikali ipuuze ushauri wa Sitta kwani ni wazi kabisa anataka kuliingiza taifa kwenye matatizo mengine makubwa.

"Watanzania na huyo Waziri Sitta ambao hawajaisoma hukumu ile naomba niwaeleze wazi mimi nimeisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya mara saba, kama taifa kupitia hukumu hiyo tumeshikwa pabaya, hivyo hatuwezi kukata rufaa, isipokuwa tu kama tutathibitisha sababu zile mbili nilizozitaja," alisema wakili Fungamtama.

Aidha, Fungamtama aliviasa baadhi ya vikundi mbalimbali vya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuzungumzia hukumu hiyo ambayo hata wengine hawajawahi kuisoma wala kuiona, kwani tayari kuna baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiandika makala kwamba wakati kesi hiyo ikiendeshwa TANESCO haijawahi kuleta shahidi hata mmoja kutoa ushahidi.

Jambo ambalo Fungamtama alisema si kweli na linalenga kuhadaa umma, kwani majibu na nakala ya hukumu hiyo ambayo anayo inaonyesha TANESCO ilipeleka mashahidi watano na walitoa ushahidi wao.

Wakili huyo aliwataja mashahidi hao kuwa ni Subira Wandiba, ambaye ni Mwanasheria wa TANESCO, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Zabuni iliyotoa tenda kwa Dowans, Balozi Fulgence Kazaura, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Dk. Idrisa Rashid, Mhasibu Mkuu wa shirika hilo, Jamhuri Ngeline na Boniface Njombe.
 
MMOJA wa mawakili mahiri wa kujitegemea nchini, Kennedy Fungamtama, ameiomba serikali na umma upuuze ushauri wa aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wa kutaka serikali kukataa kuilipa fidia ya sh bilioni 94 Kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans, kwani ushauri huo unaweza kulidhohofisha taifa kwa kuliingiza katika matatizo makubwa.

Fungamtama aliyasema hayo juzi katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima yaliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ikiwa ni muda mfupi baada ya gazeti hili kupata taarifa kuwa wakili huyo ni miongoni mwa wanasheria walioisoma hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Kusuluhisha Migogoro ya Uwekezaji (ICC).

Mwanasheria huyo ambaye alimuelezea Sitta kuwa mtu anayejaribu kucheza na akili za Watanzania, kwa sababu ya kutojua kwao undani wa hukumu ya ICC, alisema endapo serikali itakaidi kulipa fidia hiyo ni wazi taifa linaweza kukabiliwa na madhara makubwa mawili.
Alisema moja ya madhara hayo ni kwa wafadhili kuiweka nchi kwenye orodha ya kunyimwa misaada, kwa sababu ya kutoheshimu sheria na mikataba ya kimataifa ambayo imeridhia.
Wakili huyo alisema madhara mengini ni pamoja na wawekezaji kuingiwa na hofu ya kuja kuwekeza hapa nchini na kuongeza kuwa hilo likitokea taifa ndilo litakalopata hasara na si Waziri Sitta binafsi.

Fungamtama alisema amefikia uamuzi wa kuzungumzia jambo hilo baada ya kuisoma na kujiridhisha kwamba hukumu hiyo yenye kurasa 150 ya kesi namba 15947/VRO kati ya Kampuni ya Dowans na TANESCO ilipokewa na ICC Novemba 20, mwaka 2008 na ikatolewa hukumu Novemba 15 mwaka jana.

Alisema mkataba kati ya TANESCO na Dowans ulisainiwa Juni 23, mwaka 2006 na mkataba huo unajulikana kama ‘Power Off - Take Aggreement (POA)” chini ya kifungu cha 14 (e) cha POA, na kufafanua kwamba pande zote mbili katika mkataba huo zilikubaliana kwamba uamuzi wa Mahakama ya ICC ndio utakuwa wa mwisho na utazibana pande zote mbili na hautaweza kukatiwa rufaa.

Fungamtama alisema kifungu cha 14 (f) cha POA, kinasomeka: “The parties waive any right to challenge or contest the validity or enforceability of this arbitration agreement or any arbitration proceeding or award brought in conformity with this section.”

Kwa tafsiri nyepesi, Fungamtama alisema kifungu hicho kinasema, TANESCO na Dowans katika mkataba wao walikubaliana kwa maandishi kuweka kando haki za kupinga au kuhoji mwenendo na tuzo zitakazotolewa na baraza la usuluhishi.

Alisema Waziri Sitta amenukuliwa na vyombo vya habari akitaka serikali itumie kifungu cha 16 cha Sheria ya Tanzania ya Usuluhishi Sura ya 15 kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2002, kwamba serikali inaweza kutumia kifungu hicho kutengua hukumu ya mahakama ile ya kimataifa.
“Ni kweli Mahakama Kuu ya Tanzania imepewa mamlaka ya kutengua maamuzi yanayotolewa na mahakama za kimataifa endapo tu itadhihirika kuwapo kwa mambo mawili yafuatayo:
Moja; msuluhishi wakati akiendesha kesi alikuwa akiegemea na kupendelea upande mmoja (arbitrator has miss - conducted himself. Pili: Mazingira ya kufikia uamuzi ule yalitawaliwa na rushwa au shauri lilifikishwa mahakamani bila kufuata taratibu za kisheria (an arbitration or award has been improperly procured).

“Hayo ndiyo mambo mawili peke yake yanayoweza kusababisha Mahakama Kuu ya hapa nchini kutengua hukumu zilizokwisha kutolewa na mahakama za kimataifa za usuluhishi na si kwa jambo jingine lolote.

“Sasa kama Sitta ana ushahidi, vigezo hivyo viwili vya kisheria katika lililokuwa shauri baina ya Dowans na TANESCO kwamba wasuluhishi wale ambao ni majaji waliipendelea Dawans, au walikura rushwa, ingekuwa ni vyema haraka apeleke ushahidi huo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kuwatuma wanasheria wake wakafungue kesi Mahakama Kuu ili iweze kutengua hukumu hiyo kupitia huo ushahidi wake kama anao na si kama anavyofanya hivi sasa kupayukapayuka kwenye vyombo vya habari,” alisema wakili huyo.
Aidha, alisema kwa mujibu wa kifungu cha 3 cha jedwali la 3 katika Sheria ya Usuluhishi ya Tanzania, Sura ya 15 ya mwaka 2002 kinasomeka hivi:
“Each contract state undertakes to ensure the execution by its authorities and in accordance with the provisions of its national laws of arbitrarily awards made in its own territory under the preceding articles”.

“Kwa tafsiri rahisi, kifungu hicho utaona tayari nchi imejifunga mikono na utekelezaji wa hukumu zinazotolewa na mahakama za kimataifa kwa sababu ni nchi yetu yenyewe imeridhia sheria na mikataba ya kimataifa.”
Alisema kwa hiyo maelezo ya Waziri Sitta ya kutaka Dowans isilipwe, ni kutaka kuishawishi serikali na umma kukaidi kutekeleza maamuzi halali chini ya sheria na mikataba ambayo serikali iliiridhia kuitii na kuitekeleza.

Aidha, alisema jambo jingine lililojitokeza wakati kesi hiyo ikiendelea baina ya Dowans na TANESCO ni TANESCO walitaka kujua wamiliki wa Dowans ni kina nani na Mahakama ya ICC iliona hoja hiyo ya TANESCO ya kutaka kumjua mmiliki haina umuhimu wowote katika mgogoro uliokuwa mbele yao na ikatupilia mbali, kwa sababu iliona hoja hiyo haina maana yoyote mbele yao.

“Kwa hiyo kwa kitendo cha Waziri Sitta kulianzisha suala hilo la kutaka kujua wamiliki wa Dowans wakati hoja hiyo tayari ilikwishatolewa uamuzi na ICC, kisheria hawezi kulianzisha tena jambo hilo la kutaka kujua wamiliki kwa njia anayoitumia ya vyombo vya habari.

“Kwa hiyo maelezo yote yanayoendelea kutolewa kuhusu hukumu hiyo ni kutaka kujinasua katika lawama wakati yeye na baadhi ya maswahiba zake enzi zile akiwa Spika wa Bunge ndio waliokuwa chanzo cha TANESCO kuvunja mkataba na Dowans, hivyo mwisho wa siku shirika hilo la umeme kujikuta likiburuzwa katika korti ya ICC.

“Na ifike mahala wananchi na vyombo vya habari na serikali itoke usingizini na ijiulize maswali yafuatayo kwamba Sitta hakuwepo kwenye usikilizwaji wa shauri hilo? Sitta hakuwa akijua kwamba TANESCO imefunguliwa kesi na Dowans katika Mahakama ya ICC?

“Kwa kuwa Sitta alikuwa mstari wa mbele kuzipiga vita Dowans na Richmond, ni wazi alikuwa akifahamu kwamba TANESCO imeburuzwa mahakamani na kama kweli Sitta ni mzalendo wa kweli na hana chuki binafsi katika hili ni kwanini hayo madai anayoyasema asingeiomba serikali imuweke kama shahidi wa upande wa TANESCO ili akatoe ushahidi anaousema kila kukicha kwenye vyombo vya habari?

“Amesubiri tayari shirika letu la umeme ambalo ndilo lilikuwa mdaiwa katika shauri hili limeshindwa kufurukuta kwenye kesi hiyo na tumetakiwa tulipe kiasi hicho kikubwa cha fidia ndiyo kila kukicha anazungumza kwenye vyombo vya habari kuhusu hukumu hiyo, tena ukitazama maoni anayoyatoa utafikiri si mtu aliyesomea sheria kabisa….naomba sana hasa serikali ipuuze ushauri wa Sitta kwani ni wazi kabisa anataka kuliingiza taifa kwenye matatizo mengine makubwa.

“Watanzania na huyo Waziri Sitta ambao hawajaisoma hukumu ile naomba niwaeleze wazi mimi nimeisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya mara saba, kama taifa kupitia hukumu hiyo tumeshikwa pabaya, hivyo hatuwezi kukata rufaa, isipokuwa tu kama tutathibitisha sababu zile mbili nilizozitaja,” alisema wakili Fungamtama.

Aidha, Fungamtama aliviasa baadhi ya vikundi mbalimbali vya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuacha kuzungumzia hukumu hiyo ambayo hata wengine hawajawahi kuisoma wala kuiona, kwani tayari kuna baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakiandika makala kwamba wakati kesi hiyo ikiendeshwa TANESCO haijawahi kuleta shahidi hata mmoja kutoa ushahidi.

Jambo ambalo Fungamtama alisema si kweli na linalenga kuhadaa umma, kwani majibu na nakala ya hukumu hiyo ambayo anayo inaonyesha TANESCO ilipeleka mashahidi watano na walitoa ushahidi wao.

Wakili huyo aliwataja mashahidi hao kuwa ni Subira Wandiba, ambaye ni Mwanasheria wa TANESCO, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Zabuni iliyotoa tenda kwa Dowans, Balozi Fulgence Kazaura, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Dk. Idrisa Rashid, Mhasibu Mkuu wa shirika hilo, Jamhuri Ngeline na Boniface Njombe.

Huyu mwanasheria wa Rostam au? Simwelewi kabisa hii kesi inamazingira yote ya rushwa kuanzai mkataba mpaka utetezi ulifaywa kwa kumsadia mdai anufaike. Hata mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa kwanza pale UDSM ataliona hilo. Kitendo cha Rost tamu na wenzake kujificha nyuma ya wakurugenzi batili ni kosa, ulitegemea mkataba gani kama wakurugenzi ni akina Rost tamu, karamu Magi na wengine wengi amboa ni washika dau ndani ya serikali na Tanesco. HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!
 
Lazima tumtafute nani alikosea na adhabu kali apewe, natamani ningekuwa nchina hapa tungenyonga faster.
 
Nimetoka kuangalia vionjo vya gazeti la taifa letu litalotoka, linasema wamiliki waliotajwa kuwa ndiyo wenye dowans ni marehemu! Itataja wamiliki halali na watakaopata mgao wakiwemo mfanyabiashara maarufu, viongozi wa serikalini na askari police ndiyo wataochukua mgao, source ni heading ya kichwa cha habari la taifa letu litalotoka,
 
Tuvute subra...ila nalo lisije pelekwa kwa pilato kama Mwananchi na Tanzania daima. Bravo
 
wakuu hili gazeti sijawahi kulisoma. Ni huru au la ccm. Yawezekana huyu jamaa analinadi
 
ha ha ha ha ha haaaaaa siasa za nchi hii zinanipa raha sana:welcome:to tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom